Clouds Entertainment inaimaliza Kili Music Awards?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Clouds Entertainment inaimaliza Kili Music Awards??

Discussion in 'Entertainment' started by Oloronyo, Apr 7, 2009.

 1. Oloronyo

  Oloronyo Member

  #1
  Apr 7, 2009
  Joined: Mar 29, 2009
  Messages: 80
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Erooo Wana JF? Natumaini ni wazima? Mimi kama mwananchi mwenye uchungu mkubwa na nchi yangu ya Tanzania naomba nitoe maoni kidogo kuhusu jambo ambalo tusipolivalia njuga litafanya hata hawa wafadhili wachache wenye moyo wa kuipigania sanaa yetu kuvunjika moyo kama si kuacha kabisa kufadhili kazi za sanaa za chipukizi wetu.
  Kwa ufupi ni jinsi ambavyo TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro kuandaa tuzo zinazowashindanisha wasanii wetu,tuzo hizi ziliasisiwa na Hayati James Dandu RIP na sasa ameaachia kina John Mhina wa The Tanzanite kusukuma gurudumu hilo.
  Kwa kweli ilipoanzishwa tuzo hii ilikuwa ni shughuli ya kusisimua sana na japo kipindi hicho sanaa ya music ilikuwa haina mwamko mkubwa kuliko sasa lakini iliweza kupita mabonde na milima kuweza kufika hapa ilipo.
  Nchini Marekani kuna Tuzo ijulikanayo kama Grammy Awards,tuzo hii ni maarufu sana hapa duniani na mara nyingi wasanii maarufu kabisa uhakikisha uwepo wao na kwa kweli hulinogesha tamasha hilo kwa jinsi mbalimbali ikiwemo mavazi,hotuba,vimbwanga vya hapa na pale na mara nyingi kama wao ni Nominees huwa wanahakikisha wanakuwepo kushuhudia tuzo hizo.
  Lakini si hapa Tanzania- Clouds Entertaiment ni kampuni kongwe katika tasnia ya burudani na kwa kweli wanastahili pongezi kwa hilo.
  Hivi majuzi walikuwa na matamasha yao waliyoita kwa jina la Shangwe 2009 aka TUGAWANE UMASKINI Uzinduzi wa Juma Nature na Ferooz katika miji mbalimbali na kwa kweli yalifana sana mfano la hapa Dar (Japo umeme ulikatika) Tanga,Dodoma na Morogoro huku wakijua siku na tarehe ya kutoa tuzo za Kili Music Awards baadhi ya wasanii waliokuwa wapate tuzo hizo,walikuwa nao katika hiyo tour ya Shangwe 2009 aka TUGAWANE UMASKINI wamiliki wa Clouds Entertaiment waliendelea na ratiba yao kama ilivyopangwa,na hivyo kufanya karibu tuzo nyingi zilizotolewa hapo Diamond siku ya tarehe nne mwezi wa nne kuchukuliwa na wawakilishi wa wasanii iliniuma sana kama mdau wa tasnia ya muziki. ni kweli kuwa watayarishaji wa Kili Music Awards hawako makini katika utoaji wa tuzo hizo mfano mwaka jana walimpatia tuzo Bushoke katika wimbo alioshirikishwa na Juliana Kanyomozi,Lakini Clouds Entertaiment mwaka huu wamefanya makusudi,Je hawa wafadhili TBL wakijitoa itakuwaje? Maana wasanii waliotakiwa kupata tuzo au Nominees wengi mlikuwa mko nao Morogoro na nakiri kusema HAKIKA HUU SI UUNGWANA!
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Apr 7, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,317
  Likes Received: 5,609
  Trophy Points: 280
  Lakini hata usa huwa wanatuma wawakilishi...hawawezi kujitoa sababu sapoti ni kubwa na marketing bab kubwa ya kileo chao...'Uomba udhuru ni kawaida ....mimi sioni cha ajabu pia kumbuka hao wasanii wanategemea. Sana ziara na matamasha kupata angalau kidogo maana album mmmm wabongo mnapiga ana copy fake na hawapati faida ila wakijaza uwanja hata wao nao wanapata hata hizo 1.mil wajipongeze kazi sanaa msuli kweli ku savaivu wajua hilo???
   
 3. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #3
  Apr 7, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Ruge unasemaje katika hili?
   
 4. senator

  senator JF-Expert Member

  #4
  Apr 7, 2009
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Sijajua vyema kama kupokea ile tuzo kulikuwa kuna ambatana na bahasha ya pongezi au ndo urembo tu(Niliona kama kila anaechukua zawadi anapitishwa kwa nyuma kule ,
  sijui kulikuwa na shoshote!!?)
   
 5. Oloronyo

  Oloronyo Member

  #5
  Apr 7, 2009
  Joined: Mar 29, 2009
  Messages: 80
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe kuhusu kupiga tamasha live na kupata hela kutokana na piracy lakini inakatisha tamaa sana wakati kuna kampuni inaamua kuwaenzi wasanii nyingine ambayo pia inasaidia wasanii inafanya tamasha siku hiyo hiyo, na kuwatuma wawakilishi kwa Tanzania bado ni mapema. Jamani Tuchukulie mfano Raisi Kikwete anawaandalia hafla pale Ikulu Wasanii wote waliofanya vizuri katika Kili Music Awards kisha wao wanatuma wawakilishi, Wenyewe wanaenda mfano kwenye kugawana umasikini Arusha au Mwanza. Je Raisi atathubutu kuwaandalia tena hafla Ikulu?
   
 6. S

  Semjato JF-Expert Member

  #6
  Apr 7, 2009
  Joined: Jun 26, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kwanza,hivi ile tour ni ya album ya shangwe ama kugawana umaskini?..
  hata hivyo sioni hoja yako ni ipi since wote ni wafanyabiashara tu..clouds na hao kilimanjaro!clouds hawakuwa na sababu ya kusimamisha biashara yao kuwapisha kili wafanye matangazo ya biashara yao,hakuna biashara ya namna hiyo popote mkuu..hasa kama clouds hawakutumika kutangaza hizo tuzo!by the way,natamani wajitokeze wadhamini wengine waanzishe tuzo zao nao,maana naona kili uzembe unazidi kila kukicha...
  wasalaam
   
Loading...