Clouds acheni kulaumu CAF kwani aliyefanya figisu ni Yanga hapa nyumbani na akafungwa

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,635
7,005
Niko sehemu namsikia Alex Lwambano akijaribu kuituhumu CAF kama walivyozoea kuituhumu TFF kuwa eti Yanga ametolewa kwa figisu figisu!

Hivi aliyefanya figisu hapa Tanzania ni nani kama sio yanga? Walifungwa wakiwa hapa nyumbani licha ya kuwafanyia figisu wanigeria wakawazuia key players watano wa Rivers United ambao hata mechi ya pili hawakuwepo.

Sasa nyie clouds kwa nini mnataka kujidai eti hamjui kuwa yanga alizidiwa?Acheni propaganda
 
Mkuu kibaravumba Hongera.

Kuwa kwangu shabiki ama philia wa YOUNG AFRICANS SC Kusinifanye niwe kipofu hata nisiyaone madhaifu yao.

Kuwa kwangu philia wa TIMU YA WANANCHI kusinifanye niyakumbatie hata yasiyo stahili.

Makosa na uzembe umefanywa na wao wenyewe, Mchawi yu miongoni mwetu kwa nini tumtafute nje yetu!?!!

Niliyaona na kuyakiri bayana SIKU YA WANANCHI kwamba kwa usajili huo, YANGA mwaka huu "tumepigwa".

Na ikiwa benchi la ufundi na kamati ya usajili havitashtuka basi mpinzani wetu SIMBA SC watatwaa kombe la ligi mara KUMI mfululizo.

Na zaidi ya hapo Klabu bingwa Afrika tutaendelea kuiona SIMBA SC ikifanya vema huku sisi YOUNG AFRICANS SC tukiboronga mwaka hadi mwaka au tukiendelea kuwangojea WATANI wetu tena WATUBEBE KWA MBELEKO kwenye michuano ya Klabu Bingwa Africa.
 
Yanga aijawai kuwa na ngumbalu Kama wewe, watu dizaini yako mko kwenye ile timu ya familia ya babra na mo sio yanga, akili zenu zinajulikana zilivyo nusu
 
Hatuwezi kufanana kimtazamo.

Si lazima uamini ninachoamini, Si lazima niamini unachoamini.

Mimi ni shabiki wa DAR YOUNG AFRICANS tangu 1998.

Nisipokuwa NGUMBALU, Mjanja na mwenye akili atakuwa nani?

Kama wote wakiwa na AKILI nani atamuongoza mwenzie?

Ukweli unachoma na pia unamuacha mhusika huru kama asiposhupaza shingo.

YANGA ikitokea kwa mfano wakapanga matokeo leo na wakashinda, Je, Na mimi nishiriki kufurahia michezo hiyo michafu badala ya kuonya na kukemea kwa sababu naipenda YOUNG AFRICANS!?!!

Tayari kumepambazuka.
 
Atatafutwa mchawi kila mahali lakini Yanga imetolewa kwa mambo mengi lakini nitaeleza machache yaliyokuwa ndani ya uwezo wao.

1. Pre season haikufanyika vizuri. Hakukuwa na sababu ya kuzurura Moroco na kurudi wakati wangetulia to Avic town wangefanya mazoezi yenye tija na yangewasaidia sana.
2. Uzembe wa uongozi na Hersi kwenye kufuatilia ITC kiasi wachezaji muhimu kama Djuma, Mayele na Aucho wakakosekana. Hili halizungumzwi kabisa na waandishi wala watangazaji sijui wamepewa nini. Na mbaya zaidi Djuma alikuwa mchezaji wa kwanza wa kigeni kusajiliwa lakini hakupata ITC katika muda muafaka.
3. Kuacha mechi na Zanaco Yanga haikupata mechi nyingine ngumu ya kirafiki. Walau viongozi wangejitahidi zingepatikana mechi nyingine mbili zaidi ya ile ya Zanaco.
4. Kushindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani kwenye mechi ya nyumbani dhidi ya Rivers. Yanga pamoja na mapungufu yao walikuwa na uwezo kabisa wa kuimaliza ile mechi hapa Dar tena kwa goli zisizopungua tatu.
5. Kukosena kiongozi wa kuituliza timu wakati wanafanyiwa figisu wakiwa Nigeria. Tunajua figisu ni kitu cha kawaida kwenye mashindano kwa nchi za kiafrika lakini ni kama vile Yanga haikujiaandaa na hilo. Kuna "clip" iltumwa mitandaoni kutoka Nigeria ikionyesha viongozi na watu wengine wasio viongozi waliokuwa wameambatana na Yanga wakibishana na wanaigeria mbele ya wachezaji kuonesha kuwa Yanga inaonewa. Na walienda mbali zaidi kufikia kusema kuwa hatuchezi mechi. Yale mambo yalitakiwa yafanywe na viongozi wachache tena mbalii kabisa ya macho ya wachezaji. Kwa namna moja au nyingine hili suala liliharibu sana saikolojia ya wachezaji kuelekea mchezo ule.
 
Wewe ndio umeeleza vitu vya maana.
 
Back
Top Bottom