Clouds 360 yamtangaza Antonio Nugas kuwa msemaji rasmi wa vivutio vya utalii mjini Chato - Geita

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,723
141,582
Meneja wa ubunifu Clouds media ndugu Ciza amesema mtangazaji wao Antonio Nugas atakuwa msemaji rasmi wa maswala ya vivutio vya utalii katika mji wa Chato mkoani Geita

Hayo yamejiri katika kipindi cha Clouds 360 on saturday ambapo Ciza alikuwa akihojiana na Nugas kuhusu mafanikio ya Chato.

Nugas amesema ataibrand Chato na vivutio vyake na kwa kuanzia ameandaa makala itakayorushwa hapo Clouds tv kwa muda wa mwezi mzima.

Nugas amewataka watanzania kuwahi fursa za uwekezaji kule Chato kwani miundombinu yake ni ya uhakika na rafiki.
Chato kuna International air port, mbuga nzuri, Stand ya kisasa ya mabasi, patajengwa uwanja mkubwa wa mpira wenye capacity ya watu elfu 45 ambao hata Barcelona wataweza kuutumia pia kuna uwezekano SGR ikapita pale kuelekea Muleba amemalizia Nugas.

Na mwisho kabisa Nugas amesisitiza uwepo wa viwanja vilivyopimwa kwa ajili ya ujenzi wa makazi kwa bei nafuu ya kuanzia sh laki sita tu.

Source Clouds tv!
 
Itangazwe tu kuwa jamhuri. Maana inaonekana hapo ndio nchi ilipo na si sehemu nyingine
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom