Clouds 360: Mahojiano na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, akifafanua mambo mbalimbali

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,735
6,292
"Hayati Magufuli alikuwa anafanya kazi sana. Alikuwa analala akiwa na usingizi tu kama hana basi alikuwa halali. Na asipolala hata sisi hatuwezi kulala".

"Rais Samia anafanya kazi sana. Ukiona anapanda ndege anashuka unaweza ukahisi ni maisha mazuri lakini hapumziki. Tuna bahati ya kuwa na viongozi wanaojitoa kwa ajili ya Watanzania, ni wachapakazi, wacha Mungu, wanawapenda wananchi wao na siku zote wanafikiria kuhusu Watanzania".

"Clouds ni vituo vya habari ambavyo nikitaka kuyaangalia mabadiliko kwenye sekta ya habari sitaacha kuitaja Clouds Media Group wanafanya kazi kubwa sana nataka niwapongeze."

"Hayati JPM aliacha miradi ambayo Mhe. Rais Samia alisema lazima imalizike na mingine ianze. Mfano Hayati JPM alianza mradi wa kujenga reli Dar to Morogoro na ilifika 86% ila sasa mradi umefika zaidi ya 92% na mwezi November treni itafanyiwa majaribio".

"Ndoto za Hayati JPM kuhakikisha kila kata ina maji, vituo vya afya, barabara hakuna kazi iliyosimama. Bil 23.8 kwa ajili ya elimu bure zinaendelea kutolewa na hakuna mtoto aliyeenda kutozwa ada hata baada ya JPM kufariki".

"Sheria haituambii tufungie magazeti inasema inaweza kutowapa leseni au kufuta leseni. Sasa hivi hatufungii chombo cha habari kinapewa leseni ya kufanya kazi natumaini vyombo vya habari havitavunja sheria kwa sababu hizi sheria zimewashirikisha wadau wa habari".

"Serikali ilikusudia kwenye tozo ya miamala na ile ya line za simu palikuwa panatarajiwa karibu Tril. 1.6 na Tril. 1 zilikuwa zinatakiwa zitoke kwenye miamala. Hizi tozo zilitakiwa ziende zikajenge barabara na vituo vya Afya huko Vijijini".

"Ile tozo ambayo Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba anaiita 'Tozo za Mshikamano' dhamira yake ilikuwa ni kwamba tuna tatizo kubwa la barabara Vijijini lengo Serikali inataka kuanza safari ya kujenga barabara za lami Vijijini" - Gerson Msigwa, Msemaji wa serikali.
 
Bora hata wangesema wanaitafta tilion moja ili wafumue mtaala wa elimu TZ

Tukishakua na werevu kitaaluma wa TZ wote kwakizazi hiki barabara zitajengwa tu mana serikali inayokua madarakani haiwezi kumpangia huyu mtanzania alipata elimu murwaaa mashuleni na vyuoni(elimu na ufumbuzi)

ndiyo hatuwezi kushuhudia kodi kama hizo (solidarity),teminoloji hizi zilitumika kudai Uhuru huko eg kuwasha mwenge mlima Kilimanjaro na ukamulike au kuangaza nuru kwenye Giza huko msumbiji,Burundi ,afghanistani (Mandela hatuwezi sema tuko huru bila afghanistan kua huru)

Tunakila kitu Uhuru ,utulivu hadi mwengewetu ukaenda kumulika huko heeee msomi mzima miaka 60 ya Uhuru unakuja nakodi kamuzi kwa mwananchi maskini mafuta ya taa koroboi moja hawezi kununua eti kodi yamshikamano


My brother hili usirudie tena.nikweli sisi nimazoba ilatambueni kadiri mnavoendelea kutugusa vipofu sisi wakati wakula ndipo mnatutawanyia mwanga


Polisi mnaowategemea kumbukeni hatawao hili limewagusa msije mkawategemea kumbe nawao wakajichanganya nawananchi KUDEMKa na ndgzao...


Kutereza si kuanguka
 
Back
Top Bottom