Clip ya Video ya Bw. Lwakatare (mtazamo tofauti) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Clip ya Video ya Bw. Lwakatare (mtazamo tofauti)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by R.B, Mar 14, 2013.

 1. R.B

  R.B JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2013
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 6,129
  Likes Received: 1,060
  Trophy Points: 280
  Nashauri viongozi wa siasa wawe makini na wanachama wageni au wanaohamia bila sababu na bila kuwachunguza wanawavisha madaraka makubwa.

  Lwakatare alifukuzwa CUF baada ya CUF kulalamika siri za ndani kuvuja.

  Nasikitishwa na viongozi wa CHADEMA kumkumbatia na wakati wakijua wazi. Ni kweli ile clip unamuonyesha.

  Tuachie jeshi la polisi litende haki yake
   
 2. a

  andrews JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2013
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ok tutaona kama anahusika ashitakiwe
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2013
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mikakati ya kifisadi kama hii hufa hata kabla ya jua kuzama.

  Je, ni nani mlalamikaji kwa Lwakatare; afisa mwandamizi wa CHADEMA huyu ili sote hapa tupate kumtambua na hata kumuuliza maswali mawili matatu hivi.

  Je, mlalamikaji ni Nape, Mwigulu au Mzee Wassira mwenyewe kabisa kujue?
   
 4. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2013
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Nimeangalia clip ya video ya Bw. Lwakatare zaidi ya mara 5, nilichobaini and i stand to be corrected, kwa kiwango kikubwa clip ilie ilivyoandaliwa inaonyesha kweli kwa sauti ni Bw. Lwakatare, kama mtaanagalia katika clip nyingine mfano ile ya Obama iliyowekwa humu utaona tofauti kubwa katika sauti yake halisi na ile ya kubambikizwa maneno. Ilivyo clip ya Lwakatare na teknolojia yetu, natamani sana kuamini alitengeneza mwenyewe, ila swali la msingi ni kwa sababu zipi alitengeneza na je ni kweli yeye ni mtu hatari ni maswali ya kuendelea kujiuliza.

  Hisia kubwa inanijia ni kuwa upo uwezekano pia Bw. Lwakatare alinunuliwa kutengeneza hiyo picha na watu ambao pia malengo yao hatujui hadi leo na ni suala ambayo yeye anaweza kuchunguzwa na kuelezea ukweli. Cha msingi uchunguzi wa kweli ufanyike bila kuendelea kubahatisha kama ambavyo siku zote tunafanya ili kubaini genge hili la wauaji ambalo sasa ni wazi limejikita zaidi katika mrengo wa maslahi ya kisiasa.

  Tafakari bila ushabiki wa kisiasa na chukua hatua, tusipotafuta majibu ya kweli hata wale ambao wanadhani ni sehemu ya genge hilo in a long run hawako salama.
   
 5. K

  KibopaII Member

  #5
  Mar 17, 2013
  Joined: Mar 8, 2013
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baadhi ya wagonjwa wa UKIMWI wana kasumba ya kutokubali kwamba wanaumwa Ukimwi, na huu ndio huwa mwanzo wa mwisho wao, maana bora wangekubali wakanywa dawa za kurefusha maisha wangeweza kuishi muda kidogo kulinganisha na juhudi zao za kukataa kwamba wameathirika.

  Ndivyo ambavyo chama nilichodhani kingekuwa chama mbadala ya CCM iliyochoka kingekuwa, yaani CHADEMA. Bahati mbaya sana Chadema kama mgonjwa wa UKimwi asiyetaka kukubali kwamba ameathirika badala yake anabaki kuamini kuwa KAROGWA ndio mwanzo wa mwisho wa Chadema!

  Hata kama viongozi wa Chama hichi walikimbia shule wengi na wengine shule zao za magumashi ,inahitaji degree ngapi kujifunza kukubali ukweli hata kama unauma? Ugonjwa huu wa kukataa kwamba unaumwa wakati unaumwa na kudhani unarogwa utakizika Chama hichi kilichoanza kuonyesha matumaini...na hapa CCM na wapambe wao watakuwa wamefanikiwa sana.

  Hivi inahitaji degree ngapi kujua kuwa Rwakatare ambaye siasa zake za upinzani alianzia CUF na wakati huo CUF ilikuwa na tabia zinazoonekana leo CHADEMA? Wakati CUF ikiwa na Rwakatare ndo ilikuwa chanzo cha vurugu za kisiasa nchini,mara kuingiza visu, mara majambia, mara maandamano, mara watu kuuawa na wengine kupoteza viungo vya miili yao!! Sasa Rwakatare huyuhuyu yuko Chadema leo, Chadema wameiga tabia zilezile zilizowamaliza CUF na wakadhani Chadema wao watakuwa na muujiza wa kuishi.

  Dawa hapa nikujua mmeteleza na kuamka sio unateleza unabaki chini unalalamika!!
   
 6. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2013
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,909
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Hakuna cha maana ulichoandika mleta mada
   
 7. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2013
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,010
  Likes Received: 607
  Trophy Points: 280
  Kuna ka-point ka kuchukua hapo!
   
 8. K

  Kageuka JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2013
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamaa waliambiwa madhara ya oil chafu wakapuuza sasa yanawatokea puani, wanaanza oooh CCM ndo wamepanga. Kama kweli CCM wamepanga haya basi wamewazidi kwa mbali sana,vita hii Chadema hawaiwezi kabisa...Rwakatare apigilia msumari wa mwisho kweli jeneza la Chadema.
   
 9. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2013
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,828
  Likes Received: 251
  Trophy Points: 180
  kibopa unaishi na ndoto za chama kushika hatamu.ccm ni maiti tayari haiwezi fufuka. Mliosalia na mtindio wa ubongo mnajitahidi ku survive kwa kutumia mbinu za kitoto ambazo sasa zinawatokea puani.mtoa mada kajiunge na shule maalum upate kuondolewa huo mtindio
   
 10. K

  Kageuka JF-Expert Member

  #10
  Mar 17, 2013
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rwakatare aliacha lini Usalama wa Taifa wa CCM? Na kwanini CCM mpaka sasa hawajasema kitu? Hatuoni tunahangaika na magamba tu hapa?.......Tafakari chukua hatua!!!!!!
   
 11. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #11
  Mar 17, 2013
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Nimeishia katikati kusoma baada ya kutokuona chochote cha maana zaidi ya ujinga mtupu! Labda ni Ma-CCM wenzio a.k.a Division 0 ndio mnaelewana.
   
 12. K

  Kageuka JF-Expert Member

  #12
  Mar 17, 2013
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sema ukweli imebidi ukimbie selo kumsaidia gaidi aka mtekaji aka Rwakatare kubeba mdondo...tena umechelewa utakuta kala kibano cha kutosha...... wahi bhana
   
 13. m

  majebere JF-Expert Member

  #13
  Mar 17, 2013
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,494
  Likes Received: 528
  Trophy Points: 280
  Rwakatare ni wa bukoba, jamaa alie weka hiyo video ni bukoba boy..
   
 14. Mkoroshokigoli

  Mkoroshokigoli JF-Expert Member

  #14
  Mar 17, 2013
  Joined: Dec 20, 2012
  Messages: 14,418
  Likes Received: 2,500
  Trophy Points: 280
  hapo kwenye blue,akili zako na mahita nadhan mlitunukiwa siku moja na mungu
   
 15. K

  Kageuka JF-Expert Member

  #15
  Mar 17, 2013
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kanisa gani linalopokea watekaji na watesaji wa wanaopinga hoja zako???? Naomba ielekeze ili Rwakatare akitoka kesho kwa dhamana awe anakwenda kusali pls
   
 16. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #16
  Mar 17, 2013
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  ...Duh! Kweli Bado tuna Safari Ndefu. Yaani wewe Yule bwana aliyekuwa na Magwaanda na Kitambi alipouza sura kwenye TiiVii na kuonyesha Visu vyenye Rangi zinazpshabihiana na Rangi za Bendera ya CUF na kudai kuwa vimeingizwa Nchini na CUF, ULIMUAMINI????? Pole.
   
 17. JAKOBO

  JAKOBO JF-Expert Member

  #17
  Mar 17, 2013
  Joined: Jan 28, 2013
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wewe cha maana unachokiona hapo nikipi? au ndio kurithi ile tabia za mabwanazako kule Dodoma kila kitu naunga mkono hoja? kweli ukiwa Ccm ni laana tosha,mawazo yenu niushirikina tu kama kawaidayenu kwa akina mwakyembe,mwandosya,unga bungeni mkijiandaa kupika chapati.Mie napita tu sichangii sana kwa wapumbavu kama wewe!
   
 18. THE BIG SHOW

  THE BIG SHOW JF-Expert Member

  #18
  Mar 17, 2013
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 13,890
  Likes Received: 1,777
  Trophy Points: 280
  Ofcourse siasa ni propaganda,na kwa kweli tunaziona na kusishuhudia propaganda hizo,

  ila yote kwa yote hakuna marefu yasiyo na ncha,pia siku zote kwenye haki na batili.batili siku zote huwa ni yenye kujitenga,

  Tambueni ya kwamba ukweli ukidhihiri kuhusu suala hili la LWAKATARE,basi picha litageuka kuwa mbaya sana kwa upande pandikizi wa suala hili,,

  yetu macho na maskio tuh..
   
 19. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #19
  Mar 17, 2013
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35

  Omba sana Mungu wako, ugonjwa huo usije ukakupata - unanyanyapaa wagonjwa kuburudisha nafsi yako iliyojaa kiu ya kisiasa. Ebu jaribu kuunganisha mwanzo wa stori yako na kichwa cha habari, vina uhusiano wowote?

  Twende mbele zaidi, waweza kutusaidia kufahamu hao majambia na visu vilivyoletwa na CUF, viliingizwa nchini lini, invoice ipi ilitumika kuviagiza, vilishushwa toka meli ipi, vilipokelewa na nani, vilisambazwa mikoa gani, ni delivery note namba ngapi iliyovifikisha nchini; na serikali ilikusanya VAT kiasi gani kwa uagizaji huo wa visu/majambia.

  Duh, taifa linaelekea kubaya, kama ndo tumeamua kuwa nukushi bila kutumia bongo zetu kuchakatua, ni taifa la aina gani ili; jamani, hata kama umekunywa maji ya bendera ndo kiasi hiki. Hata kama minyoo ya tumbo inafaidika kutokana na propaganda, ndo ziwe za kabila hii. Oooh! taifa la kufikiria kwa style ya mlegezo halitatufikisha ktk nchi ya ahadi, tafakari.
   
 20. K

  KibopaII Member

  #20
  Mar 17, 2013
  Joined: Mar 8, 2013
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmesha mwaga mdondo wa MTEKAJI wenu au ndo mmeshamtelekeza?
   
Loading...