Wanajukwaa Salaam kwenu.
Juzi nilikutana na Vijana wanne wanaosoma Clinical Officers Training College - Lindi (COTC). Pamoja na story zingine lakini pia nilivutiwa na hasa story kadhaa Zifuatazo:-
1. Mwanafunzi kusoma kwa miaka 7 kwa kukamatwa kwenye somo moja linalofundishwa na Dr. Mmoja sababu ya chuki. Kwa kawaida chuo kile huwa kina Train officers kwa level ya Diploma kwa Miaka 3.
2. NACTE kutoa cheti kwa mwanafunzi lakini Bado yupo darasani na wiki hii amefanya mtihani wake.
3. Wanafunzi wa mwaka wa tatu kuzuiwa kufanya mtihani wao wa mwisho na wanafunzi kukosa namba za NACTE bila kujua tatizo
------------------------------
Clinical Officers Training Collage (COTC) Lindi na Uongozi wake.
MKUU WA CHUO - Dr. KATISA.
MLEZI WA CHUO - Dr. AFRED MAGANI.
ACADEMICS - Dr. MBEZI
Iko hivi:;
Chuo Cha COTC Lindi
Kwa sasa chuo hicho cha COTC Lindi wanafunzi wako kwenye mitihani yao ya mwisho kwa ajili ya kumaliza course zao za mwaka wa tatu na kusubiria matokeo yao na kupatiwa vyeti vyao maisha yaendelee.
Kwa kawaida kwenye hizi collage huwa namba za mitihani zinatoka NACTE, baada ya kuhakiki vyeti vya O-level wanavyo submit wakati wa kujoin chuoni. Utaratibu huu huwa Ni kuazia mwaka wa Kwanza. Sasa wanafunzi zaidi ya 80 wamekosa namba za kufanyiwa mtihani huo kutoka NACTE huku wachache wakipata namba zao tena wa course moja.
kimsingi wanachuo walipewa namba usiku wa kuamkia siku ya kuaza mitihani yao ya mwisho. Hivyo wachache ndo waliopata na wengine kukosa namba. ilipofika siku husika wengi waliaza kuranda nje ya chumba Cha mtihani. Ambapo wasimamizi walipouliza waliambiwa kwamba hawajapata namba.
Wanafunzi waliamua kuuliza kwa Dr. Alfred Magani ambaye ndiye Mlezi wa chuo. Aluwajibu hawatafanya mtihani Hadi mwezi February mwakani sababu hawajamaliza ada ya shule pamoja malipo mengine. Na Kuna wengine hawapewa namba kwa kuwa usajili wao haujakamilika? Wanafunzi waliamua kumfuata mkuu wa chuo Dr. Katisa ambaye baada ya kuona kunataka kutokea shida aliamuru kwamba wapewe nafasi ya kufanya mitihani yao kwa namba walizofanyia mwaka wa pili wa masomo yao.
Kuna mwanafunzi aliwahi kuhoji na kutaka kuoneshwa matokeo yaliyotoka NACTE maana alikuwa anaona si kweli somo hilo kukamatwa Kila wakati akanyimwa. Na ndo hapo ilipoaza chuki baina yake na huyo Dr. Afred Alitamka na atamkomesha.
Kweli ikawa hivyo Kila mwaka lazima afanye somo hilo Kama sup, na hata sasa kwenye mitihani ya mwaka wa tatu amelazimika kufanya kipolo Cha mtihani wake wa nyuma ila mitihani yake ya mwaka wa tatu maana yake atafanya mwezi wa sita mwakani 2020!
Sasa wakati anaendelea kusoma Kuna siku aliingia oficn akaona cheti chake na vyeti vya wanafunzi wenzie wanne ambao miongoni mwao walishaacha chuo kwa kukosa ada baada ya kuambiwa wanapaswa kurudia mwaka na kulazimika kulipia ada na hawakuwa nazo hivyo wakaondoka.
Na alipoona alimfuata mlezi wa chuo na kumueleza kwamba ameona cheti chake Cha kuhitimu chuo lakini hajawahi ambiwa na anahitaji cheti chake. Dr. Alfred hakukataa ila alidai kwamba hatapewa cheti lakini lazima alipie Tsh 380,000/= ndo apewe. Alipouliza deni la kitu gani ikiwa alishalipa mwaka ule alioofanya mitihani ilifanya NACTE kutoa cheti hicho? Aliambiwa Kama hataki aendelee kusoma. Maana yake huyo kijana Hadi mwaka huu anatimiza Miaka 7 masomoni kwa hoja za kukamatwa kwenye mitihani.
Aliamua kumfuata mkuu wa chuo na kumueleza haya lakini Cha ajabu naye mkuu wa chuo alimueleza kwamba Kama cheti kimetoka Basi NACTE walikosea kukitoa cheti hicho. Hivyo hapaswi kupatiwa. Lakini kwa Mlenzi wa chuo anachotaka Ni laki tatu na themanini apatiwe cheti chake.
Story Ni ndefu Sana Ina kadhia nyingi na Ina rushwa za ngono na fedha kwa baadhi ya Dr. Wanaofundisha kwenye hicho chuo. Ila mie naomba kujua Mambo machache ambayo ninajiuliza!
1. Hivi kweli NACTE wanaweza kutoa cheti Cha ku satisfy elimu ya mtu bila uhalali?
2. Kama kweli NACTE walitoa cheti Je mitihani aliyofanya Miaka miwili wamesahihishaje? Hawakujua na hawana kukmbukumbu ya kijana huyu kwamba alishamaliza elimu yake na kupatiwa cheti?
3. Kama wanafunzi zaidi ya 80 wamefanya mitihani yao kwa namba zao walizotumia mwaka wa pili wakati huo wengine Wana namba mpya, Je watapata matokeo yao kweli? Je namba zao hizo zilizokwisha tumika zinatambulika tena NACTE kwa mitihani hii ya mwaka wa 3?
-------------------------
Humu ndani Ni jukwaa la the great thinkers naamini mtashauri au mtasaidia njia ya kuwasaidia wanafunzi Hawa.
Kuna wengine walikwenda Hadi wizarani walikutana na Dr. Ndimila Wambura kulalamikia madhira hayo wanayofanyiwa chuoni. Majibu waliyopewa hayakuridhisha:-
Waliajibiwa hivi "Mnachezea nauli za kuja hapa, mnatakiwa Mkae hata Miaka 10 kwani chuo si mlikwenda kwa miguu yenu?"
Wanajamvi wenzangu naomba kuwasilisha!!!!