Climate Change: Nchi za Kiafrika, hususan Tanzania tuwe waangalifu na njama pana zaidi

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,314
24,173
Katika kuongea na wenzetu wana siasa Ulaya na Marekani, ni muhimu kutazama tatizo lolote kwa uwigo mpana zaidi.

Wakati wa utumwa , waafrika walichukuliwa kuwa kama wanyama wa kazi, kama punda na farasi.

Ulaya na Marekani walipo ingia Industrial revolution ,sasa nguvu kazi iliyotumika kwa miaka 400 sasa ikawa haihitajiki.

Ati sasa ndio wakajitokeza wenzetu huko ati wanawahurumia waafrika.
Nguvu kazi sasa ni ya mashine, ambazo zimetumika kwa karibia miaka 200 sasa.

Kwa vile mashine zinatumia malighafi nyingi, ugomvi wa makoloni ukaingia, Ulaya haswa.
Walipotosheka sehemu za kuvuna maliasili sasa wakubwa hawa wakajidai ati kuyapa uhuru makoloni.

Mpaka sasa mashine zao zinazidi kufurumua moshi, taka na magonjwa kutokana na mazingira machafu.

Wenzetu wamekuwa na tabia ya makusudi ya kuondoa ngazi kwa maendeleo ili wao wabaki juu kutuendesha watakavyo.

They want all the rime to be in a controlling position.

Hiyo ni Geo Strategy, maana nchi za 3rd World nazo zimeanza kuendelea kwa kasi.

China, India, Brazil na South Africa zimeanza kupiga hodi na kupata maendeleo ya juu.

SASA: Yaingia Climate Change.

Hili ni tatizo mahsusi yaliyosababishwa na nchi za magharibi kwa zaidi ya 90%.

Nikitengemea wao Magharibi waanze kubomoa maviwanda vyao vinavyozalisha sumu kwa 90%.

Kuzishirikisha nchi za dunia ya tatu kama Tanzania ati tuachane na Mchuchuma, ni kukubali kujifunga goli huku tunaona.

Tusikubaliane na unyonge huu wa kuingizwa chaka kila wakati.
 
Si Mchuchuma tu, bali pia ile gas ya Mtwara; bomba la mafuta toka Uganda na hata kupunguza idadi ya mifugo ambayo nchi yetu inajivunia. Hawa Mabeberu na wale Wajamaa wakubwa ndio wanaongoza kwa uchafuzi wa mazingira na hata layer ya Ozone huko juu. Jiulize kwa nini yule Trump aliamua kujitoa kabisa toka Paris Club? Jibu ni rahisi. Aliona kuendekea kufuata makubaliano ya Paris kutaifanya nchi yake ianguke kiuchumi wakati yeye alilenga "Make America Great Again". Hao Wajamaa hata hawakwenda kushiriki COP26 huko Uingereza.
 
Ni kweli kabisa.
Hata China na Urusi zimekataa msimamo huo wa Magharibi.
 
Katika kuongea na wenzetu wana siasa Ulaya na Marekani, ni muhimu kutazama tatizo lolote kwa uwigo mpana zaidi.

Wakati wa utumwa , waafrika walichukuliwa kuwa kama wanyama wa kazi, kama punda na farasi.

Ulaya na Marekani walipo ingia Industrial revolution ,sasa nguvu kazi iliyotumika kwa miaka 400 sasa ikawa haihitajiki.

Ati sasa ndio wakajitokeza wenzetu huko ati wanawahurumia waafrika.
Nguvu kazi sasa ni ya mashine, ambazo zimetumika kwa karibia miaka 200 sasa.

Kwa vile mashine zinatumia malighafi nyingi, ugomvi wa makoloni ukaingia, Ulaya haswa.
Walipotosheka sehemu za kuvuna maliasili sasa wakubwa hawa wakajidai ati kuyapa uhuru makoloni.

Mpaka sasa mashine zao zinazidi kufurumua moshi, taka na magonjwa kutokana na mazingira machafu.

Wenzetu wamekuwa na tabia ya makusudi ya kuondoa ngazi kwa maendeleo ili wao wabaki juu kutuendesha watakavyo.

They want all the rime to be in a controlling position.

Hiyo ni Geo Strategy, maana nchi za 3rd World nazo zimeanza kuendelea kwa kasi.

China, India, Brazil na South Africa zimeanza kupiga hodi na kupata maendeleo ya juu.

SASA: Yaingia Climate Change.

Hili ni tatizo mahsusi yaliyosababishwa na nchi za magharibi kwa zaidi ya 90%.

Nikitengemea wao Magharibi waanze kubomoa maviwanda vyao vinavyozalisha sumu kwa 90%.

Kuzishirikisha nchi za dunia ya tatu kama Tanzania ati tuachane na Mchuchuma, ni kukubali kujifunga goli huku tunaona.

Tusikubaliane na unyonge huu wa kuingizwa chaka kila wakati.
Uko sahihi kabisa kwenye hoja yako. Ukiangazia mkutano wa mazingira uliomalizika hivi karibuni, Chief wetu Hangaya ameenda kuomba ufadhili badala ya kuwanyoshea kidole wanaochafua mazingira bila kupepesa macho.

Kama tumekuja na mbinu ya kulipwa fidia ili tusiguse akiba yetu ya makaa ya mawe kule Mchuchuma, basi hakuna haja tena ya kuendeleza mradi wa makaa ya mawe wala kujenga reli ya SGR kule Mtwara.
 
Back
Top Bottom