Michael Amon
JF-Expert Member
- Dec 22, 2008
- 8,775
- 3,610
- Thread starter
- #41
wakati nasoma sekondari shule yetu ilikuwa nzuri sana kwa drama, tulikuwa na mashindano ya drama na shule za wilaya ile. tulikuwa na mwalimu alikuwa mtunzi mzuri sana wa michezo, yaani hata tukiigiza sasa tunaweza tukawa wazuri sana kuliko haya masinema yao.
Nilikuwa pia actor mzuri sana. nakumbuka yaani ni kama somo. mnapewa scripts, unaisoma mwezi mzima, then mnaanza mazoezi, ni kila siku muda ambao wenzenu wanaenda kazi za nje nyie zoezi kwa zaidi ya miezi, yaani mpaka muende mashindano ni ndani ya miezi kadhaa ya kufundishwa na ku-practice. kuna vipaji, yes, lakini kufanya kitu kizuri kunahitaji kufundishwa.
sasa aembu jiulize ni wasanii wangapi wa hapa bongo wamekwenda shule kujifunza sanaa ya uigizaji? Asilimia kubwa wanaishia kudandia treni tena kwa pembeni wala sio kwa mbele tena.