Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,193
- 25,504
Hebu vuta picha kwenye sherehe za kitaifa: kabla hata ya sherehe husika mhusika analetewa mualiko nyumbani kwa bashasha na heshima kubwa. Ukumbini au uwanjani, mhusika anaketi kwenye sehemu ya 'wakubwa na wazito' wenzake kufuatilia kinachojiri huku akichagiza na vistori vya hapa na pale na wakubwa na wazito wenzake.
Kwa pembeni, kuna gari ya maana inamsubiri mhusika. Mhusika anaitwa kwenye mimbari kutoa kaneno kadogo akishangiliwa na wahudhuriaji. Picha za pamoja baada ya shughuli hufuata huku stori zikinoga na wenzake wakiwa wanakumbushana raha na karaha za kazini na hata majuu safarini. Wanacheka na kugonga mikono.
Muda wa misosi unawadia. Misosi na vinywaji kadiri ya avitakavyo vinawekwa mbele ya mhusika. Akiwa nadhifu, mhusika anapita kwenye mstari wa misosi huku akiendeleza vistori vya hapa na pale na wenzake. Anachukua kadiri ya atakavyo na kinywaji akipendacho. Anakula na kunywa atakavyo. Stori tamutamu zinaendelea.
Baada ya yote hapo, gari zuri na la kifahari linasogea. Anawapungia marafikize na kuingia kuelekea nyumbani, ofisini au mahali pengine. Dereva anaondoa gari na wanatokomea kuelekea huko. Raha sana. Ni mambo ya 'classes' hayo. Ndiyo hasa yanayofanya wanasiasa wasahau kwa muda hata shida za wanachi wao.
Ni raha zinazomsukuma mhusika kuhama au kuhamia chama cha kisiasa. Kuwa karibu na marafiki zake na heshima yake ni jambo muhimu. Kuwa sehemu ambayo una uchaguzi wa maneno ili ushangiliwe ni burudani tosha. Kuwa kwenye tabaka lako ni jambo la heri sana. Nani aliye siasani hataki raha hizi? Wananchi myajue haya na kukubali matokeo wakati mwingine.