Clarence Seedorf atimuliwa Cameroon

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,373
217,434
Waziri wa Michezo wa Nchi ya Cameroon Profesa Kombi ametangaza kwamba Clarence Seedorf hatoendelea kuwa kocha wa Timu ya Taifa hilo kuanzia sasa .

Bado haijatangazwa atakayetwaa nafasi yake
 
Naona kuna kasumba inataka kutamalaki katika soka la Africa;ukiona yule anatimua kocha na wewe timua wako.

Hivi unamtimua Clarence Seerdof kwa kosa lipi hasa?Hatua waliyofika kwa kikosi kile tia tia maji hawajatosheka?au walifikiri wataingia fainali tena na kikosi kile kibovu?

Hebu angalia maandalizi ya timu, hebu kumbuka mgomo uliokuwepo kabla hawajaenda Misri, na kisha usisahau kujiondoa kikosini kwa wachezaji waandamizi kabla ya kupaa kwenda Misri;akina Joel Matip, Alain Nyom,n.k NA HAYO YOTE YAMESABABISHWA NA FECAFOOT halafu mzigo wa mavi anaangushiwa Seerdof! Eto'o alishaingia mgogoro kitambo sana na viongozi wa FECAFOOT kwa sababu ya mambo yao ya 'Kiswahili'.

Chama cha soka Cameroon jichunguzeni wenyewe,na nyie TFF ya Bongo mjichunguze pia NA MUWAJIBIKE KWANZA KABLA YA KUMUWAJIBISHA YEYOTE.
 
Back
Top Bottom