Ciproflaxin ya India inatibu Typhoid vizuri kweli??? !!!! mbona dalili ni zile zile

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,928
3,225
Wiki 2 zilizopita mke wangu alimaliza dozi ya ciprofaxin za India.

Sasa nashangaa anaumwa tena, dalili zile zile.

naomba msaada wa dawa zipi efective za kutibu typhoid.

je, baada ya kumeza dawa za typhoid, inatakiwa muda gani upite ndo mtu ameze tena??
 
Baada ya wiki tangu amalize cipro, afanye stool culture and sensitivity test. Hapo utapata ukweli kama bado hao bacteria bado wapo au wameisha
 
Baada ya matibabu unahitaji vipimo. Pia kwa suala la Typhoid, inashauriwa ukapime hospitali au dispensary zenye uhakika vinginevyo unaweza kuambiwa unayo kumbe hakuna. Mara nyingi vipimo vyake uchukua muda mrefu.
 
Anyway,kwani shemeji ana dalili gani?
May be ametumia dawa za typhoid wakati tatizo lake sio hilo.Mara nyingi watu wamekuwa wakitumia dawa za typhoid bila sababu.
 
Nchi hii ina Cipro ya Ujerumani-inauzwa laki kwenda mbele nazandia zinaanzia 2000 mpaka 15000!Ebu tuwekane sawa hapa effectiveness yahizi dawa nisawa kweli?
 
Nchi hii ina Cipro ya Ujerumani-inauzwa laki kwenda mbele nazandia zinaanzia 2000 mpaka 15000!Ebu tuwekane sawa hapa effectiveness yahizi dawa nisawa kweli?
Pamoja na kukubali kwamba cipro za Ujerumani ni ghali, lakini kwa Tanzania hizo cipro zinazodaiwa kuwa za ujerumani zinaweza pia kuwa fake. Hatuna njia ya kusema kwa uhakika kama ni genuine. Unakumbuka zile Metakelfin fake za ITALY?
 
Nchi hii ina Cipro ya Ujerumani-inauzwa laki kwenda mbele nazandia zinaanzia 2000 mpaka 15000!Ebu tuwekane sawa hapa effectiveness yahizi dawa nisawa kweli?

Mkuu kama ni effectivenes bei sio factor.Kwa sababu ikiwa hizi za bei ya chini bado zinatibu watu na wanapona,then kwa nini utumie kiasi kikubwa cha pesa kwa jili ya dawa iliyotoka Ujerumani?
 
Wiki 2 zilizopita mke wangu alimaliza dozi ya ciprofaxin za India.

Sasa nashangaa anaumwa tena, dalili zile zile.

naomba msaada wa dawa zipi efective za kutibu typhoid.

je, baada ya kumeza dawa za typhoid, inatakiwa muda gani upite ndo mtu ameze tena??

Fanya mpango apime kwanza kisha ndo unaweza ukapata jibu kama dawa zimefanya kazi au la. Ila kwa uzoefu wangu nimegundua kuwa dawa za kutoka india,kenya au tz hazitoi matokeo matokeo mazuri kwa walio wengi kwenye tatizo la typhoid.

Cipro nzuri ni za kutoka europe,egypt,jordan,korea ambazo ndo zinapatikana kwa wingi hapa nchini. Pia mwambie huyo mgonjwa awe makini na kachumbari za mtaani kwani ni moja ya vyanzo vikubwa vya typhoid
 
Mimi nilizitumia kabla ya Christmas last year nikapadhani nimepona, ilivyopita 2 weeks nikaumwa tena, this time nikadhani ni malaria kupima sina nilipotaka kupima typhoid walisema haitaonekana kwa kuw 3 months haijapita.
Nilipata dozi upya nimepona
 
Kuna matibabu ya biashara nchi hii. Kati ya vituo vya tiba kumi utakavyo pima sana sana vya binafsi ni kimoja tu au hakuna kabisa watakaokupa jibu la kuwa huna typhoid.
Hii ndio ilipelekea wizara husika kuweka mipaka ya kupima typhoid yaani kuanzia hospitali za wilaya hadi ya taifa. Wengi wanauza dawa hilo litambue kaka.

Hata hivo mtu akiugua typhoid haina ubishi kuwa amekula kinyesi cha mwingine maana vimelea vya typhoid hutoka kwenye mwili wa mtu alienavyo bila kuwa na dalili za ugonjwa (carrier) kupitia haja kubwa na endapo hicho kinyedi kitachanganyika na maji au chskula chochote aliyevimeza ataugua. Hivo basi tahadhari ya kula vyakula usivyokuwa salama na pia kunawa mikono baada ya kujisaidia kabla ya kuandaa chakula ama kula ni muhimu sana kujikinga. Kinga ni bora kuliko tiba.

Ushauri wangu nenda hospitali zilizoruhusiwa kupima ili ukadhibitishe kabla ya kubugia madawa. Lkn pia kupenda vya nje nako tatizo mbona dawa zinazotengenezwa hapa TZ ni nzuri na zinaponya vizuri.
 
Nenda kanunue top cef tablet ameze vidonge tano kwanza kisha anakaa siku saba kisha tano halafu baada ya siku saba akapime
 
Mimi nilizitumia kabla ya Christmas last year nikapadhani nimepona, ilivyopita 2 weeks nikaumwa tena, this time nikadhani ni malaria kupima sina nilipotaka kupima typhoid walisema haitaonekana kwa kuw 3 months haijapita.
Nilipata dozi upya nimepona

Ulikuwa unahisi dalili gan mkuu
 
Back
Top Bottom