JamiiTalks CIPESA na Jamii Media waendesha mafunzo ya siku 2 ya Sera ya TEHAMA na Uhuru wa maoni mtandaoni

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,806
11,968
Kampuni ya Jamii Media kwa kushirikiana na CIPESA (Collaboration on International ICT Policy for East and Southern Africa) Wameendesha mafunzo juu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wakiwashirikisha wadau mbalimbali kutoka kada ya Habari na Sheria.

20170711_091448.jpg

Juliet Nanfuka kutoka CIPESA akielezea uhusiano kati ya TEHAMA, Haki za Binadamu na Demokrasia.

TEHAMA ni kifupi cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, inamaanisha teknolojia za kisasa inayowezesha watu kupata taarifa na mawasiliano kwa kupitia intaneti, kompyuta, simu na njia nyingine zinazofanana na hizo

Katika ulimwengu wa sasa TEHAMA inazidi kuwa ya muhimu na mataifa mbalimbali yamefanya mapinduzi kwenye nyanja mbalimbali kwa kutumia TEHAMA, na serikali ya Tanzania inatambua umuhimu wa TEHAMA kwenye kuleta maendeleo yake kama kurahisisha njia za utumaji na upokeaji fedha, na kuleta mabaoresho kwenye utoaji huduma katika sekta binafsi na serikali

IMG-20170711-WA0018.jpg

Asha D. Abinallah akielezea jinsi JamiiForums inavyohusika kupigania uhuru wa kujieleza mitandaoni.

Sera na Sheria mbalilimbali zinazoongoza TEHAMA Tanzania
Sera ya mpya inayoongoza matumizi ya TEHAMA kwa Tanzania ilisainiwa mwaka 2016 ikichukua nafasi ya sera ya mwaka 2003 kutokana na mabadiliko yanayotokea katika Teknolojia hii, sera hii imeundwa kuendana na dira ya maendeleo ya taifa kufikia mwaka 2025 ambayo inatambua TEHAMA kama msingi wa mabadiliko ya kiuchumi na kijamii

Baadhi ya sheria muhimu zinazohusu TEHAMA ni kama zifuatazo
1.Sheria ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) iliyoundwa mwaka 2003 na kuunda TCRA kama chombo cha kudhibiti sekta ya mawasiliano

2.Sheria ya mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010
Sheria hii ilipitishwa ilikutambia mihamala inayofanywa kwa njia ya kielektroniki kama kutuma na kupokea pesa kwa njia ya elektoniki, kulipia huduma mbalimbali kwa njia za elektroniki, kutumia vifaa vya TEHAMA kama njia za kukusanya ushahidi utakaoweza kutumika mahakamani na mengineyo

3.Sheria ya Makosa ya Mtandao ya 2015
Hii ni sheria inayotoa muongozo wa makosa mbalimbali yanaoyohusiana na utumiaji wa TEHAMA

Hapa inaonekana kuwa Sera ya TEHAMA Tanzania imekuja (2016) baada ya sheria mbalimbali kuhusu TEHAMA kupitishwa jambo ambalo linaweza kuleta mkanganyiko kwa kuwa sheria inapaswa kutengenezwa kulingana na sera iliyopo

Uhusiano wa TEHAMA, Haki za binadamu na Demokrasia
Haki za binadamu ni haki ambazo binadamu yoyote anapaswa kuwa nazo kwa kuwa ni binadamu bila kujali jinsia, rangi yake, dini yake, jinsia au asili yake yoyote.
Moja wapo wa haki za msingi za binadamu ni haki ya kuishi, haki ya kutoa maoni, haki ya kuabudu dini au kuwa na imani aipendayo.
Demokarsia ni mfumo wa utawala ambapo wananchi wanakuwa na nguvu ya kuchagua ni anai awawakilishe na kuwaongoza katika serikali.

TEHAMA inawawezesha wananchi kujua haki zao na kuwapa uwanja wa kutoa maoni mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii.

20170711_101527.jpg

Dr. Wairagala Wakabi kutoka CIPESA Uganda akifafanua jambo katika siku ya pili ya Mafunzo yaliyofanyika Serena Hotel.

TEHAMA pia inawezesha wananchi kupata taarifa juu ya mtu anayetaka kuwaongoza na kutoa uwanja wa kufanya majadiliano juu ya ubora wa mtu huyo kama kiongozi
TEHAMA pia natumiaka kwenye upigaji kura ambapo mwaka 2015 Tanzania ilitumia njia ya BVR kuandikisha wapiga kura wake


Hali ya Uhuru wa Mtandao ilivyo Tanzania
Uhuru wa Mtandao inamaanisha hali ya uhuru wa mwananchi kutoa maoni yake kwenye mtandao wa kijamii bila kuvunja sheria pasipo woga wa kukamatwa.
Kwa Tanzania serikali inaonekana kushikilia uhuru wa mtandao kwa kupitisha sheria kama Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015, Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2015 na sheria mpya ya Habari iliyopitishwa mwaka 2017 na pia kumekuwa na matukio ya serikali kufuatilia mawasiliano binafsi ya watu, kulingana na utafiti uliofanywa na CIPESA mwaka 2016.

Kumekuwa na matukio pia ya polisi kutumika kuminya uhuru wa mtandaoni kwa kuwatumia barua kadhaa kampuni ya Jamii Media inayomiliki mtandao wa JamiiForums kuwataka kutoa taarifa za watumiaji waliotoa taarifa kwenye mtandao huo.
Utafiti huo unaonyesha pia kuwapo kwa hali ya woga iliyoletwa na sheria ya Makosa ya Mtandaoni.
Kumekuwa pia na usumbufu kwa makampuni ya simu kutoka kwa polisi na TCRA kuwataka kutoa taarifa za wateja wao sababu ya sheria ya makosa ya mtandao ilipitishwa bila kuelezea ni namna gani taarifa juu ya mtu fulani inaweza kuchukuliwa hivyo kuwaaachia polisi kufanya wanavyoona ambapo wakati mwingine wamekuwa wakitumiwa na watu binafsi.
Kwa sasa watanzania wengi wanaogopa kutoa maoni kwenye mitandao ya kijamii, ambao wapo huru wa kutoa maoni yoyote ni wale wanaoungana na serikali.

Hii inahusu sheria mbalimbali kwa ajili ya kuendana na mabadiliko kwenye mawasiliano ya kielektroniki
 
Dah nimefarijika kumuona Ashadii madam hakika tumekumiss sana jukwaani au majukumu yamekuwa mengi tunakuomba sana ukipata nafasi ujongee huku jukwaani.

Back to topic Bado nchi za kiafrika zipo nyuma sana kwenye matumizi ya internet elimu inahitajika. Sana. Congrats JF teams for good work.
 
I know my rights i respect the rule of law and i know the consequences aisee kwenye ukweli mtaniuwa u better kill me 1st ndo ucheze na haki yangu
 
Liserikali la ajabu lisilopenda kukosolewa ni matatizo. Viongozi viburi na mambumbumbu yasiyo na vyeti pia ni kikwazo kwa wanyonge. Hata viongozi wenye vyeti bado elimu zao ni za mashaka na ndo hao wanaoyalinda mataahira yasiyo na vyeti kwa kodi za wanyonge. Ni aibu kwa sasa kujiita mtanzania.
 
Safi sana...
Aisee hicho kipengele cha saba kinawafanya mfanye kazi kwenye mazingira magum mno....
Mungu awatangulie kwa kweli....
 
AshaDii maadamu umekuwa kimya sana jamani yaani mpaka nimekusahau vipi ile tour ya kwenda tena ocean road hospital kuwaona wangonjwa haipo tena tuambiane tuchangie twende tena kama wakati ule
Nakumbuka kama sijakosea, ilikuwa Mwaka 2014 mliobahatika kwenda kuwaangalia Wagonjwa.

Mijumuiko kama hii ni mizuri sana, na inakupa hamasa ya kuwafikiria wenzio ambao wako Mahospitalini Kimaradhi, Kimatibabu, kuliko vile vikao vya Starehe.

Safi sana
 
Back
Top Bottom