Uchaguzi 2020 Cecilia Mwanga, Mgombea wa Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia Makini, amechukua fomu za uteuzi NEC

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,802
11,961
Cecilia Mwanga, Mgombea wa Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia Makini amechukua fomu za uteuzi wa kugombea nafasi hiyo leo Agosti 8, 2020 katika ofisi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jijini Dodoma. Bi. Mwanga ameambatana na Mgombea Mwenza, Tabu Juma pamoja na viongozi wa chama.
20200808_151352.jpg
20200808_151349.jpg
 
Cecilia Mwanga, Mgombea wa Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia Makini amechukua fomu za uteuzi wa kugombea nafasi hiyo leo Agosti 8, 2020 katika ofisi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jijini Dodoma. Bi. Mwanga ameambatana na Mgombea Mwenza, Tabu Juma pamoja na Viongozi wa chama.

1596889669308.png
 
Anataka yatokeee kama ya Mama Anna Mghwira eegh
 
Hiki Chama kinaitwa Chama Cha Demokrasia Makini au hio makini ina maana kwamba ni Chama Makini, ila kina jina lake ?
 
Huyu anasema kwenye kampeni yake atatumia guta na punda

Ova
 
Wanawake wangekua na umoja 29/ 10 /2020 ingezaliwa Tanzania mpya. Na haya mazingaubwe na ujinga mwingi ungekoma.
 
Mgombea urais kwa tiketi ya Demokrasia Makini, Cecilia Augustino Mmanga aliyekwenda kuchukua fomu ya uteuzi wa kuwania urais NEC Makao Makuu wakiwa na Bajaji, Agost 8, amesema huo ndio utakuwa usafiri wao.

Amesema kwa kipindi chote cha kampeni kitakachoanza Agosti 26 wao watatumia Bajaji, pikipiki na baiskeli, guta na punda katika kufanya kampeni zao nchi nzima.

Akiongea na waandishi wa habari amesema watatumia usafiri huo kwa kuwa wakulima walio wengi ndio hutumia usafiri huo na wao chama chao ni Makini yaani makini ni maarifa, kilimo na nishati.

1596950378391.png
 
Back
Top Bottom