Leo Oktoba 9 ni miaka 40 tangu kuuawa kwa mwanamapinduzi Che Guevara nchini Bolivia. Nimepata kukisoma kitabu kiitwacho " The African Dream"- The diaries of the revolutionary war in the Congo. Ama hakika ni kitabu chenye maelezo yenye kusisimua, kufurahisha na kusikitisha juu ya mwanamapinduzi huyu na harakati zake za mapambano ya ukombozi wa kimataifa.
Che aliingia Dar April 1965, alikutana na Nyerere na kupata baraka zake. Aliingia Mashariki ya Congo akiwa na kikosi cha askari 100; Hawa ni Wa-Cuba weusi waliopata mafunzo ya kijeshi Havana bila kuelewa kuwa walikuwa wanakwenda Congo. Uwepo wa Che Guevara jijini Dar April 1965 haukufahamika na wengi.
Hata CIA hawakuelewa hilo. Hadi mwaka 1990 CIA waliamini kuwa Che Guevara aliingia Congo akitokea Congo Brazaville. Kwamba Che Guevara alikuwa Dar kwa juma moja na zaidi unadhihirisha ukweli wa simulizi kuwa Che Guevara alitembelea mgahawa wa Zahir ( Sasa New Zahir Restaurant) mtaa wa Msikiti. Che alikuwa na mazoea ya kunywa chai na kula chakula mahala hapo.
New Africa Hotel kulikuwa na mgahawa maarufu kule juu kabisa, lakini pale pangemfanya aonekane kirahisi hata na mawakala wa CIA. Che Guevara anamweleze Laurent Kabila ( Baba yake Joseph Kabila) kama mtu ambaye hakuwa makini katika kuendesha harakati za mapambano.
Che anaandika; kuwa Kabila alipenda sana pombe, hakuonekana kwenye uwanja wa mapambano, mara nyingi alituma ujumbe wa mdomo au maandishi kutoa maelekezo. Che alikwenda na kikosi chake Mashariki ya Kongo bila ya mwenyeji wake, Laurent Kabila. Kiumri, Laurent Kabila alikuwa na miaka 26 tu wakati huo. Kuhusu umri wa Kabila Che Gueavara anandika hivi; " Kabila is young, and it is possible that he will change. But I have very great doubts about his ability to overcome his defects in the environment in which he operates".
Nisimalize utamu wa kitabu; tafuta kitabu hiki ukisome. Kinatoa picha tofauti na kutusaidia kuelewa baadhi ya sababu zinazopelekea vita vinavyochukua muda mrefu katika ukanda wa Maziwa Makuu.
Kwa habari zaidi katika picha tembelea; http://mjengwa.blogspot.com