Chura Anayebadilika badilika Rangi Aabudiwa Kama Mungu India | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chura Anayebadilika badilika Rangi Aabudiwa Kama Mungu India

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by MziziMkavu, Jun 10, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Chura Anayebadilika badilika Rangi Aabudiwa Kama Mungu India
  [​IMG]
  Chura Anayebadilika badilika Rangi Aabudiwa Kama Mungu India Tuesday, June 09, 2009 9:17 PM
  Chura anayebadilika rangi tofauti tofauti muda wote ambaye aligunduliwa hivi karibuni nchini India na mwanaume mmoja wakati akimwagilia maji bustani yake amekuwa kivutio kikubwa kiasi cha kwamba mamia ya wahindi wanamiminika kumuona na wengine wanamuabudu kama mungu. Mamia ya wahindi wanamiminika kwenye mji wa Kerala kumuona na kufanya maombi yao kwa chura ambaye muda wote anabadilika badilka rangi na kuwa na rangi tofauti.

  Reji Kumar, mkazi wa mji wa Kerala alimgundua chura huyo kwenye bustani yake wakati akimwagilia maji na baadae alimuhifadhi kwenye chupa.

  Reji anahofia chura huyo anaweza akafariki baada ya kugoma kula tangia mamia ya watu walipoanza kumiminika nyumbani kwake kumuona.

  "Tatizo ni kwamba huyu chura ameacha kabisa kula, najaribu kila njia kumlisha lakini amegoma kabisa".

  Chura huyo alikuwa rangi nyeupe wakati Reji alipomgundua baada ya muda mfupi aligeuka kuwa njano na alipomfikisha nyumbani kwake chura huyo alibadilika na kuwa wa kijivu.

  "Usiku ulipofika alibadilika na kuwa rangi ya njano iliyokolea na baadae akabadilika tena na kuwa na rangi iliyoonyesha viungo vyake vya ndani " alisema Reji.

  "Ni kama muujiza vile chura kuwa na uwezo wa kubadilika rangi mbali mbali watu wamekuwa wakimiminika kwa wingi kumuona na kupiga dua zao".

  Profesa Oommen V. Oommen wa chuo kikuu cha Kerala University alisema kuwa si kawaida kwa wanyama kubadilika rangi.

  "Chura hubadilika rangi kuwatishia maadui zao wanapokuwa hatarini, lakini chura wa Reji kwa jinsi anavyobadilika rangi tofauti tofauti kila mara si jambo la kawaida" alisema Profesa Oommen.

  Wataalamu wa wanyama nchini India wana mpango wa kumchukua chura huyo kumfanyia uchunguzi kujua inakuwaje anabadilka badilika rangi namna hiyo.

  Chura ni miongoni mwa wanyama wanaoabudiwa nchini India, miungu mingine ya wahindi ni njiwa na ng'ombe.
   
 2. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mh! ni ajabu.
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Jun 10, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  Wakimalizana hiyo ibada wanaanza safari za kutafuta utajiri TZ.
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Jun 10, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,381
  Likes Received: 22,253
  Trophy Points: 280
  wahindi kwa kuabudu abudu kila wanachokiona..
  Hakika ni mabingwa,.
  David beckham alitembelea india naye alipewa hadhi ya umungu...
  Cha ajabu wakija hapa kwetu wao ndio wanageuka miungu na watawala wetu wanawaabudia
   
Loading...