Chupuchupu waiage dunia kwa kuning’inia garini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chupuchupu waiage dunia kwa kuning’inia garini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Aug 23, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,605
  Trophy Points: 280
  WATU watatu wamenusurika kifo baada ya kuanguka kutoka garini na kuangukia barabarani na kuponyeka kukanyagwa na magari.

  Tukio hilo lilitokea jana majira ya saa 1 jioni, huko maeneo ya barabara ya Mandela ambapo watu hao walikuwa wakining’inia mlangoni mwa basi lililokuwa likifanya safari zake kutoka Ubungo kuelekea Mbagala.

  Kutokana na usafiri kuwa wa shida hasa nyakati za jioni watu hao walilazimika kuingia kweny e basi hilo huku wakiona limefurika watu na kujitosa na kupelekea kukosa nafasi ya kuingia ndani ya basi hilo na kuishia mlangoni waking’inia wahahi majumbani mwao.

  Hivyo kwa kuwa barabara hiyo ipo kwenye matengenezo ambayo hayajulikani yatakamilika lini dereva wa gari hilo alikuwa akiendesha gari hilo kwa kutozingatia kanuni za usalama barabarani akitaka kuyapita magari yaliyombeleyake.

  Basi hilo kufika maeneo ya Tabata lilikuwa linajaribu kulipita lori lililokuwa mbele yake na kushindwa na kupelekea kusimamisha basi hilo kwa ghafla na watu waliokuwa wakining’inia kuanguka chini na kunusurika na kukanyagwa na magari.

  Watu hao walianguka chini na kunusurika na kukanyagwa na magari yaliyokuwa yakija nyuma yao.

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=2891038&&Cat=1
   
Loading...