Chupa za vileo na uharibifu wa Mazingira

masare

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
1,377
1,517
Wadau,
Hili ni janga jipya ambalo Serikali inabidi itunge sera au sheria ya kukabiliana nalo kama vile ilivyotunga sheria ya kuondoa vifungashio vya vilevi maarufu kama viroba.

Ieleweke kuwa makampuni ya kutengeneza soda hukusanya chupa zilizotumika. Pia baadhi ya makampuni ya vileo kama "Banana" pia hukusanya chupa zilizotumika. Chupa za soda huwa zimeandikwa "This bottle is refundable" ikimaanisha kuwa endapo utanunua soda na kuondoka na chupa basi kuna gharama utapaswa uongezee.

Hii imefanya chupa za soda zilizotumika kuwa ni bidhaa kama zilivyo nyingine.Ukienda kwenye duka lolote la vinywaji la rejareja au jumla utatakiwa upeleke chupa tupu kulingana na idadi ya soda au kreti unazotaka ili ubadilishiwe na soda za chupa halisi.

Lakini kwa upande wa vileo hali ni tofauti, kumekua na utupaji wa hovyo wa chupa zilizotumika simply kwa sababu haziko "refundable". Mnunuzi wake akishanunua anakua amenunua jumla yaani hicho kileo+chupa yenyewe.

Hali imeanza kuwa mbaya hasa mitaani ambapo mabaki ya chupa za vileo kama K-VANT, Konyagi, Wines n.k yanatupwa tu hovyo hovyo kwenye mitaro pamoja na sehemu nyingine.

Ni wakati sahihi sasa kwa wadau wa mazingira kutafuta njia mbadala ya kurecycle hizo chupa za vileo zilizotumika kabla hatujanotice madhara makubwa zaidi kwenye mazingira yetu.
 
Pia pampas zilizotumika zimekuwa zinatupwa ovyo na kuleta uchafuzi wa mazingira na kero kubwa kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom