Chuo Kikuu UDSM mna nini na Wanafunzi wa Post-Graduate?

Kilemakyaaro

JF-Expert Member
Jul 19, 2016
4,600
2,000
Kwa miaka ya karibu kumekua na Idadi kubwa ya Wanafunzi wa Post Graduate katika Chuo kikuu Cha Dar es Salaam wanaoshindwa kumaliza masomo yao. Wengi wao ni kutokana na baadhi ya Wahadhiri kutofuata ratiba za wanafunzi haswa kwenye eneo la Thesis.

Walimu wanajitia ubusy usio na sababu, mtu ana submit kazi yake lakini msimamizi hajali muda, yuko anahangaika na mishe zake na mwisho mwanafunzi anashindwa kumaliza kwa wakati.

Yaani wanasahau kabisa kuwa wengine wameomba ruksa makazini na muda hio ukiisha wanarejea bila kuwa wamemaliza. Kiukweli hili limekua tatizo kubwa kias kwamba kila ukitaka kujiunga na chuo unakutana na ushauri wa wengi wanaoteseka na hizi mambo kiasi unakata tamaa.

Ninadhani kunahitajika kufanyika jambo
 
Mwanamaji

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
1,902
2,000
Mwaka jana mwishoni (Mwezi Novemba) nilihudhuria ''orientation'' ya shahada za juu (postgraduate studies), moja ya mambo yaliyozungumzwa ni hili uliloliwasilisha hapa.

Ni wazi kwamba uongozi wa chuo uliliona hili kutokana na malalamiko ya wadau wengi.

Katika kulitatua na kuondoa hii kero na malalamiko, walisema kwamba wanakuja na mfumo maalumu wa online (waliuita ARIS 3) ambao utaonyesha wazi ni lini mwanafunzi amewasilisha kazi yake kwa msimamizi wake, ni lini msimamizi huyu amemjibu na amemjibu nini, n.k.

Mfumo huo (kwa maelezo yao) utaleta uwazi na kuondoa mizengwe ya wasimamizi wacheleweshaji. Endapo kutakua na madai ya mwanafunzi kucheleweshwa, basi mfumo huu utasema na hivyo msimamizi yule atachukuliwa hatua stahiki.

Lakini pia uwazi huu utawalazimisha wasimizi ''wenye mambo mengi'' kuhakikisha wanatimiza majukumu yao kwa wanafunzi wanaowasimamia kwa wakati.

NB: Sijajua kama mfumo huu ulishaanza kazi tayari au la. Kwasababu fulanifulani sikuendelea na masomo katika chuo hicho hivyo sina ushahidi wa kutosha juu ya kukamilika kwa mpango huo.
 
Kilemakyaaro

JF-Expert Member
Jul 19, 2016
4,600
2,000
Aise nnawaza kuanza Masters hapo lkn nnajiwazia tu ntakavyonyongewa chini maana sintavumilia huu uhuni
Mwaka jana mwishoni (Mwezi Novemba) nilihudhuria ''orientation'' ya shahada za juu (postgraduate studies), moja ya mambo yaliyozungumzwa ni hili uliloliwasilisha hapa.

Ni wazi kwamba uongozi wa chuo uliliona hili kutokana na malalamiko ya wadau wengi.

Katika kulitatua na kuondoa hii kero na malalamiko, walisema kwamba wanakuja na mfumo maalumu wa online (waliuita ARIS 3) ambao utaonyesha wazi ni lini mwanafunzi amewasilisha kazi yake kwa msimamizi wake, ni lini msimamizi huyu amemjibu na amemjibu nini, n.k.

Mfumo huo (kwa maelezo yao) utaleta uwazi na kuondoa mizengwe ya wasimamizi wacheleweshaji. Endapo kutakua na madai ya mwanafunzi kucheleweshwa, basi mfumo huu utasema na hivyo msimamizi yule atachukuliwa hatua stahiki.

Lakini pia uwazi huu utawalazimisha wasimizi ''wenye mambo mengi'' kuhakikisha wanatimiza majukumu yao kwa wanafunzi wanaowasimamia kwa wakati.

NB: Sijajua kama mfumo huu ulishaanza kazi tayari au la.
Kwa sababu fulanifulani sikuendelea na masomo katika chuo hicho hivyo sina ushahidi wa kutosha juu ya kukamilika kwa mpango huo.
 
6321

JF-Expert Member
Oct 16, 2016
449
1,000
Unakuta mwal mmoja anafundisha ardhi,muhimbil, udom kila chuo anafundisha, hapo bado ni external reviwer wa thesis, bado kuna projects nying za kitaifa na kimataifa ambazo akipiga mihayo tu anaingiza dola. Tusiwalaumu sana
 
Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
3,967
2,000
Waliofanyiwa wawashitaki wasimamizi/washauri wa theses zao pamoja na chuo kikuu. Watalipwa gharama zao na upotevu wa muda hata matarajio. Naamini hili likifanyika watatia adabu. Angalia mwanafunzi aliyekutana na haya mnayosema nchini Kenya alivyolipwa Kshs. 500,000 hata kama ni kidogo. UoN To Pay Former Student Sh500,000 For Delaying Graduation By 5 Years. Ni uzembe wa kipumbavu ambao haupaswi kufanywa na watu wanaojiita wasomi. Na huu ni ushahidi kuwa wahusika hawajaelimika vilivyo.
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
9,858
2,000
Ndiyo, inahitajika kufanyika jambo.

Kwanza hiyo ni dalili ya kuwepo ubovu kwenye chuo kizima. Maana yake hao maprofesa hawafanyi kazi zao inavyopasa wafanye. Ubora wa elimu hapo ni wa mashaka sana.

Jambo la kwanza muhimu ni kuwa na ushahidi usiopingika.

Wewe na wenzio mnaocheleweshwa, kusanyeni ushahidi kisayansi. Tafuta wote waliocheleweshwa katika muda maalum; kwa mfano miaka kumi iliyopita hadi wakati huu ni wangapi wamecheleweshwa na wangapi imelazimu kuacha kabisa kutokana na uchelevu huo.

Hapo hapo, kutakuwa na takwimu za nyuma, chukueni kwa mfano miaka ya 1980 hadi 2000, linganisha kuona kama kuna tofauti na pia tafuta sababu za kila aliecheleweshwa au aliyebidi aache moja kwa moja.

Ikiwezekana, tafuteni mifano ya vyuo vingine vyenye hadhi sawa na hicho chuo chenu. Chukueni ushahidi wa huko

Mkishakusanya ushahidi wote huu, mnaweza kuwaendea utawala hapo chuoni; kama hawatoi ushirikiano chapisha kwenye vyombo vya habari, n.k.

Huo utakuwa ni mwanzo wa kufanya jambo.
Kumbuka, hawa wanawapotezea muda, na hapo hapo mnapoteza hela zenu. Hawa hawawafanyii fadhila, ni wajibu wao kutimiza ahadi yao kwenu. Kwa hiyo wanawanyima haki yenu.

Mahakama zipo kulinda haki za watu.

WaTanzania tunapenda sana kulia lia kwa kila jambo hata mahali ambapo haki tunanyimwa.

Ni lazima sasa tuanze kujifunza kusimamia, kulinda na kutafuta haki zetu zinapoporwa.

Kwa nini tusiwe tumejifunza kutoka kwa tuliyoyashuhudia wakati wa Magufuli, na tukatae kuendelea kuonewa?
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
9,858
2,000
Unakuta mwal mmoja anafundisha ardhi,muhimbil, udom kila chuo anafundisha, hapo bado ni external reviwer wa thesis, bado kuna projects nying za kitaifa na kimataifa ambazo akipiga mihayo tu anaingiza dola. Tusiwalaumu sana
Mwalimu asiyejua 'time management', huyo ni mwalimu wa dunia gani mkuu!

Kama anakubali kubeba majukumu yote hayo, bila kujali atayamudu vipi, bado unamsifia kitu gani?
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
57,376
2,000
Kuna Profesa Palamagamba Kabudi alipopata uteuzi alishukuru kwa kuondolewa jalalani, ikaonekana kama utani hivi.

Kumbe kuna machafuchafu hivi kweli?
 
Sonofsoil

JF-Expert Member
Feb 13, 2014
1,962
2,000
Kwa miaka ya karibu kumekua na Idadi kubwa ya Wanafunzi wa Post Graduate ktk Chuo kikuu Cha Dar es Salaam wanaoshindwa kumaliza masomo yao. Wengi wao ni kutokana na baadhi ya Wahadhiri kutofuata ratiba za wanafunzi haswa kwenye eneo la Thesis.
Walimu wanajitia u busy usio na sababu, mtu ana submit kazi yake lkn msimamizi hajali muda, yuko anahangaika na mishe zake na mwisho mwanafunzi anashindwa kumaliza kwa wakati.
Yaani wanasshau kabisa kua wengine wameomba ruksa makazini na muda hio ukiisha wanarejea bila kuwa wamemaliza. Kiukweli hili limekua tatizo kubwa kias kwamba kila ukitaka kujiunga na chuo unakutana na ushauri wa wengi wanaoteseka na hizi mambo kias unakata tamaa. Nnadhani kunahitajika kufanyika jambo
Some lecturers there are clinically dead academically.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom