Chuo Kikuu St. John chafungwa kwa sababu ya vurugu

OgwaluMapesa

JF-Expert Member
May 24, 2008
10,943
428
Vurugu za wanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. John mkoani Dodoma za kuushikiza uongozi uwape fedha za kujikimu zimeibuka tena jana na kusababisha chuo hicho kufungwa hadi Januari 3, mwakani. Hali hiyo imeibuka jana asubuhi ambapo wanafunzi wa shahada ya kwanza wa mwaka wa kwanza hadi wane, walipoendelea kuushinikiza uongozi wa chuo hicho kuwapa fedha za kujikimu. Mgomo huo ulianza Jumatatu wiki hii, ambapo wanafunzi hadi walikusanyika na kuutaka uongozi kuwapa fedha za kujikimu kwa madai wao hawana fedha.

Aidha, mgomo huo ulishindwa kuendelea baada ya Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kufika chuoni hapo na wanafunzi hao kutimua mbio. Hali hiyo iliendelea kuwa tete baada ya wanafunzi hao jana asubuhi kurudi tena na kuanza mgomo upya huku wakiendeleakuushinikiza uongozi huo kutoa fedha hizo. Wanafunzi hao walikuwa wametanda kwenye eneo la Utawala la chuo hicho huku wakipiga kelele na wengine wakirusha mawe. Kutokana na vurugu hizo, chuo kiliamua kuomba
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom