Chuo Kikuu Huria Tanzania(OUT) chashika nafasi ya 13 duniani, ya pili Afrika

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
1,000
1075515CHUO Kikuu Huria nchini (OUT) kimeshika nafasi ya 13 kati ya vyuo vikuu huria 102 kwa ubora duniani na kwa Afrika kimeshika nafasi ya pili. Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Elifas Bisanda alisema hayo alipokuwa akizungumza na HabariLeo chuoni hapo juzi.

Profesa Bisanda alisema Februari, mwaka huu ilitolewa taarifa ya ubora wa vyuo vikuu huria duniani ambapo vipo vyuo vikuu huria 102 kati ya hivyo, OUT imeshika nafasi hiyo ya 13 kwa ubora. Aliongeza kuwa katika Afrika vyuo vikuu huria vipo tisa, chuo hicho nchini kimeshika nafasi ya pili kwa ubora na Chuo Kikuu Huria Afrika Kusini ndicho kilichoshika nafasi ya kwanza. Kwa mujibu wa Profesa Bisanda, katika vyuo vyote 49 vilivyopo nchini, OUT ni namba sita kwa ubora.

Kwa upande mwingine alielezea changamoto iliyopo katika chuo hicho kuwa ni Jumuiya ya Watanzania kutoelewa vizuri mfumo wa elimu masafa, wakikiria kuwa ni elimu ya chini na hafu. Alisema katika chuo hicho wanafunzi wanakuwa na uelewa mkubwa kwa kuwa hawafundishwi darasani lakini wanapewa maeneo yote ya kusoma ili wayapitie waweze kufanya vizuri katika mitihani yao.

“Mtihani unatungwa kulingana na mtaala. Na ubora wa elimu inayotolewa chuoni hapa hauwezi kulinganishwa na vyuo vingine kwa kuwa mwanafunzi anasoma katika wigo mpana,” alisema. Alisema hata wanafunzi wanaomaliza Kidato cha Sita hawaelewi ubora wa elimu unaotolewa na chuo hicho, hivyo wamekuwa wakifanya kampeni shuleni kwa ajili ya kuwaelimisha wanafunzi hao kujiunga na OUT.

Mwaka jana chuo hicho kilikuwa na wanafunzi 8,000 lakini sasa wamekia wanafunzi 12,994 na kabla ya kuondolewa kozi ya foundation mara ya kwanza na hatimaye kurudishwa chuo hicho kilikuwa na wanafunzi 16,000.
 
Manofu

JF-Expert Member
Nov 3, 2018
1,317
2,000
Lakini labda na wewe fanya utafiti wako ujue imekuwaje OUT imetajwa kwenye huo utafiti. Jee ni Lazima kwenye zama hizi za TEHAMA kusubiri kuambiwa na Professa Elifas Bisanda hitimisho la utafiti huo umefikiwaje.
Kina polepole kwa mjibu wa utafiti wao wanasema CCM inapendwa sana na wananchi. Do u conquer with the conclusion?
 
Edzone

JF-Expert Member
Jan 26, 2017
1,105
2,000
View attachment 1075515

CHUO Kikuu Huria nchini (OUT) kimeshika nafasi ya 13 kati ya vyuo vikuu huria 102 kwa ubora duniani na kwa Afrika kimeshika nafasi ya pili. Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Elifas Bisanda alisema hayo alipokuwa akizungumza na HabariLeo chuoni hapo juzi.

Profesa Bisanda alisema Februari, mwaka huu ilitolewa taarifa ya ubora wa vyuo vikuu huria duniani ambapo vipo vyuo vikuu huria 102 kati ya hivyo, OUT imeshika nafasi hiyo ya 13 kwa ubora. Aliongeza kuwa katika Afrika vyuo vikuu huria vipo tisa, chuo hicho nchini kimeshika nafasi ya pili kwa ubora na Chuo Kikuu Huria Afrika Kusini ndicho kilichoshika nafasi ya kwanza. Kwa mujibu wa Profesa Bisanda, katika vyuo vyote 49 vilivyopo nchini, OUT ni namba sita kwa ubora.

Kwa upande mwingine alielezea changamoto iliyopo katika chuo hicho kuwa ni Jumuiya ya Watanzania kutoelewa vizuri mfumo wa elimu masafa, wakikiria kuwa ni elimu ya chini na hafu. Alisema katika chuo hicho wanafunzi wanakuwa na uelewa mkubwa kwa kuwa hawafundishwi darasani lakini wanapewa maeneo yote ya kusoma ili wayapitie waweze kufanya vizuri katika mitihani yao.

“Mtihani unatungwa kulingana na mtaala. Na ubora wa elimu inayotolewa chuoni hapa hauwezi kulinganishwa na vyuo vingine kwa kuwa mwanafunzi anasoma katika wigo mpana,” alisema. Alisema hata wanafunzi wanaomaliza Kidato cha Sita hawaelewi ubora wa elimu unaotolewa na chuo hicho, hivyo wamekuwa wakifanya kampeni shuleni kwa ajili ya kuwaelimisha wanafunzi hao kujiunga na OUT.

Mwaka jana chuo hicho kilikuwa na wanafunzi 8,000 lakini sasa wamekia wanafunzi 12,994 na kabla ya kuondolewa kozi ya foundation mara ya kwanza na hatimaye kurudishwa chuo hicho kilikuwa na wanafunzi 16,000.
Naamini mm ni mwanafunzi pale.
 
Masiya

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
7,064
2,000
Kwa upande mwingine alielezea changamoto iliyopo katika chuo hicho kuwa ni Jumuiya ya Watanzania kutoelewa vizuri mfumo wa elimu masafa, wakikiria kuwa ni elimu ya chini na hafu. Alisema katika chuo hicho wanafunzi wanakuwa na uelewa mkubwa kwa kuwa hawafundishwi darasani lakini wanapewa maeneo yote ya kusoma ili wayapitie waweze kufanya vizuri katika mitihani yao.
Ni miongoni mwa vyuo vikuu bora kabisa lakini hili neno HURIA linanifikirisha sana
Nami niwapongeze OUT kwa kazi nzuri wanayoifanya. Pili kwa Prof. Bisanda na wasaidizi wake wanahitaji kuwekeza ili watanzania wengi zaidi waelewe aina ya elimu inayotolewa na OUT. Yaliyotokea hapa karibuni yalionyesha kuwa hata huko serikalini kuna wakubwa ambao bado hii kitu haijawakaa sawa (sakata la Foundation program lahusika na sasa imebanwa sana).
Neno huria limetolewa kwenye neno "open" ikimaanisha elimu yake iko wazi kwa yule anaefikiri anastahili na vigezo vyake vya kudahiliwa vinatakiwa viwe CHINI kabisa. Hii haina maana kila mtu anaiweza bali wale ambao wako tayari kufanya kazi watapata elimu yenye viwango sawa na wale wanaopitia mifumo mingine. Hawaangalii sana unaingiaje bali quality control yao ni kubwa hivyo kwamba ukipata shahada yao hauna wasiwasi. Hivi ndiyo inatakiwa elimu HURIA kuwa na ni jukumu la chuo kuhakikisha elimu yake ina thamani inayotarajiwa. Hapa pia ni wajibu wa serikali kuhakikisha chuo kina infrastructure (walimu na vitendea kazi stahiki).

Chuo gani hata vilaza wanapata degree
Elewa kwanza maana ya elimu HURIA, halafu tujulishe ni vilaza wepi unaowafahamu walipata degree ya hapo OUT na ilikuwa mwaka gani?
 
sagaciR

JF-Expert Member
Jun 17, 2017
645
1,000
Hongera sana The Open University of Tanzania (O.U.T)

Hichi Chuo kwa hakika nakikubali sana, Wapuuzi wachache wanaokidharau wamekaririshwa tu kudharau na kusifu ila hawaelewi lolote!
Wahenga walisema "MWAMBA NGOMA HUVUTIA KWAKE" Hongereni kwa kuwa wazalendo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom