Chuo Kikuu Huria chabadili mfumo wa kufanya mitihani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chuo Kikuu Huria chabadili mfumo wa kufanya mitihani

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Ngongo, Aug 31, 2009.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280
  CHUO kikuu Huria Tanzania kimebadili mfumo wa utoaji majaribio kutoka mara tano kwa mwaka hadi mara mbili, ili kuongeza ufanisi na ubora wa kukuza uwezo wa wanafunzi katika kufaulu mitihani.

  Akizungumza katika mkutano wa Wahadhiri na wanafunzi wa chuo hicho, Makamu Mkuu wa chuo Tolly Mbwette, alisema mfumo huo mpya utawawezesha wanafunzi kupata muda na nafasi ya kujiandaa na mitihani ya majaribio.

  "Hatua ambayo chuo imechukua ni nzuri, kwa sababu njia hii itamsaidia mwanafunzi kukuza uelewa wake badala ya kutegemea kufanyiwa majaribio na mwenzake", alisema.

  Mbwette alifafanua kwamba, wanafunzi waliowengi wamekuwa wakifanyiwa mazoezi na wanafunzi wengine kwasababu ya kuwa na kazi nyingi ambazo zinawafanya washindwe kumudu kufanya majaribio yanayotolewa na chuo.

  " Hatua hii itasaidia kwani walimu waliowengi hawasahihishi mitihani kwa muda mwafaka, baadhi yao wanasaisha mitihani mingi bila kujali ubora kwa ajili ya kulipwa fedha nyingi" alisema Mbwette.

  Hata hivyo, alifafanua kwamba bajeti ya fedha iliyotolewa na serikali mwaka huu ni ndogo haiwezi kukidhi mahitaji yote ya chuo hivyo bado wanaendelea kufanya jitihada za kuweza kupata fedha za kutosha ili kuboresha elimu ya juu katika chuo hicho.

  "Tunaishukuru serikali kwa kukubali kutuongezea wanataaluma ambao watasaidia kwa kiasi kikubwa kufundisha na kufunya chuo kuendelea kuongeza idadi ya wanafunzi, " aliongeza.

  Kwa upande wa wanafunzi, walisema wamefurahishwa na hatua iliyochukuliwa na viongozi wa chuo kwa kubadili mfumo ambao ulikuwa ukiwabana, hivyo mfumo huo mpya utatoa nafasi kwa kila mwanafunzi kufanya mtihani kwa nafasi.

  Mwanafunzi wa mwaka wa tatu Happy Mbile, alisema mfumo wa awali haukuwa mzuri kwasababu wanafunzi wengi hawakuweza kuonyesha uwezo wao, kwakukosa mda wa kufanya majaribio wenyewe, kulingana na kazi nyingi hasa kwa wale wanaofanya kazi maofisini.
   
  Last edited: Aug 31, 2009
 2. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Wanauwezo wa kupokea na kuhudumia wanafunzi wangapi kwa ufanisi mzuri wakati wanafanya haya?Je inasaidia vp kuondoa uwezekano wa mtahiniwa kufanyiwa mtihani na mwenzake?
   
 3. N

  Nanu JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2009
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  It is always good to have a look back and make continual improvement. I applaude OUT for that!!!! Keep up guys. Nasikia siku hizi kuna masters ya mwaka mmoja Mzumbe-Dar Campus (coursework & dissertation within one year, halafu ni evening classes).
   
 4. K

  Kagoma Member

  #4
  Sep 2, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  CHUO kikuu Huria Tanzania kimebadili mfumo wa utoaji majaribio kutoka mara tano kwa mwaka hadi mara mbili, ili kuongeza ufanisi na ubora wa kukuza uwezo wa wanafunzi katika kufaulu mitihani.


  Hata hivyo, alifafanua kwamba bajeti ya fedha iliyotolewa na serikali mwaka huu ni ndogo haiwezi kukidhi mahitaji yote ya chuo hivyo bado wanaendelea kufanya jitihada za kuweza kupata fedha za kutosha ili kuboresha elimu ya juu katika chuo hicho.


  Kwa mtazamo wangu Chuo kimepunguza majaribio from 5 to 2 times because of Budget constraints and NOT to improve! Kimefulishwa na serikali ikabidi wa ji adjust!


   
 5. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kwa mtazamo wangu naona uongozi wa chuo umefanya jambo zuri sana
  Hii itasadia kumpa mwanaffunzi muda mzuri wa kujisomea na kufaulu vizuri
  Lakini pia itatoa nafasi ya Lecturers kusahihisha kwa umakini na nafasi mitihani hiyo na sio kulipua kama wanavyofanya sasa hivi
   
Loading...