Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) mnatia shaka kwenye hili, zile tafiti bora kabisa zimeenda wapi?

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
18,174
27,217
Nimeshangaa sana kuona chuo kikubwa na kikongwe afrika ya mashariki kinaanza kudidimia.

Ukweli usipingika ni kuwa chuo kikuu chochote bora ni lazima kiwe kimepika na kuwa na tafiti bora kabisa. Chuo kisichofanya tafiti bora ni sawa na sekondari tu.

Mwaka huu wa 2021 Kuna mabadiliko makubwa sana yanafanywa na wenzetu huko kwenye suala.zima la teknolojia. Vyuo vikuu na wasomi wake wanakesha kuja na tafiti bora ili kukuza teknolojia.

Nimeshangazwa na tuzo aliyopewa chemical ya tafiti bora kwa wanafunzi wa masters.

Inafikirisha na kuhuzunisha sana, kweli nyimbo wanazoimba wavuvi wakiwa wanavua ndio tafiti hiyo?

Namnukuu chemical "nilikuwa nikienda kisimani mkoani Lindi, wanawake wanalalamika kuwa wanaimbwa nyimbo mbaya na waume zao wakiwa kwenye shughi zao za uvuvi, hapo ndio nikaamua kufanya tafiti ya nyimbo wanazoimba"

Tafiti bora ya chuo kikuu kikongwe kabisa inahusu nyimbo za wavuvi wakiwa wanaimba kwenye shughuli zao za uvuvi?......astaghfirullah, astaghfirullah, astaghfirullah.

Na hapa ndio kuna siku tunataka Tanzania tuwe na viwanda vya kutengeneza magari na ndege?
Nilitegemea tafiti bora iwe kwenye waliotafiti kuhusu kukua kwa teknolojia na sio eti nyimbo wanazoimba wavuvi.

Tafiti bora ziwe kwenye masuala ya sayansi na teknolojia, ndio dunia ilipo huku. Tunahitaji kuwa na akina elon musk wetu.

Tunachangamoto kibao kwenye masuala ya sayansi na teknolojia ambapo wasomi wetu wanapaswa kuelekeza nguvu zaidi huku.

Sijui Kama tutafika ikiwa chuo kikuu kikongwe na kinachotegemewa kinatoa ushindi wa tafiti bora inayohusu nyimbo za wavuvi.

20210605_113328.jpg
 
Wasomi wetu wa kujisifu na GPA. UDSM hakuna utafiti pale wanashindwa kufanya utafiti wa kumsaidia mkulima wa chini kabisa.
 
Kwa hiyo kuna wanafunzi walinyimwa tuzo na walifanya tafiti bora kuliko hiyo ya kemiko?
Au hii ya nyimbo za wavuvi kuwaimba wanawake ndio ilikuwa tamu kupita zote mkuu?
 
  • Thanks
Reactions: Mj1
Kwa hiyo kuna wanafunzi walinyimwa tuzo na walifanya tafiti bora kuliko hiyo ya kemiko?
Au hii ya nyimbo za wavuvi kuwaimba wanawake ndio ilikuwa tamu kupita zote mkuu?
Yani tafiti bora iwe kuhusu nyimbo wanazoimba wavuvi? Hiki chuo kimepotea kabisa
 
Juzi kati nilikuwa semina moja hvi kigamboni...mmoja wa mhadhiri aliekuja kutoa mhadhara aliwahikuuwa kiongozi mkubwa sana tu kwenye moja ya taasisi nyeti Tanzania..alisema

Kuna kijana ana msapoti yupo kitaa ni mtaalam sana wa hesabu...ameunda fumola zake nyingi tu za hesabu...sasa huyo muhadhiri akaamua kumshika mkono..wakaenda nae UD kuomba kuonana na department ya hesabu sijui..watu wa ile department wakaangalia hesabu za dogo then wakamwambia watamwita..imepita zaidi ya miez 6 hawajawah hata kumissed call

Huyo mzee anafahamina na Dr mmoja anaefundisha hesabu Denmark..sasa huyo Dr alipokuwa likizo wakampelekea kile kitabu..yule Dr akakiangalia then akamwita dogo akawa anamuuliza maswali ya papo kwa papo kuhusu alichokiandika...dogo alijibu maswal yote kuhusu alichoulizwa bila kubabaika wala kudai atafute sehemu alipoandika ajikumbushe...yule Dr akamfanyia mpango sasa hvi dogo yupo denmark huko...anachukua MA Ya hesabu

Bongo watu wamekalia vitengo tu..hawatambui vipaji..wao wanataka usagike kama walivyosagika wao...
 
Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Safi Sana , huku wanapeana tuzo kwa nyimbo za wavuvi
 
Interesting...nadhani siyo UD pekee bali jamii kama jamii kuna sehemu dishi liliyumbishwa na sasa ndiyo matokeo yanaanza kuonekana wakati tukihitaji majawabu ya matatizo sugu bila kukumbuka tulikoyumbishwa dishi.
 
Inasikitisha sana, hapa kuna mambo mawili
1. Kuna mtu anataka kufurahishwa kwenye hii tuzo kwan watz wengi huwa wanaangalia ugali wao.
2. Tumekosa kabisa tafiti za maana, hiyo ikaonekana ni bora. Kama ndio hvyo basi taifa kama taifa tuna safari ndefu sana.
Maoni yangu namba moja itakuwa sahihi maana siamini kama chuo kikubwa kama UD kukosa vitu vya kutafiti
 
Ni vigumu sana kuijudge hiyo tuzo kwa maelezo yako maana ni mafupi sana na ya upande mmoja kuweza kutoa hitimisho..
ila pamoja na yote kama huyo mtu anastahili kupata tuzo kutokana na tafiti yake bila kujali ametafiti nini, inawezekana labda amepewa kutokana na kazi nzuri aliyoifanya kuhusiana na sanaa ya uimbaji, sio lazima kila mtu afanye tafiti za technolojia, eng. uchumi nk... yeye ameamua kubase kwenye sanaa.

Tusiwahukumu UDSM kwa kutoa hiyo tuzo kwenye huo utafiti, labda tuwalaumu kwa nini hawafanyi PIA na tafiti nyingine kwenye mambo ya tech, uchumi, biashara.. nk.
 
Back
Top Bottom