Chuo kikuu cha Nairobi chagundua Samaki wanaotoka China wana sumu za Mercury, ZINK, COPPER,LEAD,IRON. Ni hatari kwa afya ya ubongo na mwili. Tz kimya

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
A study done by the University of Nairobi in 2019 found that fish imported from China had traces of Mercury, Lead, Arsenic and Copper.

KEBS, then, denied that the fish posed any danger to human health. #ToxicFlow

Screenshot_20200217-203021.png

Kwanini tuagize samaki China wakati samaki wapo wa kututosha kwenye maji yetu!!?

Kama kuna uhitaji wa samaki hivyo kwanini nchi zetu zisishirikiane kununua meli kubwa za uvuvi ili zisaidie kuongeza supply ya samaki maana kutegemea wavuvi wadogo wanaotegemea mitumbwi na nyavu tu haiwezekani kupata samaki wengi wa kukidhi soko
 
Wachina wameleta SGR kwenu Kenya mnaanza kuwatukana kwa kuwa mmeshaipata treni ya mwendo kasi sio?? Mnadhani China wanataka pesa zenyu au kununua na kuajiri watu wao??
Kuleni hio samaki kwanza mkimaliza mtakuwa na hizo madini kwa wingi mwilini. Hamtazeeka
 
Kwa sasa tunanunua ndege cash kwanza
 
Kwahiyo wewe unafurahia watanzania wenzako wapate matatizo kupitia hao samaki wa wachina?
Wachina wameleta SGR kwenu Kenya mnaanza kuwatukana kwa kuwa mmeshaipata treni ya mwendo kasi sio?? Mnadhani China wanataka pesa zenyu au kununua na kuajiri watu wao??
Kuleni hio samaki kwanza mkimaliza mtakuwa na hizo madini kwa wingi mwilini. Hamtazeeka

In God we Trust
 
Hivyo vipimo ni vya aina gani?

Hawa wanasayansi wetu nao wakati mwingine wanayo matatizo.

Hiyo 'chart' inaonyesha vipimo na kiasi walichopata, na 'Limits' zake; lakini haisemi 'units' zake ni nini, milligrams/au micrograms ama nanograms ama picograms, au ni 'asili mia'?

Je hizo limits za madini hayo, ni kiasi anachotakiwa mtu asizidishe kiasi hicho kwa siku ama?

Au ni vipimo tu kulinganisha kiasi kinachotakiwa kisizidi kwa uzito maalum wa samaki huyo?

Kuna maswali mengi hapo!

Lakini kwa upande wa pili, waChina waliweka ngumu sana kuruhusu Kenya wauze 'avocado' zao huko China kwa visingizio chungu nzima kama 'sanitary standards' hadi wakalazimu 'avocado' yawe yanagandishwa nyuzi za sentigredi chini ya -30 C jambo ambalo mkulima na wafanya biashara wadogo linawaongezea gharama mara dufu.
 
Kwanini tuagize samaki China wakati samaki wapo wa kututosha kwenye maji yetu!!?

Kama kuna uhitaji wa samaki hivyo kwanini nchi zetu zisishirikiane kununua meli kubwa za uvuvi ili zisaidie kuongeza supply ya samaki maana kutegemea wavuvi wadogo wanaotegemea mitumbwi na nyavu tu haiwezekani kupata samaki wengi wa kukidhi soko
Wacha tufe ujinga wetu ndiyo kiama chetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini tuagize samaki China wakati samaki wapo wa kututosha kwenye maji yetu!!?

Kama kuna uhitaji wa samaki hivyo kwanini nchi zetu zisishirikiane kununua meli kubwa za uvuvi ili zisaidie kuongeza supply ya samaki maana kutegemea wavuvi wadogo wanaotegemea mitumbwi na nyavu tu haiwezekani kupata samaki wengi wa kukidhi soko
Ya nini mameli yote hayo mkuu yenye gharama kubwa namna hiyo.

Nenda tu hapo kijijini kwenu kawahimize watu wachimbe mabwawa kwa wingi wakusanye maji yanayopotea bure na kuleta uharibifu.

Kwa upande wako, nenda kaweke kakiwanda kadogo ka kutengeneza vyakula vya hao samaki.

Mbona watu tunahangaika sana hivi jameni?

Hao samaki wa kichina wanaouzwa hapo Nairobi na Kisumu?, fikiria Kisumu ilipo - wote wanafugwa kwenye madimbwi tu ya watu huko uchina, halafu wanaletwa huku kutuuzia!

Na watu (vijana) kutwa nzima wapo vijiweni wakilia - "Hakuna kazi", na serikali yao nayo badala ya kuwapa nyenzo waifanye kazi hiyo, nayo wanabaki wanalilia tu.

TASAF inapunguza umaskini? Kweli? Mbona mimi hili silielewi?

Umaskini upunguzwe kwa wazee kugawiwa pesa za mkopo wa 'World Bank'?

Kwa nini hela hiyo isiwekwe kwenye miradi ya hawa vijana, nao wakawa wanatozwa kiasi cha kuwalipa hao wazee?

Huenda kuna kitu nisichokielewa kuhusu mpango huu wa TASAF.
 
Samaki wanaotoka China ni wa kufugwa,,,wao ni namba 1 duniani kwa ufugaji wa samaki.
Kwanini tuagize samaki China wakati samaki wapo wa kututosha kwenye maji yetu!!?

Kama kuna uhitaji wa samaki hivyo kwanini nchi zetu zisishirikiane kununua meli kubwa za uvuvi ili zisaidie kuongeza supply ya samaki maana kutegemea wavuvi wadogo wanaotegemea mitumbwi na nyavu tu haiwezekani kupata samaki wengi wa kukidhi soko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tusiishie kuwalaumu wachina na samaki wao... Wa kwetu wamefanyiwa utafiti na kugundulika wapo salama??
My take: Kila mtu awe makini sana na anachokula!
 
Kwanini tuagize samaki China wakati samaki wapo wa kututosha kwenye maji yetu!!?

Kama kuna uhitaji wa samaki hivyo kwanini nchi zetu zisishirikiane kununua meli kubwa za uvuvi ili zisaidie kuongeza supply ya samaki maana kutegemea wavuvi wadogo wanaotegemea mitumbwi na nyavu tu haiwezekani kupata samaki wengi wa kukidhi soko
Tanzania tuna maziwa makubwa manne pamoja na Bahari, tuna mito mikubwa mingi yenye samaki lakini bado tunaagiza samaki nje....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom