Chuo Kikuu Cha HKMU Kufanya Makubwa!, Kusafisha Figo Kwa Dialisis na Kupandikiza Mimba, IVF, 288 Wahitimu Udakitari.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,969
2,000

03/12/2017 Mchango wa Sekta Binafsi Kwenye Elimu, Wapongezwa

Mchango wa Sekta Binafsi kwenye utoaji wa Elimu ya Juu nchini Tanzania, umepongezwa na kuelezewa kuwa unalisaidia Taifa kukidhi mahitaji ya wataalamu wa fani mbalimbali, hivyo kusaidia kwenye maendeleo ya taifa.

Pongezi hizo, zimetolewa jana na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki, Dr. Salim Ahmed Salim, wakati wa mahafali ya 15 ya Chuo hicho, yaliyofanyika jana chuoni hapo ambapo jumla ya wanafunzi 288 Walihitimu kozi mbalimbali za astashahada, shahada na shahada za uzamili katika fani ya uuguzi na udakitari wa binadamu, wakiwemo wanafunzi 136 waliohitimu udakitari wa binadamu wakiongozwa na mhitimu, Dr. Delilah Mwindadi aliyeibuka mwanafunzi bora wa udakitari.

Dr. Salim amesema, tangu chuo hicho kimeanzishwa, kimetoa madaktari wengi wanaolisaidia taifa hili, hii ikiwa ni ishara ya kutimizwa kwa azma ya muasisi wa chuo hicho, Marehemu Prof. Hubert Kairuki, la kuhakikisha chuo hicho kinatoa mchango kwa maendeleo ya taifa.

Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Chuo hicho, Mama Kokushubira Kairuki, aliwataka wahitimu hao, kwenda kuyatumia mafunzo waliyoyapata kwa bidii, weledi na uadilifu, ili kuendelea kulinda sifa na heshima za wahitimu wa chuo, waliojinjengea kwa miaka mingi.

Makamo Mkuu wa Chuo, Prof. Charles Mgone, amesema wahitimu wa Chuo hicho, wamefunzwa kuweza kufanya kazi popote nchini Tanzania, na mrejesho wa wahitimu hao huko makazini ni mzuri kwa sababu ni wachapa kazi kwa kujituma kwa bidii, weledi na waadilifu sana. Kwa upande wa chuo hicho, kinaongeza kampasi nyingine, na kutanua wigo wa mafunzo na huduma za kusafisha figo, dialysis, na huduma za kupandikiza uzazi, IVF kwa wanandoa wenye matatizo ya kutopata watoto.

Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, John Ulanga, amesema, mahafali haya ya 15, ni kielelezo cha mchango wa sekta binafsi katika kusaidia maendeleo ya taifa, kwa upande wa sekta ya afya na tiba ya binadamu, hivyo akatoa wito kwa serikali na sekta ya umma, kuendelea kujenga mazingira wezeshi kuwezesha sekta binafsi, kukua na kutoa mchango wake kuisaidia serikali na sekta ya umma kuleta maendeleo ya taifa letu, kwa sababu maendeleo ya kweli, yatapatikana kwa ushirikiano wa sekta binafsi na sekta ya umma, pamoja, tutaweza.

Jumla ya wahitimu 288 walihitimu, kati yao wauguzi ni 49, shahada za uuguzi ni 22, shahada za udaktari 136, na shahada za uzamili kwenye udakitari, ni 21.
Photo 1. MK  wa Baraza la Chuo, Mkuu wa Chuo na VC wakiingia.JPG
Photo 2. Baadhi ya Wahitimu wakiingia.JPG
Photo 3. Meza Kuu Ikisimama.JPG
Photo 4. Mwanafunzi Bora wa Udaktari, Dr. Delillah Mwindadi Akitunukiwa Udakitari.JPG
Photo 6. Mhitimu Uzamili Katika Udakitari, Mrs Haika Eden Mashayo.JPG
Photo 7. Wahitimu wakila kiapo cha udakitari.JPG
Photo 7. Wahitimu wakila kiapo cha udakitari.JPG
Photo 8. Meza Kuu Wakifurahia jambo.JPG
Photo 9. Mkuu wa Chuo Dr. Salim Ahmed Salim, na Mwenyekiti wa Bodi, Wakiteta jambo.JPG
Mhitimu Uzamili 1.JPG
Mhitimu Uzamili 2.JPG
Mhitimu Uzamili 3.JPG
Mhitimu Uzamili 4.JPG
Mhitimu Uzamili 5.JPG
Mhitimu Uzamili 6.JPG
Mhitimu Uzamili 7.JPG
Mhitimu Uzamili 8.JPG
Mhitimu Uzamili 9.JPG
Mhitimu Uzamili 10.JPG

Beira Boy

JF-Expert Member
Aug 7, 2016
17,954
2,000
Pascal jana nimekuona kwenye clip moja hivi ukimponda mkulu siku zako zinahesabika lazima utakula chuma

Huwez kumtolea povu mkulu kias hicho afu ukabak salama
 
Bhikalamba

JF-Expert Member
Dec 6, 2015
870
1,000
Ni habari njema, tena njema sana.
Lakini mkuu paskali kwa habari hiyo kulikuwa na haja ya picha zote hizo? Au kuna MTU umedhamilia tumujue kuwa kahitimu, au tu umeamua kumpa promo?!!!
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,969
2,000
Ni habari njema, tena njema sana.
Lakini mkuu paskali kwa habari hiyo kulikuwa na haja ya picha zote hizo? Au kuna MTU umedhamilia tumujue kuwa kahitimu, au tu umeamua kumpa promo?!!!
Mkuu Bhikalamba, mwisho wa idadi ya picha ni 20, hapo hazijafika picha 20!.

Ila pia naomba kukiri udhaifu wa kupenda sana picha nzuri nzuri.
Tembelea hapa

Vicky Kamata Anastahili Pongezi!, Asimama Kidete Kupinga Uonevu, Ubabe na Double Standards za Zungu!

CRDB Bank -Lumumba ni "Maua" na Maua!.

Paskali
 
M kathias

JF-Expert Member
Jun 13, 2017
2,340
2,000
Kwenye kichwa cha habari , umesema waliohitimu udaktari ni 288, ndani ya habari umeandika ni 136 waliohitimu udaktari.
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,969
2,000
Wahitimu hawa ni miongoni mwa mafanikio ya awamu ya tano kutokana na mazingira mazuri na wezeshi kwa vyuo vikuu binafsi kutoa elimu yaliyokuwa set na serikali ya awamu ya tano chini ya Dr. John Pombe Joseph Magufuli, hivyo tarehe 28 October, do the right thing, mambo mazuri zaidi ya haya, yaje.
P
 
mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
51,529

Huduma za matibabu hayo yanafanyika bure au

Ova
 
kirumonjeta

JF-Expert Member
Feb 9, 2008
3,983
2,000
Wahitimu hawa ni miongoni mwa mafanikio ya awamu ya tano kutokana na mazingira mazuri na wezeshi kwa vyuo vikuu binafsi kutoa elimu yaliyokuwa set na serikali ya awamu ya tano chini ya Dr. John Pombe Joseph Magufuli, hivyo tarehe 28 October, do the right thing, mambo mazuri zaidi ya haya, yaje.
P
Kumbe kampeni??? Ahsante kaka
 
Ceftriaxon

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
213
500
Wahitimu hawa ni miongoni mwa mafanikio ya awamu ya tano kutokana na mazingira mazuri na wezeshi kwa vyuo vikuu binafsi kutoa elimu yaliyokuwa set na serikali ya awamu ya tano chini ya Dr. John Pombe Joseph Magufuli, hivyo tarehe 28 October, do the right thing, mambo mazuri zaidi ya haya, yaje.
P
Awamu ya 4 ndio iliyotengeneza mazingira bora kwa vyuo na wanafunzi kupata Elimu.
 
marxlups

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
13,795
2,000
Pascal jana nimekuona kwenye clip moja hivi ukimponda mkulu siku zako zinahesabika lazima utakula chuma

Huwez kumtolea povu mkulu kias hicho afu ukabak salama

Paskali tunayemjua sisi sote au wa kuigiza!!! can we share that
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom