Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kumtunuku Rais Magufuli Shahada ya Falsafa

Ameona afiche aibu yake ya PhD feki kwa kupewa huo uchafu.

Baada ya uzinduzi wa kitabu cha yule mstaafu wa Lupaso. Akakaa nae akamuomba yeye kama mkuu wa chuo cha kata afanye mpango wa kumpa phd ya mezani ili kuua so la phd feki

RIP Ben Saanane
 
#HABARI

*Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kesho kitamtunukia Rais Dk. John Magufuli Shahada ya Heshima ya Daktari wa Falsafa (Honorary PhD) kwa uongozi wake hususani katika ujenzi wa uchumi wa viwanda, kuwekeza kwenye elimu, miundombinu, kuimarisha utawala bora, na mapambano dhidi ya rushwa.*

wananchi wanatukanwa na hawa maprofessa, yaani amejenga vyerehani ama kitu gani?
viwanda vinafungwa , wawekezaji wanakimbia, hakuna mtu mwenye hamu na nchi , then wanamtunuku badala ya kumpa ujumbe wa kumuonya?
hii nchi ina laana ya damu za kina Ben sa 8 na Azory, alphonce mawazo na wengine wale walikuwa kwenye viroba RUVU
cleardot.gif
 
Kuna siku Huyo wanayempa heshima aliwaita Wanafunzi wa hicho chuo ni VILAZA na UDSM ni VIPANGA.

Hizo shobo za kumpa heshima wakati aliwatukana sijui inakuwaje.

Anyways, This is stupid Tanzania.
Tumefika pahala Maprofesa wamekuwa wapuuzi tu, ssamahani kwa hii lugha, yani watanzania wanaofanya tafiti, kugundua dawa, wengine wamefundisha panya kutegua mabomu hawajapewa hiyo heshma mnampa mtu anayeua viwanda kweli, WTF
 
Naomba niende moja kwa moja kwenye hoja yangu, binafsi napongeza chuo kikuu cha Dodoma kwa kutekeleza ili la kumpa Mh wetu Rais mpendwa PHD ya zawadi ya heshima.

Kwanza katika ili naomba viongozi wa vyuo watambue kuwa Mh Rais huyu tulie nae si miongoni mwa watawala wanao pendezwa na DEGREE za kupewa na si kwamba hapendi kwa ufupi ni kuwa mtu yoyote anae toka KANDA ya ziwa huwezi peleka cheti cha Degree ya kupewa pahala popote na ukaeleweka watu wa kule wanajua AKADEGREE hakagawiwi kama njugu.

Pili hii gedree ya heshima kwa Rais mimi ninaielewa ila vipengele vyote walivyoviweka kwa maana ya kushaiwishi ili jamii tujue kwa nini amepewa n kama vifatavyo.

1. Kuwezesha ujenzi wa viwanda/uchumi wa viwanda Tanzania hii ni siasa tu.
2. Kuboresha Elimu mimi najua aliamasisha elimu bure na kila mwezi anatoa pesa hakika ili nakubaliana nalo.

3. Utawala bora.

Hii no tatu Rais nadhani hata yeye akipewa nafasi aelezee utawala wa Demokrasia alio urisis kwa jakaya ndio tulio nao?

Karbuni tutafakari.
 
Lakini pia ni muda muafaka Dunia asa jeshi kumtunuku Mh.Rais wetu mzalendo nishani ya Field Marshal
 
Lakini pia ni muda muafaka Dunia asa jeshi kumtunuku Mh.Rais wetu mzalendo nishani ya Field Marshal
Makaika Mkuu King Field Marshall Dr. Pombe Jiwe Ngosha Magufuli Conquer of the Tanzania Empire.
Hii itakuwa imekaa vizuri
 
sifi leo,
Hata wakianzisha some sort of Nobel prize hapo UDOM wampe tu! au UDOM wapendekeze kwa Nobel Prize committee in Sweden apewe in any field of their choice! Ndio kujikomba kulivyo!
 
Kuna Jamaa yangu kanitonya kwamba Chuoni kwao wameshitushwa sana na UDOM kumtunuku Mkuu Phd ya Heshima hivyo na wao wanajiandaa mapema mwakani wafanye hivyo. Wanachohofia ni kwamba mkuu anaweza mind sana na pia hii ya UDOM inawapa sifa sana na huenda tukashuhudia Maprof wa UDOM wakipigwa vyeo muda wowote ule.

Hivyo kuna vyuo kama 3 vinajanidaa mwakani kutunuku mkuu Phd ya Heshima.

Kwa staili hii mkuu anaweza vunja record ya Mugabe ya Phd za heshima
 
Back
Top Bottom