Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,009
- 9,874
Katika mwendelezo wa mahafali ya 50 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Spika mstaafu, Pius Msekwa atatunukiwa shahada ya heshima ya udaktari.
Mahafali hayo yanayoenda sambamba na maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa chuo kikuu hicho pia yatamtunuku shahada ya heshima ya uzamivu Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Netumbo Nandi-Ndaitwah.
Taarifa iliyotolewa leo na makamu mkuu wa chuo hicho, Profesa William Anangisye inasema Msekwa na Nandi-Ndaitwah watakuwa kati ya wahitimu 7,091 watakaotunukiwa shahada zao zikiwamo 82 za uzamivu.
“Chuo kitamtunuku shahada ya heshima ya udaktari Pius Msekwa ambaye alikuwa makamu mkuu wa chuo wa kwanza wakati kinaanzishwa mwaka 1970. Kuanzia Novemba 30 hadi Desemba 10 chuo kinatoa bure huduma mbalimbali kwa jamii kama sehemu ya maadhimisho ya mahafali ya 50,” amesema Profesa Anangisye.
Licha ya wahitimu wa uzamivu, wanafunzi 608 watapata shahada za umahiri wakati 19 wakipewa stashahada ya uzamili. Wahitimu wa shahada za awali watakuwa wengi zaidi, Profesa Anangisiye amesema watakuwa 6,382.
“Chuo kinawakaribisha wadau wote wa elimu kushiriki maadhimisho haya maalumu,” amesema Profesa Anangisye.
Mahafali hayo yatafanyika kwa siku mbili, Jumanne na Alhamisi katika ukumbi wa Mlimani City ambako Msekwa amesema atatoa hotuba kutathmini maendeleo ya miaka 50 ya elimu ya juu nchini.
Watakaohitimu Jumanne ni kutoka ndaki ya Teknolojia za Habari na Mawasiliano (Tehama), uhandisi na teknolojia, sayansi za kilimo na teknolojia ya chakula, na ndaki ya sayansi asilia na tumizi.
Alhamisi itawahusisha wahitimu kutoka ndaki ya sayansi za jamii, insia, na shule kuu ya elimu, biashara, sheria, uandishi wa habari na mawasiliano kwa umma, taasisi ya taaluma za maendeleo, na ile ya taaluma za Kiswahili.
“Nikuombe uje ukumbini kusikiliza hotuba yangu. Nilikuwa makamu mkuu wa kwanza wa chuo hiki wakati (Mwalimu Julius) Nyerere akiwa mwenyekiti. Tuliweka misingi ya elimu ya juu nchini,” amesema Msekwa alipoulizwa tathmini yake kuhusu maendeleo ya vyuo vikuu nchini