Chuo kikuu cha Dar es salaam! Chuo pekee chenye mazingira bora zaidi Africa.

menny terry

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
509
667
Wakuu,

Chuo kikuu cha Dar es salaam yaani UDSM ndio chuo chenye mazingira bora zaidi Africa. Kampuni ya ma inginia bora kutoka Israel walifanya kazi bora sana. Miaka zaidi ya 60 sasa bado UDSM ina mvuto wa kutosha. Mvuto Na ubora wa chuo hiki umeongezwa na Library kubwa kabisa Africa Mashariki na Kati uliojengwa kwa msaada wa serekali ya China. Chakusikitisha pamoja Na ubora,,ukongwe na mvuto wa chuo hiki bado hakipo hata kwenye 30 bora Africa. Wapi wanakwama?

Nawasilisha.

Nenda udom halafu uje ufute huu uharo
 
Umetumia kigezo gani?

Je umepata kuviona vyuo vyote barani africa mpaka uje na hitimisho hilo?
 
UD ilivunjwa vunjwa kama USSR ikazaa vyuo kama 'sita' hivi. Hapo ndipo walipoimaliza UD iliyokuwa inaingia top ten.
 
Hakuna chuo kizuri Kama mwalimu Nyerere hapa dsm ktk mazingira
Hahahahaaaa MNMA!
Ndio chuo chenye Wanafunzi wanaosoma uchumi 28

Kozi ambazo hazipo katika mfumo wa utoaji ajira
MSD Tamisemi hawatambui kabisa.

Mwisho kabisa chuo hakina uhusiano wowote na umahiri wa muhusika.

Unaweza kusoma Education MNMA ukawa bora kuliko mwalimu wa mkwawa (udsm) iringa
 
Hahahahaaaa MNMA!
Ndio chuo chenye Wanafunzi wanaosoma uchumi 28

Kozi ambazo hazipo katika mfumo wa utoaji ajira
MSD Tamisemi hawatambui kabisa.

Mwisho kabisa chuo hakina uhusiano wowote na umahiri wa muhusika.

Unaweza kusoma Education MNMA ukawa bora kuliko mwalimu wa mkwawa (udsm) iiria
Unakalili Mambo?
 
By the way mama inatakiwa akae na TBA awaongezee pesa kidogo ili waongeze flr moja moja kwenye hostel za Magufuli ili ziezekwe mabati zikamilike ziwe kama Mabibo hostel... UD yetu ipendeze.
 
Udsm iliharibiwa kwa kuvunjwa vunjwa na hapo ndipo ilipopoteza kwenye ranking za vyuo.

Makerere mpaka leo ipo vile vile toka inaanza

University of nairobi, university of zambia etc zipo vile vile kama zamani

Udsm iliyokuwa ina college za kibabe kama college za land kama uclas, ina college za health kama muhas, ina college za aglicultural kama sua ilikuwa ina nguvu sana tofauti na hii iliyojaa college za ngwini tu. Ambazo hazina mchango mkubwa kwenye dunia

Ubora wa chuo kikuu chochote duniani huwa unapimwa kwa kutazamwa kwenye technology, engineering, health, agliculture, na mambo ya land. University yoyote bora duniani inaangaliwa hapo tu. Sasa udsm waliporwa hizo college
 
Ukisema UDSM unanikumbusha hawa maprofesa vituko:
1. Prof. Benson Baba
2. Prof. Kabudi
3.Dr. Mwakyembe
4.Dr. Tulia
5. Prof. Luoga
 
Back
Top Bottom