Chuo Kikuu cha Addis Ababa nchini Ethiopia kuanza kufundisha Kiswahili

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,813
4,546
Chuo Kikuu cha Addis Ababa nchini Ethiopia kitaanza kufundisha lugha ya Kiswahili baada ya kutia saini makubaliano na chuo kimoja kikuu cha Tanzania.

Masomo hayo ya lugha yatafanikishwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Hatua hiyo inajiri siku chache baada ya Umoja wa Afrika kupitisha Kiswahili kama lugha rasmi ya kazi.

Kiswahili kinazungumzwa katika nchi kadhaa za Kiafrika.

Unesco mwaka jana ilitangaza tarehe 7 Julai kuwa siku rasmi duniani ya kuadhimisha lugha ya Kiswahili.

Chanzo: Star TV
 
Alafu utasikia waalimu wanatoka Kenya, Tanzania wanao jifanya wajuzi na manguli wa kiswahili wataishia kuandaa makongamano ya kitaifa ya kiswahili.
 
Kiswahili kinapigiwa chapuo ila Kiingereza, Kifaransa, Kijerumani, Kichina ndio mpango mzima.
 
Back
Top Bottom