Chuo Kikuu bora TZ ni kipi kwa kusomea Uhasibu au Biashara? - ni UDSM, Mzumbe au IFM?

Ivi, sasa ivi hata level ya certificate na diploma unaenda NACTE. Wao ndio wanakupangia. Swali langu je? Kama mtu ana shughuli zake mkoa husika. Inakuaaje kama atapangiwa mkoa mwingine na yeye anataka abaki apo wadau tufahamishane apo
 
Ushauri pia ulinganishe na AIA kwa accounting na TIA kwa Public sector accounting & finance na pia degree ya accounting.
Mie naomba nikupatie ushauri wa kitaaluma zaidi ya habari za kusikia. Vyuo vyote ulivyotaja hapo juu vina faida na hasara zake. Pia inategemea unataka kijana wako asomee kitu gani kama ni economics, accounting , finance, econometrics, business management, management etc.

Mzumbe - kiukweli sio chuo kinachofaa kwani hakina waalimu na kinachukua walimu wake wengi IFM , na UDSM. Na sababu kubwa ni baada ya scandal ile ya vyeti feki wengi wametimka au wameamua kurudi tena shule wakasome vizuri. Ila faida yake ni kwamba gharama za ada yao ni chini kidogo kulinganisha na vyuo vyengine kama kijana wako unamlipia ada. Pia admission competition ni ndogo kulinganisha na IFM na UDSM hivyo basi unaweza kuwa na uhakika wa kupata admission.

IFM - hiki ni tertiary university ijapokuwa miaka ya karibuni wameanza kuwa wanatoa degree. IFM ni tertiary university but wameexcell vizuri sana katika sekta ya Accounting, Finance na Banking. Hivyo kijana wako ukitaka asomee sekta hizo ni bora nakushauri aende IFM kulinganisha vyuo vyote hapo hasa kwasababu sasa hivi wataalamu wengi wa finance, accounting wako IFM. Tatizo la IFM ni ada yake aghali sana kulinganisha na mzumbe sijui UDSM? Pia IFM vijana wanakuwa hawakai darasani hasa akina dada kutwa wako mitaani. Vile vile waalimu wa pale IFM kutwa wapo kwenye consultancy, research na masemina wana muda mchache wa kufundisha hilo linachangia kuleta mapungufu kwenye ufundishaji.

UDSM - Ni chuo kizuri sana kwa mtu anayekusudia kusomea Economics, Econometrics kwani kuna wataalamu waliobobea pale. Hata hivyo nao wanatatizo sawa na IFM waalimu kutwa wapo katika consultancy, research na masemina. Hivyo kijana wako kama ni kilaza anaweza kusumbuka .

SUA - Kama alivyosema mtu mmoja wazuri sana katika research na economics. Ila wanapungufu katika sekta ya decision making, accounting, finance. Kwahiyo kama unataka kijana wako awe mchumi SUA kuzuri, kama UDSM.

Zanzibar University- Ni kweli hichi ni chuo kizuri ila hakina jina. Na wanafundisha vizuri sana na wanafunzi wengi wanaenjoy pale na ada sio kubwa sana. Tatizo lake liko katika cheti (kwasababu ni chuo cha kiislamu), pia kuna tatizo la kimazingira maana kipo zanzibar, vilevile waalimu wake wengi ni kutoka nje ya nchi sasa sielewi ufanisi wao but overall vijana wamesoma pale wamemaliza na wamepata ajira.
 
Huna haja ya kumake assumption ya vitu uvionavyo bora pindi unapotafuta kitu quality, kama ishu ni popularity nenda vyuo ulivyotaja ila kama unataka kujua uhasibu basi nakushauri uende institute of accountancy of Arusha (I.a.a) chuo kinatoa taaluma ya juu sana binafsi hiki chuo nmesoma degree kiukweli nliona taaluma ya hiki chuo ipo juu sana ......N.B pale I.a.a ni kazi tu hakuna mchezo, ukicheza unakula sup, unacarry unadisco kama vp nenda C.B.E kama unataka urahisi
 
Back
Top Bottom