Chuo Kikuu bora TZ ni kipi kwa kusomea Uhasibu au Biashara? - ni UDSM, Mzumbe au IFM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chuo Kikuu bora TZ ni kipi kwa kusomea Uhasibu au Biashara? - ni UDSM, Mzumbe au IFM?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by kichwat, Apr 3, 2011.

 1. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #1
  Apr 3, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Wadau naomba msaada. Nina uncle wangu anataka kumrejesha mtoto wake aje asomee shahada ya biashara kwenye University/Chuo hapa Tanzania. Ameniomba ushauri kuhusu wapi ampeleke mtoto wake (Chuo bora kwa masomo ya Uhasibu au Biashara). Kwa vigezo rahisi vya popularity x 'quality' nimepata vyuo 3 - UDSM, Mzumbe na IFM. Naomba mwongozo kuhusu ubora (just views/ simple ranking). Naomba kuwakilisha.
   
 2. Mipangomingi

  Mipangomingi JF-Expert Member

  #2
  Apr 3, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,719
  Likes Received: 980
  Trophy Points: 280
  Kama issue ni 'popularity' mpeleke udsm,ifm au mzumbe lakini kama unataka quality ya graduand bac kuna chuo huko zenj kinaitwa Zanzibar university kinatoa vijana wazuri sana wa uhasibu/biashara believe or not! Si kwamba hicho chuo kiko ranked high,ispokuwa ma-lecturer wao wako wako kwa ajili ya kazi hiyo na hakuna leakage na kudesa wala pass/love(hizi ndo sababu za wengi niliowahoji). Tatizo la udsm,ifm ma-prof na Dr's wako buisy na politics,consultants,warsha na mishemishe nyingine!
   
 3. MwanaIFM

  MwanaIFM Member

  #3
  Apr 3, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 41
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 15
  Fuata ushauri wa mipango mingi ndugu yangu au kama ikishindwa saaaana ni bora umpeleke Mzumbe,........I am saying that kwa kuangalia hiyo popularity, environment nzuri kwa usomaji pia na hiyo factor ya huyo mchangiaji aliyetangulia lecturers wa Mzumbe hawana mambo mengi kama wa hapa mjini! last option kama kuna ulazima saana wa kusomea Dar then IFM is the place you are looking for but ni lazima awe comitted kwelikweli! I know wat am saying am in the same boat na najua vijana wadogo yanayowapata pale na nnajua hata ingekua mimi katika umri ule ingekua shida kiasi fulani, ukitaka msaada zaidi kuhusu hapo mahala feel free to ask
   
 4. R

  Ramsonlee Member

  #4
  Apr 3, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  mlete mliman huyo kijana ila acwe kilaza manake elimu ya hapa full utata na inataka m2 anayeji2ma na cyo m2 legelege UDSM NDO MPANGO MZMA
   
 5. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #5
  Apr 3, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  vilaza hawana nafasi hapa, vingnevyo ajiandae na mzigo wa sup, udbs iko kamili
   
 6. c

  chabutwa Member

  #6
  Apr 3, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamaa yangu yuko IFM, nasikia ukishikwa tu, jamaa wanadai ukate laki laki nanusu. mlimani inategemea, maana si kuelewa ni kuafaulu tu, kariri au egesha bora kufaulu. Mzumbe sijasikia baya. Yote niliyosema nimesikia tu. Mwambie jamaa yako mwache aamue mwenyewe.
   
 7. m

  matunge JF-Expert Member

  #7
  Apr 3, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 60
  Asome SUA "Bsc in Agricultural Economics and Agribusiness" atakuwa bora fanya utafiti ..kwa watumishi wa benki...na mashirika katika sekta ya biashara waliosoma hiyo kozi...wako fiti na wanawafunika wote waliosoma vyuo vilivyotajwa. Tatizo ilo jina "agricultural" na BSc vinaweza kukutisha ila niamini...kama amesoma basic applied mathematics atafanya vizuri sana tu...............na kumbuka principles za biashara ni zilezile tu hata kama chuo ni cha kilimo. SUA ni chuo bora zaidi believe me...katika interview yeyote inayohusisha wanafunzi wa masomo husika...wa sua lazima awamwage wote.....atafundishwa na maprofesa na dr tu na wote ni bora ..wanafunzi wachache.....achana na upopulality...angalia ubora wa elimu
   
 8. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #8
  Apr 3, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Asante kwa ushauri, vigezo ulivyotoa (in red) naona NAAM! ila tatizo kwa SUA ni hiyo 'Agri' tu. Labda nitumie vigezo hivyo kwa kupambanisha Mzumbe, UDSM, IFM na Zanzibar University?
   
 9. N

  Ngo JF-Expert Member

  #9
  Apr 4, 2011
  Joined: May 25, 2010
  Messages: 284
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  matunge;Asome SUA "Bsc in Agricultural Economics and Agribusiness" atakuwa bora fanya utafiti ..kwa watumishi wa benki...na mashirika katika sekta ya biashara waliosoma hiyo kozi...wako fiti na wanawafunika wote waliosoma vyuo vilivyotajwa. Tatizo ilo jina "agricultural" na BSc vinaweza kukutisha ila niamini...kama amesoma basic applied mathematics atafanya vizuri sana tu...............na kumbuka principles za biashara ni zilezile tu hata kama chuo ni cha kilimo. SUA ni chuo bora zaidi believe me...katika interview yeyote inayohusisha wanafunzi wa masomo husika...wa sua lazima awamwage wote.....atafundishwa na maprofesa na dr tu na wote ni bora ..wanafunzi wachache.....achana na upopulality...angalia ubora wa elimu


  Mwamba Ngoma naona unavutia kwako. Nilimaliza UD nisingemushauri kwa sasa ampeleke pale mwanae, ningemshauri ampleke mwanae Mzumbe kama anataka kuwa mzuri katika hiyo fani ya biashara na kumpa nafasi ya kujiandaa na ACCA au CPA baada ya kumaliza chuo. Mzumbe wanapata exemptions nyingi (cost saving) zaidi ya vyuo vyote hapa TZ kama unataka kufanya ACCA
   
 10. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #10
  Apr 4, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Hivi what about OUT (Open University) si na wao wana kozi za biashara.
   
 11. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #11
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mie naomba nikupatie ushauri wa kitaaluma zaidi ya habari za kusikia. Vyuo vyote ulivyotaja hapo juu vina faida na hasara zake. Pia inategemea unataka kijana wako asomee kitu gani kama ni economics, accounting , finance, econometrics, business management, management etc.

  Mzumbe - kiukweli sio chuo kinachofaa kwani hakina waalimu na kinachukua walimu wake wengi IFM , na UDSM. Na sababu kubwa ni baada ya scandal ile ya vyeti feki wengi wametimka au wameamua kurudi tena shule wakasome vizuri. Ila faida yake ni kwamba gharama za ada yao ni chini kidogo kulinganisha na vyuo vyengine kama kijana wako unamlipia ada. Pia admission competition ni ndogo kulinganisha na IFM na UDSM hivyo basi unaweza kuwa na uhakika wa kupata admission.

  IFM - hiki ni tertiary university ijapokuwa miaka ya karibuni wameanza kuwa wanatoa degree. IFM ni tertiary university but wameexcell vizuri sana katika sekta ya Accounting, Finance na Banking. Hivyo kijana wako ukitaka asomee sekta hizo ni bora nakushauri aende IFM kulinganisha vyuo vyote hapo hasa kwasababu sasa hivi wataalamu wengi wa finance, accounting wako IFM. Tatizo la IFM ni ada yake aghali sana kulinganisha na mzumbe sijui UDSM? Pia IFM vijana wanakuwa hawakai darasani hasa akina dada kutwa wako mitaani. Vile vile waalimu wa pale IFM kutwa wapo kwenye consultancy, research na masemina wana muda mchache wa kufundisha hilo linachangia kuleta mapungufu kwenye ufundishaji.

  UDSM - Ni chuo kizuri sana kwa mtu anayekusudia kusomea Economics, Econometrics kwani kuna wataalamu waliobobea pale. Hata hivyo nao wanatatizo sawa na IFM waalimu kutwa wapo katika consultancy, research na masemina. Hivyo kijana wako kama ni kilaza anaweza kusumbuka .

  SUA - Kama alivyosema mtu mmoja wazuri sana katika research na economics. Ila wanapungufu katika sekta ya decision making, accounting, finance. Kwahiyo kama unataka kijana wako awe mchumi SUA kuzuri, kama UDSM.

  Zanzibar University- Ni kweli hichi ni chuo kizuri ila hakina jina. Na wanafundisha vizuri sana na wanafunzi wengi wanaenjoy pale na ada sio kubwa sana. Tatizo lake liko katika cheti (kwasababu ni chuo cha kiislamu), pia kuna tatizo la kimazingira maana kipo zanzibar, vilevile waalimu wake wengi ni kutoka nje ya nchi sasa sielewi ufanisi wao but overall vijana wamesoma pale wamemaliza na wamepata ajira.
   
 12. Observer2010

  Observer2010 Senior Member

  #12
  Apr 4, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 198
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  Ulivyoandika hapo red ndio rank ilivyo. Utazunguka kufanya utafiti ila huo ndio ukweli usiopingika. Tz hakuna chuo cha kulingana na UDSM kwa vigezo vyako unavyovisema. Ila kwa upande wa ubora wa hadhi ya kimataifa, Tanzania hakuna chuo bora, ila kuna chuo afadhari. Maana yake ni kuwa vyuo vyote vinatoa elimu ya kawaida sana, hakuna madarasa ya kutosha, hakuna hostel za kutosha na mazingira kwa ujumla sio bora. Ni jambo la kawaida sana kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kukimbilia viti madarasani maana ukichelewa unaweza hata kukaa chini au kukaa kwa nje na kusikiliza lecture kwenye madirisha. Na kama atakaa hostel ni kawaida kwa wanafunzi wa vyuo kukimbilia daladala na hata kuingilia madirishani km usafiri wa mbagala.

  Elimu ya UDSM ni kama bundesliga, lazima awe amezoea mchakamchaka, kama yupo lelemama atazoa sup kapu zima na si ajabu kudisco. Kama mdau mmoja hapo juu alivyosema, competetion ya kuingia UDSM ni ya juu sana, so ni lazima awe amefaulu vizuri masomo ya A level, vinginevyo afikirie hivyo vyuo vingine, maana vyenyewe vinachukua bila competion kubwa.

  Kwa ujumla, asitegemee huo ubora unaoufikiria, sana sana ategemee mazingira ya kujirusha na kuspend, na km ni binti ndio ategemee kupata mapedeshee wanaovizia wanafunzi wa vyuo.

  :A S-omg:
   
 13. R

  Renegade JF-Expert Member

  #13
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 3,770
  Likes Received: 1,074
  Trophy Points: 280
  UBORA WA ELIMU UNATEGEMEANA NA MAMBO MENGI, KAMA DHANA ZA KUFUNDISHIA, HUPATIKANAJI WA VITABU, SUPPORT TOKA KWA WALIMU, IDADI YA WANAFUNZI KATIKA DARASA, MAZINGIRA YA KUSOMEA ,MODES OF ASSESMENT .
  LAKINI PIA MSISAHAU KUWA VYUO VYOTE HAPA TANZANIA VINAFANANA. walimu wale wale, Akikukosa Mzumbe anakukuta IFM kama siyo UD.
  JITIHADA BINAFSI YA MWANAFUNZI INATAKIWA SANA ILI KUMFANYA MWANAFUNZI KUWA BORA.
   
 14. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #14
  Apr 4, 2011
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Wekeni programme contents, itakuwa rahisi kufanya judgement.
   
 15. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #15
  Apr 5, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Ok. Kuhusu kuwa na comparable programmes, nalenga courses zifuatazo:

  ================
  UDSM:
  1. BCom - Accounting
  2. BCom – Finance
  3. BCom - Banking
  4. BCom - Marketing
  5. BBA

  Mzumbe:
  1. BAcc – BAF
  2. BAcc - Local Government & Public Sector Accounting
  3. BBA – Marketing
  4. BBA - Procurement
  5. BBA – Entrepreneurship

  IFM:
  1. Bachelor of Accounting (BAcc)
  2. Bachelor of Banking and Finance (BBF)
  3. BSc. Taxation
  ==========
  Naomba kuwakilisha.
   
 16. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #16
  Apr 5, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Kama nilivyosema mwanzo mie kuwa na pia nakushauri soma course content za BcomFinance ya UDSM na Bachelor of Banking and Finance. Utagundua kuwa kama unataka kijana wako ajengeke katika ulimwengu wa sasa in Finance and Accounting mpeleke IFM. Ikiwa kama unataka kusoma Economics au Econometrics kasome UDSM au SUA.

  Vile vile katika Accounting ni hivyo IFM ijapokuwa ni Tertiary University ila wamejijenga zaidi katika field hizo za Banking, Finance and Accounting na wanakubalika mpaka Marekani na Ulaya na Middle East (wamepublish articles zao huko). Na walimu wake wengi ndio wanafundisha pia Mzumbe, UDSM na Tumaini. Hivyo ningelikushauri kwanza soma course content zao UDSM na vile vile angalia mfuko wako. Ikiwa mfuko umetoboka basi wewe nenda Mzumbe, au UDSM (ijapokuwa sasa hivi sijui private candidate analipa bei gani). Kama mfuko umetuna kamsomeshe IFM utakubali maneno nayoyasema. Tatizo la IFM kubwa liko kwenye walimu wake na ubusy wao usiokuwa na msingi na kuna tetesi kutoka kwa wanaosoma huko pia mitihani migumu wanayoitunga inawaumiza vijana.
   
 17. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #17
  Apr 5, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Nimesahau ila ukitaka kijana asomeshwe vizuri na kufatiliwa maendeleo yake basi mpeleke Zanzibar University nasikia wanafatilia kwa ukaribu sana maendeleo ya vijana wao. Ila sijui course content zao zimebadilika last time niliziona ni afadhali ukasome UDSM au IFM ila tatizo la vyuo hivyo ni walimu wako busy mno na mishe mishe zao.
   
 18. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #18
  Apr 5, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  ..ni kweli, OUT wanazo, LAKINI kiukweli QUALITY ya elimu bado haiaminiki sana sokoni. (ushabiki pembeni)
   
 19. funzadume

  funzadume JF-Expert Member

  #19
  Apr 5, 2011
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 6,494
  Likes Received: 2,090
  Trophy Points: 280
  SUA ni kuzuri kwa baadhi ya masomo kama walivysema hapo juu kuna maprofesa wengi na wazuri wa Economics na pia BSc Agricultural Economic and Agribusiness na MBA Agribusiness na Msc Agicultural Economic ni kozi zilizotulia sana
   
 20. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #20
  Apr 5, 2011
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,425
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 160
  Ongeza ARDHI UNIVERSITY BAF= Bachelors in Accounting and Finance na BA in Economics
   
Loading...