Chuo cha Uvuvi Tanga chauzwa kwa bei ya kutupwa na Halmashauri ya Wilaya ya Pangani. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chuo cha Uvuvi Tanga chauzwa kwa bei ya kutupwa na Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by nngu007, Mar 28, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  WAKATI serikali ikikemea vitendo vya ubadhilifu wa fedha na mali ya umma kuna taarifa kuwa halmashauri ya wilaya ya Pangani inakabiliwa na tuhuma ya kuuza Chuo cha Uvuvi kwa gharama ya kutupa ya milioni 57.
  Hayo yameelezwa na baadhi ya madiwani wa wilaya hiyo walipozungumza na mwandishi wa habari hizi jana kwa njia ya simu kuwa wana pinga uwaumuzi huo uliojaa ujanja ujanja, haukufuata matakwa ya wadau hivyo kutaka mkataba huo uvunjwe mara mojana.
  Diwani Seif Ali akiongea kwa niaba ya wenzake alisema hawakubaliani na taratibu zilizotumika kuuza Chuo hicho kutokana kwamba gharama zilizotumika haziendani na thamani halisi ya chuo hicho.
  “Gharama ni ndogo ukilinganisha na ukubwa wa chuo chenyewe ila kilichotumika ni usanii huenda pesa zilizotolewa ni nyingi lakini zikaandikwa hizo wakati thamani halisi ya mauzo inakadiliwa ingefikia sh mil.700,” alilalamika Ali huku akiungwa mkono na wenzake.
  Aidha, Ali alibainisha kuwa hakukuwa na haja ya kukitupa chuo hicho kwa bei ndogo kama ile wakati kungefanyika mipango ya kuwapata wawekezaji huku majengo yakibaki ya halmashauri ya wialaya hiyo milele.
  Katika hali ya kujichanganya katika kujibu tuhuma hizo Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Neneka Rashidi, alikanusha habari hizo kuwa chuo hicho hakijauzwa kilichofanyika wamepewa taasisi ya Chuo Kikuu inayojishughulisha na viumbe bahari ili kukiendeleza. Alisema fedha hizo sh mil. 57 zilizotolewa ni kifuta jasho ambacho ameshindwa kuzitolea maelezo ya kuridhisha kwamba katika stakabadhi zao za kumbukumbu wameziandikaje huku akikata simu. Naye Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Salimu Sinani, alitofautiana na mkurugenzi huyo kwa kusema chuo hicho hakijauzwa bali kimekodishwa ambapo hana taarifa kama kuna kifuta jasho kilichotolewa na taasisi hiyo ya chuo kikuu hali iliyozidi kutia shaka katika upatikanaji wa fedha hizo sh mil. 57.
   
 2. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mmh, Mwandishi!,

  Kimeuzwa au kukodishwa?

  Ni vyema utafiti wa kina wa kujua undani ukafanyia. Yaonyesha hata anayedaiwa kukodishwa ("taasisi ya Chuo Kikuu!!") ni kana kwamba hawajaulizwa kama walinunua au wamekodi na kama kukodi ni tasisii ipi na kwa masharti gani (miaka mingapi na kodi wanalipa kwa utaratibu upi??)...
   
 3. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Haina mashiko!
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Tanzania ukikodisha ndio kuuza hakuna ufuatiliaji
   
Loading...