Chuo cha Usafirishaji chawa rasmi Chuo Kikuu na Shahada 6 adimu, Wabongo tuzichangamkie! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chuo cha Usafirishaji chawa rasmi Chuo Kikuu na Shahada 6 adimu, Wabongo tuzichangamkie!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Pascal Mayalla, Feb 16, 2012.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,307
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,


  Chuo cha Usafirishaji nchini, NIT, kimepewa changamoto ya kuukabili upungufu mkubwa wa watalaamu waliobobea kwenye taaluma ya uchukuzi na usafirishaji ili pato la sekta hiyo lichangie katika kukuza pato la taifa na mchango huo uchangie kuinua uchumi wa nchi yetui.

  Changamoto hiyo, imetolewa leo na Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Eng.Omari Nundu (Mb.) wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa mitaala sita mipya ya Stashahada za Uzamili (Postgraduates Diploma), zitakazoanza kufundishwa na chuo hicho mwezi Aprili mwaka huu 2012, uliokwenda sambamba na uzinduzi wa ujenzi wa jengo jipya la chuo hicho lililopo Mabibo Dar es Salaam.

  Waziri Nundu. Amesema, Tanzania imezungukwa na mataifa mengi yalifungiwa (land locked ) hivyo sekta ya usafiri na ushafirioshaji ni sekta muhimu sana kwa uchumi wa taifa, ila mpaka sasa mchango wa sekta ya uchukuzi na usafirishaji katika pato la taifa ni mdogo ukilinganisha mahitaji halisi, na kutolea mfano mwaka 2009 sekta hii ilichangia asilimia 7.1 tu ya pato la taifa kutoka asilimia 6.1 mwaka 2005.

  Nae mwenyekiti wa baraza la udhamini la chuo hicho, Bibi, Prisicilla Chilipweli amesema chuo chake kimeshaanza kuzifanyia kazi changamoto hizo kwa kubuni kozi mpya zinazohitajika katika soko la ajira hivyo kuwataka Watanzania wachangamkie fursa hizo huku akizitaka taasisi mbalimbali kuwafadhili watumishi wao au kuwadhamini Watanzania kusomea fani hizo ambazo sasa zinatolewa nchini kwa gharama nafuu.

  Naye Mkuu wa Chuo Hicho cha Usafirishaji, (NIT), Eng.Dr.Zacharia M.D. Mganilwa Alizitaja kozi mpya kuwa ni
  1. ’Postgraduate Diploma in Air Transport Management’
  2. ’Postgraduate Diploma in Shipping and Port Management’
  3. ’Postgraduate Diploma in Logistics and Transport Management’
  4. ’Postgraduate Diploma in Travel and Tourism Management’
  5. ’Postgraduate Diploma in Procurement and Logistics Management’ na;
  6. ’MBA - Logistics and Transport Management’
  Chuo cha Taifa cha Usafirishaji kilianzishwa mwaka 1975, chini ya lililokuwa shirika la uchukuzi la Taifa (NTC), kwa madhumuni ya kutoa huduma za kitaalamu kwa makampuni tanzu yaliyokuwa chini ya shirika hilo. Baadaye kupitia sheria ya bunge Na. 24 ya mwaka 1982 serikali ilikipandisha hadhi na kuwa taasisi ya elimu ya juu na kukipa majukumu ya kufundisha, kufanya utafiti na kutoa ushauri wa kitalaamu katika sekta ya usafirishaji na uchukuzi. Kwa sasa Chuo kipo chini ya Wizara ya Uchukuzi. Chuo kina usajili na ithibati ya Baraza la Taifa la Ufundi (NACTE).
  MY Take.
  Kwa vile hizi ni kozi adimu haswa kwa wanaopenda kupata ajira mashirika ya kimataifa, nawashauri wenzetu haswa wanaomaliza form six msikimbilie vyuo vikuu kichwa kichwa huku huna uhakika wa ajira kwa unachokwenda kusomea, fikiria kujiunga na chuo kama NIT, ukimaliza hapo ni ajira nje nje na starting salary zake, take home sio chini ya Dola 2,000 kwa mwezi!.

  Pasco.
   
 2. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2012
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Huwa nakukubali sana Pasco kwa nyuzi zako,japo kuna muda huwa unanichefua sana haswa ukileta habari za lile ***** lowasa
   
 3. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  pasco unapenda ushabiki!!inaonyesha wewe ni muandishi wa magazeti ya udaku.hivi majuzi pinda alisema serikali imesitisha kuvipandisha hadhi vyuo mbalimbali vya ufundi stadi,badala yake vibuni kozi mbalimbali zitakazosomwa na wale wa diploma na vyeti.haya yalisemwa na pinda akiwa arusha tech college.sasa nakushangaa pasco unakuja na thread yenye kumpinga waziri wako mkuu,huoni kwamba unaiharibia serikali?
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,494
  Trophy Points: 280
  hio namba 4 nani atakuajiri? au usome tu
   
 5. M

  Mxelodkw New Member

  #5
  Feb 16, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ziko vizuri
   
 6. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #6
  Feb 16, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Chuo cha usafirishaji NIT hakijageuzwa kuwa chuo kikuu bali ni kutokana na mfumo wa NACTE ambao unaviwezesha vyuo vya elimu ya juu visivyokuwa vyuo vikuu(tertiary institutions/non university higher learning institutions) kuweza kudahili, kufundisha na kutunuku shahada ya kwanza, shahada ya uzamili hadi shahada ya uzamivu.

  Kwahiyo kilichofanyika hapo ni uzinduzi wa mitaala ya stashahada za uzamili (post graduate diplomas) katika fani za uchukuzi na usafirishaji ambazo zimeidhinishwa na NACTE. Katika mfumo huo chuo hakilazimiki kugeuzwa kuwa chuo kikuu bali kinawezeshwa kutoa tuzo za juu kama vyuo vikuu.

  Na kwa mfumo huo wa NACTE ndipo unaona karibia vyuo vyote vya elimu ya juu kuanzia DIT, NIT, TCA, IFM, CBE, TIA, ISW, RWI na vingine vya aina hiyo vinatoa astashahada, stashahada, shahada, stashahada za uzamili na shahada za uzamili.

  Hapa vyuo vya VETA havihusiki kabisa, kwani bado mhitimu wa VETA hawezi kutumia matokeo yake ya VETA kupata admission ktk vyuo hivi.
   
 7. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #7
  Feb 16, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145

  Mkuu hapo si ndipo tunaambiwa kila siku kwamba foreiners wamejazana nchini kwakuwa hatuna wataalamu? bora sasa NIT wameileta ili tuisome, mimi mwenyewe nafikiria kuomba kozi hiyo!!
   
 8. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  ndio maana napinga title aliyoweka pasco kwani imekaa kiudaku.
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,307
  Trophy Points: 280
  Mkuu Matumbo, kazi ya uandishi haihitaji kubagua, ni kama kazi ya taxi driver, wote ni abiria wangu. Ikitokea nimekutana na habari ya CCM au Kikwete, naleta, ikitokea habari ya Chadema, Dr. Slaa, Mbowe, Zitto hata Lissu, naleta, ikitokea habari ya CUF, Maalim Seif, Lipumba, Jussa, Mtatiro pia na naleta, vivyo hivyo kwa Lowassa au whoever!. Tuna tatizo humu jf la wengi kuegemea chama fulani, hivyo nikileta habari yoyote kinyume cha matarajio yao, cha moto utakipata!.

  Wito kwa wanajf, tukubali political tolerence, tukubali differing idears, tujifunze political divesity ya kuwakubali hata tusiokubaliana nao. EL is a human being kama walivyo wengine wote na anastahili rights zote kama mimi na wewe!.
   
 10. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #10
  Feb 16, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  acha ubishi we soma tuuuuuu.....
  Utaambiwa sio lazima uajiriwe, jiajiri...
   
 11. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #11
  Feb 16, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,307
  Trophy Points: 280
  Mkuu Meningits, kwenye mambo ya elimu ya juu, who is Pinda?, hizi nilizokupa ni nondo za leo na full of facts!. Nakushauri usiwaaminie sana wanasiasa, mara nyingi hutoa political statements for political gain, tena Pinda ndio usimzungumzie kabisa, ni nyanya kabisa!.

  Juzi wakati wa mgomo wa madaktari kawaita Jumapili, wao wakamwambia Jumatatu, akajiona yeye ni shoka, hakubali Jumamatu, na kuwatishia nyau!. Kilichofuata si wote mlishuhudia alivyokwenda kuwalamba miguu!. Kwenye hili la hizi kozi za NIT, nawashauri msimsikilize Pinda, fuatilieni addmission mjiunge msome, tusilete siasa kwenye elimu!.
   
 12. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,321
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  Hivi tunaelewa vema roles na vyuo vikuu na nini tunahitajika kukifanya kama tunataka mafanikio? Guys, lets change our mindset na kujifunza kuiangalia hii dunia na opportunities zake kama vile ilivyo
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,307
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mwita Maranya, asante sana kwa hoja hii, nakukubali uko juu sana na mimi umenifungua macho, japo kimoyo moyo naumizwa na Veta kutoingizwa kwenye mpango huu!.
   
 14. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #14
  Feb 16, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,321
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  Tuache sasa hivi kusoma tukijiandaa kuajiriwa tu...until when tutawatumikia watu wengine ilhali nafasi za kutoka zipo wazi kwa watanzania wote ambao watakuwa na nidhamu na kujituma??? Elimu ni taa inayotuongoza njia na kamwe tusiitumie kama kifungo cha kuwatumikia watu wengine.
   
 15. m

  mwasumbi Member

  #15
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Hapo Pasco umeprove uweledi wako na ufanisi katika kazi yako hao wanaokuponda nadhani hawana sifa za kusoma kozi hizo ndiyo maana wanaleta longo longo, siye watanzania tunakushukuru kutuletea info za kutufanya tupate sifa za kuwazidi wakenya wanaotuchukulia post zetu katika soko la ajira. Vijana twendeni tukapige nondo hizo za NIT tutoke!
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #16
  Feb 16, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,307
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mtakatifu Ivuga, Watanzania tuna tatizo kubwa la wataalamu wa hiyo number 4, Wakenya ndio wameshika upper hand!. Asilimia 90% ya mameneja wote wa hoteli za maana ni foreiners, kati ya mameneja wazawa wachache wa hoteli za maana ni Nderumaki aliyekuwa Holiday Inn, Ngewe wa Kempiski, na yule mzee Sebastian aliyeko Sea Cliff baada ya kutoka Mt. Meru, the rest ni Wakenya na Wazungu kisa Watanzania hatuna watu hao!.

  Hata Arusha meneja mzawa ni Moleli aliyeko pale Impala, ila hoteli nyingine za bosi huyo huyo mwenye Impala, Naura Spring na Ngurdoto ameweka Wakenya!. Watanzania ni walalamishi, wavivu na watu wa visingizio kibao!. Sasa mnapewa opportunities, mnaanza oh.. oh.., subirini Wakenya waje mpaka wajaze hizo nafasi ili waendelee kupandia mpaka vichwani!.
   
 17. +255

  +255 JF-Expert Member

  #17
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,908
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 180
  Kunat tofauti gani kubwa kati ya 3&5 au ndo ilimradi kuongeza idadi ya kozi! Af sijaona uadimu wa hz kozi mbona zilishaanza kutolewa na baadhi ya vyuo hapa TZ, labda hy 1&2
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Feb 16, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,565
  Likes Received: 18,307
  Trophy Points: 280
  3. 'Postgraduate Diploma in Logistics and Transport Management'
  5. 'Postgraduate Diploma in Procurement and Logistics Management'

  Can't you really see the difference?.
   
 19. +255

  +255 JF-Expert Member

  #19
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,908
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 180
  Najua kuna Utofauti ila kwa upande wangu naona ni mdogo sana hadi ziwe kozi mbili tofauti..Sidhani ka mtu aliyesoma Procurenent & logistics mgt atashindwa kufanya kazi za mtu wa Logistics & Transport mgt
   
 20. R

  RUTARE Senior Member

  #20
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 10, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waliomaliza form six wana qualification ya kudahiriwa kwenye hizo course?
   
Loading...