saigilomagema
JF-Expert Member
- Jun 5, 2015
- 4,149
- 6,142
Chuo cha Uhasibu Arusha(IAA) ni chuo kinachomilikiwa na Serikali yetu kupitia wizara ya fedha. Kama ilivyo vyuo vingine vya elimu ya juu na vyuo vikuu wanakuwa na upungufu wa teaching staff(walimu). Tatizo la hawa jamaa ni arrogance yaani kujisikia, majivuni, kujiona wa kipekee wakati ukweli ni kwamba ni chuo cha kawaida kabisa hata siyo Univeristy.
Siku za hivi karibuni walitangaza nafasi kadhaa za part-time, walitaka utume CV na nakala(copies) za vyeti. Sasa cha ajabu eti part-time teaching unataka umfanyie interview mtu ambaye CV yake inaonesha tayari anafundisha aidha ktk chuo kingine cha elimu ya juu au chuo kikuu kingine? Are you serious guys? Kwa kazi ya miezi 4 tu? Mtu atoke Dar Es Salaam, Dodoma,Mwanza au Mbeya kuhudhuria interview siku 2 kwa kazi ya miezi 4?
Kwa hiyo nyie hamuamini vyuo vingine vya elimu ya juu vilivyowaajiri hao wahadhiri? Acheni kiburi na dharau kwa kudhani kuwa watanzania ni maskini kiasi hicho. Msiwanyanyase watanzania kwa kutumia kodi zao wenyewe, hizo pesa ni kodi za watanzania isiwaleweshe.
Nitamshangaa sana mtanzania atakayekubali udhalilishaji huu kwa kuhudhuria hayo ma-interview yao. Watakulipa nini kuzidi utu wako, viwango vyao vinajulikana kwa saa unalipwa sh. 18,000/ jumlisha 10,000/ ya nauli jumla sh. 28,000/. Kwa wiki utafundisha masaa 4 utavuna sh. 112,000/. Semester haizidi wiki 16 ukimaliza vizuri utaambulia sh.1,792,000/. Ukitoa gharama utakazokuwa umetumia plus hii ya interview huna cha maana utakachobakiwa nacho.
Point yangu hasa siyo malipo ni dharau na udhalilishaji eti mtu tayari umeshafundisha miaka pengine km 15 na zaidi ktk vyuo vingine uje ufanyiwe interview na vitoto vidogo kwa kazi ya muda mfupi. Ni vyuo vingi tu vinachukua part-timers hawafanyi upuuzi huu, unawapatia CV yako na pengine unaonesha vyeti au unawaachia nakala za vyeti inatosha. IAA badilikeni enendeni km wenzenu.