Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) chatoa somo kwa Waratibu wa Matukio

Apr 9, 2022
66
32
IMG-20230413-WA0072.jpg

Chuo cha utalii nchini (NCT) kimewataka wadau wa uratibu wa matukio (events), kuongeza ujuzi wao kwa kujifunza chuoni ili kukuza weledi na kuacha tabia ya mazoea katika utendaji kazi wao wa kila siku.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano kati ya NCT na wadau wa uratibu wa matukio Kaimu Makamu mkuu wa chuo,Taaluma,Tafiti,na ushauri Jesca william amesema lengo la kukutana na wadau hao ni kujadiliana kwa pamoja na kuangalia namna ya kujenga uwezo zaidi wa watoa huduma wengine katika tasnia ili chuo kiweze kuzalisha watoa huduma wanaoenda na mahitaji ya sasa ya soko.

"Tunambua kuwa tasnia ya uratibu wa matukio inamchango mkubwa sana katika kukuza utalii,tutakubaliana wote kwamba tukio ambalo limeratibiwa vizuri linaweza likawa na mafanikio sana kwa wageni kuliangalia na kupenda sana kushiriki".

Lakini pia tasnia hii inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa Taifa kufikia malengo yake yakuweza kufikia watalii milioni tano ifikapo mwaka 2025, kwahiyo tunatambua ni sekta muhimu sana ambayo sisi kama chuo cha Taifa cha Utalii ni lazima tuangalie namna tunakwenda kutengeneza watu ambao wataendana na mahitaji ya soko la sasa".

Aidha amewataka wadau mbalimbali wanaojihusisha na maswala ya uratibu wa matukio wakimo washereheshaji(Mc), wapambaji, wapishi, waratibu tukio (events plan) na wengineo kushiriki kwenye mafunzo ya muda mfupi yatakayoanza kutolewa chuoni hapo kwa siku tatu kuanzia march 15-17 mwaka huu 2023 ili kuongeza ujuzi wao katika uratibu wa matukio yao.

Kwa upande wake mmoja wa wadau wa matukio Mc Enna Kiondo amesema katika tasnia hiyo inahitaji watu wanaoweza kupangilia vizuri matukio, hivyo wanashukuru chuo cha utalii kwa kuja na program hiyo ambayo itasaidia kuboresha sekta na kukuza weledi zaidi.

Nae Mahsein Awadhi maarufu kama Mc Dr Chen amesema licha ya mtu kiwa na kipaji fulani ni lazima kipaji hicho kinolewe kwa kupewa maarifa kutoka chuoni na kumwezesha mtu huyo kuwa bora zaidi hivyo amewataka wanatasnia hiyo kutafuta zaidi maarifa na kuacha kutumia uzoefu pekee katika utekelezaji wa majukumu yao.
 

Attachments

  • 1.jpg
    1.jpg
    40.6 KB · Views: 2
Back
Top Bottom