Mhesh.Raisi wetu mpendwa JPM na Mhesh. Waziri wa Sheria na katiba Kabudi, sisi watoto wa walalahoi wenye nia ya kusoma chuo hicho cha mafunzo kwa vitendo ya sheria tunaomba sana kihamishiwe DODOMA. Gharama za kuishi Dar es salaam kwa miezi 6 pamoja na kwenda kusupp ni kubwa sana.Maisha huwa magumu na stress kubwa kwasababu ya gharama ya maisha ya Dar. Kwaajili ya kulinda masilahi ya wanyonge tunaomba chuo hicho kihamishiwe Dodoma. Watanzania wengi wanashindwa kuhudhuria chuo hicho kwasababu ya gharama ya maisha ya Dar. Hivyo waliowengi wanaomuda gharama za kusoma ktk chuo hiki ni watoto wa matajiri.Sisi walalahoi.ni vigumu kusoma ktk chuo hicho kwasababu ya gharama za maisha ya Dar.Dodoma ni katikati, hivyo ni jirani na kila mkoa.Hata gharama za vyakula na vyumba ni chini.Tunaomba kwa unyenyekevu mkubwa Raisi wetu mperndwa na waziri wa sheria mtusaidie kwa hili, ili na sisi watoto wa walalahoi tupate fursa ya kuwa MAWAKILI. Asante