Chuo cha Ardhi Morogoro chapima viwanja 40,813 ndani ya miezi miwili

Abuka

JF-Expert Member
Sep 17, 2013
247
241
Katika kipindi kuanzia mwezi Desemba 2020 hadi mwezi Februari 2021 Chuo cha Ardhi Morogoro kimefanya upimaji wa viwanja elfu arobaini mia nane kumi na tatu (40,813), kati ya hivyo viwanja 19,102 vipo Jijini Arusha katika Mitaa ya Mlimani (9,420), Msasani (1,349), Muriet (5,820), Mtaa wa Mashariki (1,041) pamoja na Mtaa wa FFU (1,552). Viwanja vingine ni Manispaa ya Iringa viwanja 2,385 Halmashauri ya Rombo viwanja 1,523 Halmashauri ya Wilaya Same viwanja 176, Halmashauri ya Wilaya ya Moshi viwanja 1,076.

Kwa upande wa Dar es salaam, Chuo cha Ardhi Morogoro kimepima Halmashauri ya Jiji (Ilala) viwanja 5,981. Manispaa ya Temeke viwanja 1,112. Manispaa ya Kigamboni viwanja 2,675. Pamoja na Manispaa ya Kinondoni viwanja 1,000. Mkoa wa Mtwara, Chuo cha Ardhi Morogoro ndani ya muda huo kimepima viwanja 1,084 katika Halmashauri ya Nanyumbu, huku viwanja 4,699 vikiwa katika eneo la Manispaa ya Morogoro.

Ni mara ya kwanza katika shughuli za urasimishaji makazi, kampuni binafsi au taasisi kufanya upimaji mkubwa kiasi hicho kwa kutegemea michango ya wananchi. Mkuu wa Chuo hicho Bw Huruma Lugalla amesema kwamba huo ni mwanzo tu kwani mpango mkakati mpya wa Chuo wa miaka mitano kuanzia 2021 – 2024 umejaa maboresho makubwa na kasi ya ajabu kuhakikisha Taasisi hii pekee ya serikali inayozalisha wataalamu wa upimaji na ramani katika ngazi ya cheti na Diploma na kwamba Watanzania wategemee mambo makubwa katika sekta ya Ardhi. Bw Lugalla ameongeza kwamba yote haya yamewezekana chini ya uongozi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Aidha, Makamu Mkuu wa Chuo hicho Bw Charles Saguda, ambae pia ni msimamizi mkuu wa Miradi ameongeza kwamba chuo kimeandaa mpango kabambe wenye kuleta matokeo chanya katika miradi yote inayosimamiwa na chuo, amesema wameanza na Mkoa wa Arusha na Sasa ni zamu ya Dar es salaam na baadae nguvu kazi kuhamia Mkoa wa Morogoro. Bw Saguda alisema kwamba lengo kubwa ni kuongeza wigo wa walipa kodi ya ardhi, ambapo kwa mchanganuo huo tayari kanzidata ya walipa kodi ya ardhi imeongezeka na serikali inaongeza mapato.

Chuo cha Ardhi Morogoro kimepitia mabadiliko makubwa ya kiutawala baada ya miradi kudhoofu kwa kipindi cha nyuma, kwa sasa mabadiliko na hatua mbalimbali zilizochukuliwa kwa baadhi ya watumishi zinaonekana kuleta tija na ufanisi zaidi katika utendaji.

IMG-20210313-WA0010.jpg
 
Hongere kwao.

Mtaani kwetu wao ndio walikuwa Wakandarasi. Lakini utendaji wao umeacha maswali mengi. Mradi bado kukamilika. Na yajayo hayaeleweki vema kwa wananchi.
 
Hongere kwao.

Mtaani kwetu wao ndio walikuwa Wakandarasi. Lakini utendaji wao umeacha maswali mengi. Mradi bado kukamilika. Na yajayo hayaeleweki vema kwa wananchi.
Sasahivi tumeboresha sana huduma, Tutumie malalamiko yoyote info@arimo.ac.tz tutayafanyia kazi haraka
 
Hizi ni siasa tu.

Hao Jamaa wapo slow, wanatumia instruments handheld ambazo Zina wigo usiokubalika wa makosa na walipita mitaa yetu 2018 na risiti zipo mpaka leo Hamna kitu.

Kiufupi ni bora liende.
 
Hizi ni siasa tu.

Hao Jamaa wapo slow, wanatumia instruments handheld ambazo Zina wigo usiokubalika wa makosa na walipita mitaa yetu 2018 na risiti zipo mpaka leo Hamna kitu.

Kiufupi ni bora liende.

Miaka mitatu kupima na kutoa hati, mpaka leo hata namba ya kiwanja haijafika. Watu wanajinasibu kinafiki.

Ukiuliza, bado mchakato kule halmashauri. Mara mashine itapita mara ya mwisho, mara tujazie fomu yetu kuhakiki waliolipa.

Yaani vululu vululu tu, hawako organized.
 
Hata walipopotelea hatujui .... Ukiweza ita private, wanakupelekea Kila kitu wizarani kwa sababu ndiyo haohao watu wa wizarani.
 
Ule mgogoro wa ulaji pesa ktk hii miradi mmesha upatia ufumbuzi? Ndg Kaduguda na wenzie walitajwa ktk ile taarifa ya mabilioni ya pesa
 
Hata walipopotelea hatujui .... Ukiweza ita private, wanakupelekea Kila kitu wizarani kwa sababu ndiyo haohao watu wa wizarani.

Wakati mwingine si vyema kumshika simba akiyejeruhiwa sharubu akiwa amelala. Wakae hukuhuki kimya, tuendelee na maisha yetu.
 
Kampuni Binafsi zinafanya Vizuri saana Kwenye hili zoezi la Urasimishaji, na naweza sema Mchango wake ni mkubwa kuliko taasisi zote za Serikali kwa Ujumla Wake.
Sema tumekua Hatupati Recognition au Endorsement. Ila Hongereni Chuo cha Ardhi Morogoro kwa kazi mliyoifanya.
 
Back
Top Bottom