CHUNYA, MBEYA: Watu 4 wafariki, 7 waokolewa baada ya kufukiwa na kifusi mgodini

Ava Sancez

Member
Jan 27, 2017
33
50
Habari wakuu,

Habari za kusikitisha kutoka Mbeya ni kuwa Watu 4 wamefariki, 7 wameokolewa baada ya kufukiwa na kifusi wakati wanachimba dhahabu katika machimbo huko Chunya.

Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi.

=======

Watu wanne wamefariki na saba kujeruhiwa baada ya kufukiwa na kifusi walipokuwa wanachimba dhahabu katika mgodi usio rasmi kijiji cha Itumbi Kata ya Matundasi Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa amesema waliofariki ni pamoja na Simon Majaliwa(25)mkazi wa kijiji cha Itumbi, Mazoea Mahona(25)mkazi wa Tabora,Benny Bahati(23)mkazi wa Mapogolo Chunya na James Alinanuswe(26)mkazi wa Tukuyu Rungwe.
Madusa amesema kuwa waliojeruhiwa ni Andrew Paul(26)mkazi wa Itumbi ,Marco Frederick(22)mkazi wa Itumbi,Isack James(30)mkaziwa Itumbi na Hamisi Mwalyosi (25)mkazi wa Mapogolo.

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Chunya amesema kuwa watu watatu walimbia baada ya tukio hilo ili kukwepa mkono wa sheria. Miili yote imetambuliwa na ndugu ambapo wamekabidhiwa kwa ajili ya taratibu za mazishi na majeruhi wamelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Chunya wakipatiwa matibabu.Hata hivyo Madusa amesema kuwa watu hao walivamia mgodi huo asubuhi februari 20 mwaka huu ambapo mmiliki wake hajafahamika na kuanza kuchimba dhahabu bila kuchukua tahadhari hasa katika kipindi hiki cha mvua.

Baada ya udongo kuporomoka juhudi za uokoaji zilianza na watu saba walinusurika ambapo watatu walikimbizwa hospitali ya Wilaya ya Chunya na watatu walitokomea kusikojulikana. Mkuu wa Wilaya ametoa wito kwa wananchi kuacha kuendesha shughuli za uchimbaji bila kibali na kuchukua tahadhari hasa katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha mkoaani Mbeya
 
Hivi ni kwamba ardhi imekuwa unstable au? Mbona machimbo yanameza watu hivi!
 
Hivi ni kwamba ardhi imekuwa unstable au? Mbona machimbo yanameza watu hivi!
Njaa Kali watu wanawaza kupata pesa tu..wanasahau usalama wao has a wakiwa ni wachimbaji wadogo hawafati ipasavyo njia zinazoweza kuzuia ajari kama hizo.
 
Taarifa nilizozipata ambazo hazijathibitishwa ni kuwa watu wengi wamefukiwa kwenye mgodi Chunya, mtoa taarifa anasema mpaka sasa mvua kubwa inaendelea kunyesha....

Chanzo inasemekana ni baada ya gari kukosea njia na kutumbukia kwenye shimo la mgodi.
 
Ee Mungu wanusuru waja wako
 
Ni kuwa mgodi umetoa dhahabu nyingi baada ya watu kusikia wakavamia mgodi ndo yakatokea hayo.Kama nilivyozipata
 
Taarifa nilizozipata ambazo hazijathibitishwa ni kuwa watu wengi wamefukiwa kwenye mgodi Chunya, mtoa taarifa anasema mpaka sasa mvua kubwa inaendelea kunyesha....

Chanzo inasemekana ni baada ya gari kukosea njia na kutumbukia kwenye shimo la mgodi.
Usiandike kitu ambacho huna uhakika hizo tetesi ukisikia we unakimbilia social media kuandika
 
[QUOTMimi dawa, post: 19807620, member: 67357"]Nashukuru mkuu kama na wewe umezipata hizo taarifa.![/QUOTE]
Mkuu mimi ni mdau wa hii biashara huku chunya, ila idadi ya watu waliofukiwa ndio sina uhakika nayo
 
Usiandike kitu ambacho huna uhakika hizo tetesi ukisikia we unakimbilia social media kuandika
Kwa JF hata tetesi ni habari pia, na kuna post hapo juu nayo imeongelea hilo swala....

Na huko sehemu ni porini mawasiliano ni shida mvua kubwa inanyesha....

Nina ndugu yangu nae alienda jana baada ya kusikia mgodi 'umetema' kufika leo anakutana na hilo janga ikabidi afikie kwenye ukoaji..

Maana hiyo tumewasiliana nae amepona.....

Ndio maana nimeweka kama tetesi habari zingine mamlaka husika zitadhibitisha .
 
idawa said:

Ni kwenye msitu eneo la MATUNDASI
 
[QUOTMimi dawa, post: 19807620, member: 67357"]Nashukuru mkuu kama na wewe umezipata hizo taarifa.!
Mkuu mimi ni mdau wa hii biashara huku chunya, ila idadi ya watu waliofukiwa ndio sina uhakika nayo[/QUOTE]
Poleni sana Mkuu, kuna ndugu yangu ameingia leo asubuhi huko baada kusikia mgodi umetema, bahati nzuri anafika tu ndio anakutana na hilo tukio hivyo ikabidi aendelee na uokoaji...
 
Mkuu mimi ni mdau wa hii biashara huku chunya, ila idadi ya watu waliofukiwa ndio sina uhakika nayo
Poleni sana Mkuu, kuna ndugu yangu ameingia leo asubuhi huko baada kusikia mgodi umetema, bahati nzuri anafika tu ndio anakutana na hilo tukio hivyo ikabidi aendelee na uokoaji...[/QUOTE]
Ndiye aliyekwambia watu 50? Waliofukiwa ni 11 na wamepona 7 na wanne wamefariki
 
Poleni sana Mkuu, kuna ndugu yangu ameingia leo asubuhi huko baada kusikia mgodi umetema, bahati nzuri anafika tu ndio anakutana na hilo tukio hivyo ikabidi aendelee na uokoaji...
Ndiye aliyekwambia watu 50? Waliofukiwa ni 11 na wamepona 7 na wanne wamefariki[/QUOTE]
Ndio maana nikasema ni tetesi.
 
Back
Top Bottom