Elections 2010 Chunya kumekucha wachakachuaji wawekwa lupango

mwalimumpole

Member
Oct 17, 2010
48
0
Wasimamizi watatu wa uchaguzi chunya wamewekwa ndani kwa tuhuma za uchakachuaji, habari kamili zinamtaja afisa elimu kilimo bwana mbulule na afisa ukaguzi na mhusika mwingine ambaye hajafahamika jina wamewekwa ndani toka jana jioni kwa tuhuma za uchaguzi. Inasadikiwa matokeo yaliyokuwa yanapikwa na yale yanayotoka maeneo ambayo mpinzani wa ccm ndungu sunday sanga anakubalika zaidi. Hatima ya matokeo ya chunya haijulikani.
 
kama ni kweli hapo safi maana sehemu nyingi wamefanya nani hafadhari wamebambwa. Stupid kabisa....
 
nani wa kumfunga paka kengele... Jumuiya ya ulaya imeshatoa tamko kuwa MAFISADI wamebebwa na vyombo vya usalama. eti Kijana muuza mihogo na mihuri ya NEC!! Watanzania tukaze buti nchi hii si ya genge dogo la majambazi pekee...
 
kibaha, tmk,kigoma mjini, segerea, na sasa chunya!!!!????
 
icon1.gif
Re: Chunya kumekucha wachakachuaji wawekwa lupango


nani wa kumfunga paka kengele... Jumuiya ya ulaya imeshatoa tamko kuwa MAFISADI wamebebwa na vyombo vya usalama. eti Kijana muuza mihogo na mihuri ya NEC!! Watanzania tukaze buti nchi hii si ya genge dogo la majambazi pekee...

Tupe taarifa ya huo mkasa wa jinsi walivyowekwa lupango........................
 
jamaa walikusanya matokeo sehemu anakokubalika zaidi mpinzani badala ya kuwasilisha kwa mkurugenzi wakajifungia mahali na kuanza kupika, wakiwa wamezima simu zao baada ya kutafutwa kwa muda wa masaa kadhaa ndipo walipogunduliwa kwenye ilikokuwa ofisi ya elimu ya zamani wakiwa wanaandika taarifa upya. vyombo vya dola vikawaweka chini ya ulinzi mpaka sasa.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom