Chunya: CHADEMA wadaiwa kuvunja masanduku ya kura na kuiba fedha za uchaguzi

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Vurugu Chunya

TUESDAY, DECEMBER 11, 2012




397010_495898903784361_1374130767_n.jpg


WATU 13 akiwemo diwani wa viti maalumu kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) kata ya saza Benadetha Zacharia(38) wanashikiliwa na jershi la polisi kwa kufanya vurugu zilizosababisha uharibifu wa mali ya umma yakiwemo masanduku ya kupigia kura.

Wengine ni katibu wa Chadema kata ya Saza wilayani Chunya Braison Mwasimba(34),John Mponzayo(52),Seleman Tanganyika(24),Ambokile Francis(23),Amos Joseph(24),Abdul Mwandeule(20),Christopher Mwanjayo(37), Baraka Saul(19),Musa Mnyonga(32),Essa Pius(18),Marco Gibson(25) wote wakazi wa kata ya Saza na Paradiso Emanuel(26) mkazi wa kijiji cha Njenjele wilayani Mbeya.

Kamanda wa polisi mkoani hapa Diwan Athuman alisema kuwa mnamo desemba 8 mwaka huu majira ya saa 11:15 katika ofisi ya afisa mtendaji wa kata ya Saza baadhi ya wananchi wakiongozwa na watuhumiwa waliamua kujichukulia sheria mikononi na kusababisha uharibifu wa mali za umma.

Kamanda Athuman alitaja uharibifu uliofanyika kuwa ni kuvunjwa kwa kioo cha mbele cha gari yenye namba SM 3830 Toyota Landcruiser mali ya halmashauri ya wilaya ya Chunya,kuvunja mlango na dirisha la ofisi ya afisa mtendaji kata.

Alisema hbaada ya uharibifu huyo watuhumiwa waliingia ndani ya ofisi hiyo na kuharibu masanduku 24 ya kupigia kura ambapo thamani ya mali zote bado haujafahamika.

Alisema chanzo cha vurugu hizo ilikuwa kushinikiza kuzuia kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya mwenyekiti wa kijiji na vitongoji uliokuwa ufanyike siku ya jumapili.

Kufuatia vurugu hizo uchaguzi huo ililazimu kusogezwa mbele siku moja na kufanyika jana(Disemba 10) huktaratibu za kisheria zikiendelea ikiwemo kufikishwa jana mahakamani katioka mahakama ya wilaya ya Chumnuya watuhumiwa 12 na kusomewa mashitaka.

Ukiachilia mbali shitaka la uharibifu wa mali za umma linalowakabili washitakiwa wote mahakamani hapo washitakiwa Amos Joseph,Braison Mwasimba na Paradiso Emanuel wanakabiliwa na shitaka jingine la unyang'anyi.

Alisema washitakiwa hao walifanya unyang'anyi wa fedha kiasi cha shilingi 2,150,000 zilizokuwa sehemu ya gharama za uchaguzi,simu ya kiganjani na saa ya mkononi.
 
Mbona wa VYAMA vingine hawashikwii? Hata CHAMA TAWALA???
 
Tatizo ni nini mpaka yatokee hayo?
Source ni gazeti la Habari leo, ni propaganda za kutengenezwa ili Chadema ionekane ni chama cha fujo.

Badala ya gazeti kujikita kwenye kiini cha tatizo wao wameshupalia Chadema.
Nani ataamini habari kama hii?
 
Asante kwa kuligundua hilo kaka, ila kitaeleweka tu hiyo 2015:boxing::boxing:
 
hiyo ni introduction tuu tusubiri mengi zaidi magamba yanakufa na mtu, chadema lazima kukaza buti sana, maana ccm ni kama farasi anayekufa teke lake la mwisho ni baya sana!
 
Source ni gazeti la Habari leo, ni propaganda za kutengenezwa ili Chadema ionekane ni chama cha fujo.

Badala ya gazeti kujikita kwenye kiini cha tatizo wao wameshupalia Chadema.
Nani ataamini habari kama hii?

Hiyo ndio kazi waliyopewa na CCM,hawana habari zingine za kuandika zaidi CHADEMA.
 

Alisema washitakiwa hao walifanya unyang'anyi wa fedha kiasi cha shilingi
2,150,000 zilizokuwa sehemu ya gharama za uchaguzi,simu ya kiganjani na saa ya mkononi

Mambo ya kupika habari kazi kwelikweli, fedha za gharama za uchaguzi wa kijiji zilikuwa kwenye masanduku ya kura!
 
Back
Top Bottom