Chungwa: Unazijua faidi hizi 13 za tunda hili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chungwa: Unazijua faidi hizi 13 za tunda hili?

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Oct 20, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  ORANGE.jpg


  Ni msimu mwingine wa machungwa, yamejaa tele kila kona. Shilingi 100 tu unapata chungwa. Lakini siyo ajabu kama kuna watu msimu unaisha hawajala hata chungwa moja, wala suala la matunda halipo kabisa katika orodha ya milo yao!


  Inawezekana pia hata kwa wale wanaokula, japo kidogo, hula kama kiburudisho tu bila kujua faida zake mwilini. Katika makala ya leo nitakujuza faida 13 unazoweza kuzipata unapokula chungwa, ambalo limesheheni virutubisho kibao.

  Kumbuka kuwa hata chungwa moja tu ukila lina kidhi yale mahitaji muhimu ya mwili ya kila siku (daily requirement), iwe chungwa lenyewe au juisi yake halisi.

  1. UKOSEFU WA CHOO
  Kutokana kuwa na kiwango kikubwa cha kirutubisho aina ya kambalishe (fibre), chungwa husaidia usagaji wa chakula tumbuni na hutoa ahueni kwa mtu mwenye matatizo ya ukosefu wa choo. Aidha, kambalishe huondoa kolestro na huimarisha kiwango cha sukari mwilini, hivyo chungwa ni zuri kwa wagonjwa wa kisukari.

  2.UGONJWA WA MOYO
  Kiwango kikubwa cha Vitamin C na virutubisho vya ‘flavonoids’, ‘phytonutrients’ vilivyomo kwenye chungwa, huondoa kwa mlaji hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo (Cardiovascular disease)!

  3. SHINIKIZO LA DAMU
  Virutubisho vya Magnesi (Magnesium) na ‘hesperidin’ vilivyomo kwenye chungwa, husaidia kuondoa tatizo la shinikizo la damu la juu (high blood pressure), hivyo machungwa ni mazuri kwa wagonjwa wa presha.

  4. UGONJWA WA MAPAFU
  Chungwa pia lina kiasi kikubwa cha Vitamin B6 na Madini ya Chuma (iron), virubisho ambavyo ni muhimu kwa uzalishaji wa seli nyekundu za damu, ambazo hufanya kazi ya kusafirisha hewa ya oksjeni mwilini, hivyo kuwa muhimu kwa kujikinga na ugonjwa wa mapafu.

  5. MIFUPA NA MENO
  Chungwa lina kiasi kingi cha madini ya kalisi (calcium) ambayo ni muhimu kwa uimarishaji wa mifupa na meno.

  6. AFYA YA NGOZI
  ‘Anti oxidants’ iliyomo kwenye chungwa, hutoa kinga kwenye ngozi ili isiharibike au kushambuliwa na magonjwa ya ngozi yanayoweza kujitokeza kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Pia huifanya ngozi ‘isizeeke’.

  7. KOLESTRO
  Virutubisho vilivyomo kwenye chungwa, hasa kwenye maganda yake, hupunguza kiwango cha mafuta mabaya mwilini (bad cholesterol). Hivyo kwa wenye tatizo la lehemu wanashauriwa kula machungwa pamoja na nyama zake.

  8. UKUAJI WA UBONGO
  Chungwa moja lina kiasi cha asilimia 10 ya ‘folic acid’ inayohitajika mwilini kila siku. Madini haya ni muhimu kwa afya ya ngozi na ukuaji wa ubongo kwa ajili ya kuimarisha kumbukumbu na uwezo wa mtu wa kufikiri.

  9. KINGA YA MWILI
  Vitamin C iliyomo kwenye chungwa huimarisha uzalishaji wa seli nyeupe ambazo ni muhimu kwa uimarishaji wa kinga ya mwili. Unapokuwa na kinga imara, huwezi kusumbuliwa na magonjwa mara kwa mara, yakiwemo malaria.

  10. UGONJWA WA FIGO
  Ulaji wa machungwa mara kwa mara, ukusaidia kujiepusha na ugonjwa wa figo kwa kiasi kikubwa.

  11. VIDONDA VYA TUMBO
  Unapokuwa na kiwango cha kutosha cha Vitamin C mwilini, una uhakika na kinga dhidi ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo, na kama tayari unavyo, ulaji wa machungwa utakupa ahueni.

  12. UGONJWA WA MAFUA
  Kutokana na wingi wa virutubisho vya kinga vilivyomo kwenye chungwa, ulaji wake mara kwa mara utakuepusha na magonjwa ya kuambukiza na vairasi (virus), kama vile mafua ambayo hivi sasa yanawasumbua watu wengi. Hivyo kula machungwa mengi kadii uwezavyo ili ujiepushe na mafua.

  13. KINGA YA MAGONJWA MENGI
  Chungwa, siyo tu linatoa kinga kwa magonjwa yaliyoainishwa hapo juu, bali pia hutoa kinga hata kwa magonjwa mengine kama vile baridi yabisi (arthritis, rheumatism), pumu, kikohozi, kifua kikuu, nimonia na kisukari. Nakushauri kula machungwa au juisi yake halisi kuanzia leo ili kupata faida hizo.
   
 2. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,108
  Likes Received: 6,583
  Trophy Points: 280
  Asante kwa elimu Mkuu.
   
 3. M

  Mwera JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante sana kwa elimu mkuu,ubarikiwe.
   
 4. harakat

  harakat JF-Expert Member

  #4
  Oct 20, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  poa kaka nimeipenda nilkua sijui
   
 5. M

  Mr.Davis New Member

  #5
  Oct 20, 2011
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahsante sana brother ningependda unisaidie katika hili...Je? ni tunda gani ambalo linasaidia kuimarisha nguvu za kiume??
   
 6. ERIC JOSEPH

  ERIC JOSEPH JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ukiwa na jambo jingine usisite kutujuza elimu mkuu hongela kwa hilo
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Sababu 9 muhimu zinazo sababisha upungufu wa nguvu za kiume
  Zipo sababu nyingi zinazosababisha wanaume kupungua nguvu za kiume katika hizo ni hizi zifuatazo:
  1.ubugiaji wa tumbaku .
  2.uvutaji wa sigara.
  3.utafunaji wa mirungi.
  4.unywaji wa pombe.
  5.kupooza kwa mwili kunakosababishwa na maradhi.
  6.ugonjwa wa kisukari.
  7.kujisaidia kwa njia ya mkono. (Punyeto)
  8.kuwa na mawazo kupita kiasi.
  9.kufanya kazi ngumu.

  TIBA YAKE:
  chukua mbegu za tikiti maji zikaange halafu zitwange ili zitoe unga, chukua juici ya kitunguu thaumu lita moja na asali lita moja changanya pamoja juisi ya kitunguu thaumu na asali weka na vijiko kumi vikubwa vya unga wa tikiti maji koroga vizuri na uwe unakunya dawa hii kikombe kimoja cha kahawa mara tatu kila siku kwa muda wa wiki moja.

  Chanzo: Mzizimkavu

  [​IMG]
   
 8. M

  Mhutu Member

  #8
  Oct 20, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 74
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante sana na Mungu akubariki!
   
 9. mgodi

  mgodi JF-Expert Member

  #9
  Oct 20, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,309
  Likes Received: 974
  Trophy Points: 280
  Tunashukuru sana mkuu.
   
 10. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #10
  Oct 20, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tunashukuru
   
 11. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #11
  Oct 20, 2011
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Thank U Mzizi 4 this useful post
   
 12. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #12
  Oct 20, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  ahsante ndugu.
   
 13. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #13
  Oct 21, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  Nilikuwa najua chungwa linatibu mafua tu, nashukuru.
   
 14. m

  majogajo JF-Expert Member

  #14
  Oct 23, 2011
  Joined: Oct 9, 2011
  Messages: 321
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  nimekukubari kwenye tiba ya nguvu za kiume..nashkuru mkuu mungu akuzidishie
   
 15. Bei Mbaya

  Bei Mbaya JF-Expert Member

  #15
  Oct 23, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,265
  Likes Received: 226
  Trophy Points: 160
  shaka yangu ni hapo unaposema chungwa huleta ahueni kwa wenye vidonda vya tumbo

  acid yote iliyopo kwenye chungwa(naomba kusahihishwa)
   
 16. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #16
  Oct 23, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Vitaminic vya kumwaga.

  vitamin c-1.JPG
   
Loading...