Chungeni waandishi wa habari wa arusha ni wezi

BigMan

JF-Expert Member
Feb 19, 2007
1,096
135
ARUSHA PRESS CLUB (APC)
P.O BOX 6011
ARUSHA, TANZANIA
TEL; 0713-231752 / 0754-299861
Email;arushapressclub@gmail.com


TAMKO LA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA ARUSHA (APC) JUU YA TUHUMA ZA WIZI WA LAPTOP KWA MWANDISHI MAGESA H. MAGESA.

CHAMA cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC), kinawajulisha waandishi wa habari mkoa wa Arusha, wadau na jamii kwa ujumla kuwa kina laani vikali kitendo kilichofanywa na mwandishi wa habari wa kujitegemea wa gazeti la Majira Magesa H Magesa kujaribu kwa nia ovu iliyo kinyume na misingi ya taaluna ya habari na sheria za nchi kuchukua LAPTOP isiyokuwa mali ya kwake kwenye semina ya Tanzania Public Health Association TPHA iliytofanyika Corridor Spring Hoteli mjini Arusha,Novemba 29,mwaka huu.

Kitendo hicho kimeidhalilisha, kimesikitisha na kimeiabisha tasnia nzima ya habari si mkoani Arusha tu bali nchi nzima kwa ujumla wake. Hivyo basi APC kinapenda kuomba radhi kwa wadau wote walioguswa na tukio hilo kwa namna moja au nyingine.

Ieleweke kwamba APC haihusiki kwa namna yoyote ile na uovu uliokithiri wa baadhi ya waandishi wa habari na kamwe haitafumbia macho masuala kama hayo.

Kwa mujibu wa Katiba yake, APC itawatetea, kuwalinda na kuwapigania wanachama wake watakao nyanyaswa, kuonewa na kubugudhiwa wakati wa utendaji wa shughuli halali za kitaaluma na nyingine za kijamii na si vinginevyo.

Kwa misingi hiyo basi, na kwa kufuata Katiba ya APC, Kamati Kuu ya APC baada ya kupokea taarifa hizo na kujadili kwa kina tukio hilo ovu,na kwa kutumia kipengele cha 3 (c) cha Mamlaka na mipaka ya Kamati ya Haki,meamua kusitisha uanachama wa Magesa H. Magesa kwa muda hadi hapo uchunguzi wa tukio hilo, unaohusisha vyombo vya dola, utakapokamilika.

Katika kipindi hicho Magesa H. Magesa amevuliwa uanachama wa APC kwa mujibu wa Katiba ya Chama, na hata ruhusiwa kujihusisha na jambo lolote linalohusiana na APC.

APC inapenda kuchukua nafasi hii kuwaonya wanachama wake wenye tabia zinazokinzana na uandishi wa habari,na zenye dalili za makosa ya jinai kuwa haitasita kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya watakaothibitika kufanya hivyo ikiwa ni pamoja na kuwafukuza uanachama kwa mujibu wa Katiba.

Aidha, APC inawaomba wadau wote wa sekta ya habari mkoani Arusha kutoa ushirikiano wa dhati kwa APC ikiwa ni pamoja na kuwaripoti chamani mara moja waandishi wote watakao kuwa na tabia hizo ikiwa ni pamoja na wale wanaovamia mikutano, semina na shughuli nyinginezo bila ya kualikwa.

Daima tutashirikiana na wadau wote wa habari katika kuhakikisha kuwa fani ya uandishi wa habari mkoani Arusha inaboreshwa kwa manufaa ya jamii nzima



Eliya Mbonea
Katibu Mkuu-APC

December 2, 2010


Nakala .

UTPC
RPC -Arusha
RC -Arusha
DC -Arusha
MCT
Gazerti la Majira
Jukwaa la Wahariri
 
wote tu wezi wanapishana aina ya vitu wanavyoiba wengine wanaiba glass sahani wengine wanaiba waume wa wenzao wengine note book bado kuna matapeli anataka alipwe kwa makini ya wenzake mm niliwahi kuwait kwenye event yangu walinitesa sana
 
Huyu angefanikiwa kuiba bila kukamatwa, angeonekana "amecheza deal". Marafiki na wafanyakazi wenzake wangemuona "mjanja". Unfortunatelly hiyo ndio Tanzania ya sasa! Wizi, rushwa, dhuruma huitwa deals.

APC inabidi msiishie kumfuta huyu uanachama. Endeleeni kwa kuifundisha jamaa tabia njema na kukemea wote wenye tabia zisizofaa. Tumieni media kuleta maana bora ya neno "deal".
 
kwani hao viongozi mikono yao misafi ,yaani inatakiwa waambiwe ambae hawajawahi kuiba ampige magesa wote wangekimbia
 
Jamila omary yeye alitapeli watu kuwa anagombea ubunge wa viti maalum akatuomba tumchangia sikuwahi kusikia hata akichukua fomu ss ukimuuliza anakwambia kura hazikutosha wkt alitugeuza desi
 
mngemsachi sehemu za siri msingekosa umma na vijiko huwa wanafilisi sana mahotel makubwa wakienda ****** unahisi wanajisaidia kumbe watu wanaumia....wenye mahotel chungen sana semina za waandishi wa habari noma
 
Nasubiri tamko la Gazeti la Majira ili niweze kumhukumu.Kuna ulazima gani wa kutoa kopi ya barua kwa wanasiasa(DC na RC)?.Nachelea kusema huenda pia alikuwa na bifu na viongozi wa klabu.
 
Barua inahusu Magesa H. Magesa, inakuwaje kichwa cha habari hii iwe "Waandishi wa Habari Arusha wezi?

BigMan change the topic.
 
ni sawa magesa ni sehemu ya wezi hao hivyo ni utambulisho wao

We acha kashfa kwa waandishi.

Ina maana ukiambiwa mwanaume x ni malaya ina maana na wewe ni malaya?,au samaki mmoja akioza.

Kumbuka kuwa fani ya habari ni kama fani nyingine hivyo si ajabu kukuta miongoni mwao wapo wezi,vibaka,wahuni nk

usidhani waandishi miungu watu,wana mapungufu kama binadamu wengine

kama mtu huyo ameiba laptop ahukimiwe kivyake,siyo waandishi wote wa Arusha

Kumbuka SIYO LAZIMA ATAKACHOFANYA MWANAUME,MWANAMKE JIRANI YAKO BASI TUKUUNGANISHE NA WEWE
 
hata sielewi hii habari, loh

Nilifikiri ni mimi peke yangu ambaye sikuielewa.
Aya ya kwanza tayari wameishamhukumu kwa kumlaani mwenzao kwa kitendo chake cha kujaribu kuchukua LapTop ya mtu kwa nguvu.
Kwenye aya ya Tano wanasema baada ya kupokea taarifa ya TENDO HILO OVU wamesimamisha, sio kumfukuza moja kwa moja, mhusika hadi pale Uchunguzi wa tukio hilo unaohusisha vyombo vya dola utakapofanyika.

Kama walijua kuwa kuna uchunguzi wa Vyombo vya dola unafanyika, kwa nini wameishamhukumu mwenzao kuwa amefanya Tendo Ovu la kujaribu kuchukuaLTop ya mtu kwa nguvu??
Kwa nini Walikimbilia kutoa taarifa ya kumlaani mwenzao wakati wanasubiri hatua sheria zichukue mkondo wake?
Itakapogundulika kuwa mwenye LapoTop kumbe alimuomba jamaa amchukulie halafu akapiga kinwaji akasahau watafanyaje?

....Kumbiliwa kwao kumlaani mwenzao kunaleta picha moja tu. Anayesemekana kuibiwa Laptop ni mtu mzito.

 
i know them all ni wajanjawajanja kila mmoja ukikaa naye anakwambia yeye ndiye bora wenzake hawana ustaarabu wkt ktk hali halisi wote walewale matapeli tu , ukimuuliza elimu yk ndiyo kabisa wengine wanafanya kazi kwa kuwa na mahusiano na waganga wa kienyeji wakibisha nitawataja majina hizi dtls nilizipata toka kwao wenyewe
 
nimempigia mmoja wa viongozi wa apc anasema suala hili lina mambo mengi wako kwenye kikao wanalijadili
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom