Chuma wa Kaole tunakukumbuka

Mohamed Ismail

JF-Expert Member
Mar 16, 2014
214
229
Sitakuomba radhi na nitangaze rasmi kuhusu kile ambacho naenda kunena kuhusu wewe. Nikikosea na ndio kawaida ya binadamu mimi ni mwanadamu lazima nikosee na mimi siyo wa kwanza watangulizi wetu Adam na mwenzie walianza kumkosea Mungu sembuse mimi na wewe.

Watanzania wanakukosea sana ila na wewe umewakosea sana labda ndio maana wanajitia wendawazimu kwa kuweka kiboriti machoni na kukufanya hawakuoni. Hivi yule Chuma wa Kaole ambaye alitufanya enzi hizo kushinda kwenye majumba ya watu kuangalia uigizaji wake na umahiri wa usukaji wa hadithi wa michezo ya enzi hizo. Ujue huyu namzungumzia Gervas Kasiga ambaye ndio kwanza ni kinda yuko Sekondari pale Jitegemee.

Zile filamu ulizoandika ukiwa kwenye vimbweta vya pale Udsm ukishangiliwa na ngedere ,kama Unfortunate love hujui kwamba bado tunasikia mwangwi wake. Usiwaaminishe watu kwamba wakorea wameingilia soko letu la hasha naamini ule utunzi uliobora ndio umepotea mwachoni mwa watu.

Tatizo langu mimi kiherehere lazima niseme kwa sababu taa unayomulika kuangalizia hata mimi huwa napata huo huo mwanga kiduchu kuangalia na mimi yanayonihusu. Leo hii Kiswahili ndio kinawekewa nguvu wakati wewe ndio yule ambaye unajitoa muhanga asubuhi na mchana kuhakikisha kiswahili kinabaki kuwa chanzo cha ubunifu wetu.

Kwenye sanaa mimi nitakuita mbobevu mahiri na msomi kwenye uwanda wa filamu, sanaa za maonyesho na fasihi ya kiswahili. Muziki ndio chakula chako unajua tulipotoka, tulipo na tunakoelekea. Yule swaiba wako Bakari Masasi sasahivi anachokifanya kutwa kuwaelezea wachina habari zako ambapo mimi hata nusu ya anayojua kukuhusu sifikii. Swebe yuko pale Kawe redioni anabaki kusema kipo chuma huko kimekwiva na hakina hata kutu.
Muhogo Mchungu sitaki kumsemea maana anajua yeye mwenyewe anachokifkiria. Bongo movie wanalia wanamtaka Chuma wao sasa mimi ni nani nisikukumbushe kuwa bado unahitajika.Chrissant Mhenga anasema anakudai sana na unajua dawa ya deni ni kulipa hivyo fanya hima.

Una deni na watanzania na watanzania wana deni na wewe. Ila mimi ninachowakumbusha tu kwamba ni wao tu nafasi bado ipo ya wao kukutumia na wewe vilevile nafasi bado ipo ya kuwatumikia.

Mlimwengu mimi najua nikiongea sana ninaweza kukufuru niishie kwa kukutakia heri ya kuzaliwa na uishi miaka mingi ili tuweze kufaidika na akili yako. Siyo kwamba tunakupenda sana ila akili na hekima zako ndio zinatufanya tuendelee kujipendekeza kwako kwa maslahi ya bongo zetu na ustawi wa nchi yetu kwa ujumla.

Najua hunaga baya na mtu na wewe baya yao kwako huipokea kama fursa ya kujifunza( kuona bin safari).

Happy birthday comrade.
#birthdaywishes
#mlimwengumimi
f0269319-7f08-4c8f-bdca-41d5e985c542.jpg
 
#mlimwengumimiView attachment 1694428
Huyu ndie chuma bhana sijui kwanini jamaa haitolei sana macho hii tasnia
 
Nampendaga huyo kaka.

Heri ya siku ya kuzaliwa kwake..aishi maisha marefu🥂
 
Kusoma kwingi nahisi ndio kumempoteza jamaa ilan nguli fulani hivi hata tuliokuwa tukiona n star wa bongo movie...swags zote waliiga kwa huyu jamaa!

Happiest birthday Nguli!
 
Nadhani anaifukuzia PHD sasa hivi. Huyu sasa hivi ni level ya juu sana. Hawezi kuambatana na utapeli wa Azam na sinema zetu. UDSM pale watu wanakula sana pesa za miradi ni moja wa wizi mtiifu kwa madaktari na Maprofesa wengi pale Mlimani.
 
Unamsema Rwekiza Mukandara na fedha za utafiti za REDET?
 
Back
Top Bottom