Chukueni tahadhari namba hii ni tapeli kupitia Tigo pesa

Good Father

JF-Expert Member
Feb 28, 2014
9,254
2,000
Habari za wakati huu mabibi na mabwana.
Nawapa taarifa hii mapema ili mchukue tahadhari dhidi ya wizi wa kitapeli kupitia tigo pesa.

Namba hii 0658 13**39, itakupigia kama mtoa huduma wa tigo, atajitambulisha vizuri kabisa, atakutajia location yako na atakwambia ni lini mara mwisho ulitembelea service center ya tigo pesa (Tigo shop).

Ni wizi flani wa kishamba ila ni vema taarifa ukawa nayo, atakwambia Tigo inakupa zawadi ya dakika 2000, 10 GB za data na pesa taslimu 200,000. Atakutaka utaje salio lako la Tigo pesa kwa wakati huo.
Usithubutu kutaja salio lako, ukitaja ataanza kukupa maelekezo ya kijinga kijinga na usipokua makini ndio unakua umeibiwa.

Alinipigia siku chache zilizopita baada ya kumbaini na kumwambia ni mwizi akakata simu, na ukijaribu kumpigia haiwezekani.

Kampuni ya Tigo kuna baadhi ya wafanyakazi wenu ni majambazi kabisa, wanashirikiana na wezi ndio mana wezi wanapata taarifa zetu na kutupigia simu.
TCRA na vyombo vya ulinzi na usalama ingieni kazini.
 
Last edited by a moderator:

danali

JF-Expert Member
Jan 30, 2012
1,137
2,000
Asnte kwa taarifa
Ila ni muhimu siku izi kua makini muda wote na hasa masuala ya kifedha mtandaoni
Kila kukicha matapeli wanabuni njia mpya ya kukamilisha lengo lao
Ni kua makini tu kwakweli hakuna mjanja ambae hana mjanja zaidi yake
 
mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
8,411
2,000
Mwingine anatumia namba 0620398269 kusambaza ujumbe huu:
Hongera!!!
Namba yako imechaguliwa kushinda Tsh10,000,000 katika droo ya JUMATAMU JENGA na BIKO.Ili uweze kutangazwa mshindi unatakiwa ulipie UPFRONT FEE (ADA YA UTANGULIZI) bima ya ushindi wako asilimia 1.18% sawa na Tsh118,000 kupitia namba 0738782918 kisha utapigiwa simu ukiwa umeunganishwa na vyombo vya habari kuutangazia umma ushindi wako.
LIPA MAPEMA ILI USIPOTEZE NAFASI YA USHINDI
 
Lagrange

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
2,093
2,000
Kuna siku niliwahoji tigo kwanini kila wizi unahusisha sana mtandao wao kwenye ukurasa wao wa Facebook hawajanijibu mpaka Leo baada ya kulizwa 201,111 za kitanzania,

Kiukweli huenda kuna wafanyakazi wa kampuni ya Tigo sio waaminifu, ni stori ndefu sana mpaka nikalizwa hiyo laki mbili.

Hata mtandao wa halotel kias flani nao unahusika sana kwenye utapeli tafaut na mtandaon mingine kama voda & na airtel.

Tuwe makini, tusifuate maelekezo ya kijinga tunapopigiwa simu na watu tusio wafahamu.
 
Hammaz

JF-Expert Member
May 16, 2018
3,659
2,000
Juzi nilipigiwa kwa hiyo namba asubuhi mapema eti Tigo huduma kwa wateja. Alikuwa ni mwanamke, nikajifanya kama bwege namsikiliza tu kuhusu huduma mpya za Tigo. Nikamuuliza "unahuduma nyengine ya kuniambia kwa ajili ya wateja"? Na ni lini mmeanza kutumia namba zinazofanana na namba za wateja wenu? Akajaa upepo sauti yake ikaanza kuwa ya mkwaruzo, yupo kama huamini piga huduma kwa wateja. Wakati Tigo huduma kwa wateja wanawake wao sauti zao ni nyorooooro. Likakata simu.
 
Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Sep 29, 2016
6,745

Mkuu hakuna dhahama ndefu kushindwa kuisimulia kwa wenzako.
Kuficha habari na matukio makubwa kama uliyofanyiwa wewe ni kulea na kuwanufaisha wezi.
Mbona mtoa mada amesimulia vizuri tu kisanga ambacho wala hakijajaza page, kwani cha kwako ni kirefu kiasi gani hadi kushindwa kukisimulia?
Tujuze ulivyolambwa hiyo laki mbili na ushee ili members tujenge uzoefu wa kujihami.
 
"Tangu lini namba zenu huduma kwa wateja zikafanana na namba za wateja?"
Mkuu ulijiandaa sangapi na jibu zito namna hiyo kwa huyo tapeli?
Kiukweli namba za huduma kwa wateja ni tofauti na za wateja na watu wengi hawafuatilii technic hizo, na ndiyo maana wanaingia kichwakichwa na kupigwa.
Nimefurahishwa sana na aina ya mtego wa swali uliomuwekea huyo mumiani.
 
Lagrange

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
2,093
2,000
Mkuu natumia simu ndo maana ningekuwa na komputa ingekuwa rahs zaid kwangu , nilitaman kuandika hapa nilivolambwa laki 2 ndani ya dakika chache kabisa
Wory out kesho ntaandika hapa .
Mkuu hakuna dhahama ndefu kushindwa kuisimulia kwa wenzako.
Kuficha habari na matukio makubwa kama uliyofanyiwa wewe ni kulea na kuwanufaisha wezi.
Mbona mtoa mada amesimulia vizuri tu kisanga ambacho wala hakijajaza page, kwani cha kwako ni kirefu kiasi gani hadi kushindwa kukisimulia?
Tujuze ulivyolambwa hiyo laki mbili na ushee ili members tujenge uzoefu wa kujihami.
 
Hammaz

JF-Expert Member
May 16, 2018
3,659
2,000
"Tangu lini namba zenu huduma kwa wateja zikafanana na namba za wateja?"
Mkuu ulijiandaa sangapi na jibu zito namna hiyo kwa huyo tapeli?
Kiukweli namba za huduma kwa wateja ni tofauti na za wateja na watu wengi hawafuatilii technic hizo, na ndiyo maana wanaingia kichwakichwa na kupigwa.
Nimefurahishwa sana na aina ya mtego wa swali uliomuwekea huyo mumiani.
Ahsante kwa hill Mkuu.

Samahani, una maanisha nini unaposema Mumiani? Nitoe ujinga tafadhali kama hautojali.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom