Chukua tahadhari unapotoa pesa kwenye ATM, na kwa wakala, tapeli akamatwa na kadi 23 za benki

Pesa ni kitu kingine. Ujasiri wa kuweka ATM cards 23 kwa bibi. Hapana aisee huyu dada akapimwe mkojo.
 
Hii habari haijakaa sawa haiwezekani kadi zote hizo zikaifadhiwa kweny uke labda mseme alikua ameifadhi ndani ya chupi
 
Vp alivoitoa uliinusa
Hahaha mkuu
Ilikua hivi,hiyo siku kulikua na ukaguzi wa halaka,ile wameshuka tu kwenye school bus wakaambiwa watulie wasachiwe,mimi nilikua nyuma yake nikaona amefanya kama anachomekea shati akaibana simu katikati ya matako na alikua nayo makubwa tu
 
Mtuhumiwa huyo alikamatwa na askari wanaolinda Benki hiyo na alipopekuliwa alikutwa na ATM kadi 23 za watu mbalimbali za benki tofauti tofauti zikiwa katika pochi yake huku akiwa amezificha katika sehemu zake za siri ukeni.
Tangu utoto tunafundishwa eneo hilo ni maalumu halitakiwi kufanyiwa mambo mengine zaidi ya matumizi yaliyokusudiwa, huyu sasa anafanya eneo hilo kama strong room, anawezaje kutembea na hivyo vipande vya plastic 23 katika slot yenye 0 mm
 
Ndugu yangu hiyo unatafsiri wewe! Kwa hiyo sehemu za Siri maana ya ndani ya chupi?
Hujasoma habari YOTE au kilaza ubongo WAKO mgumu kuelewa hizo kadi ziliwekwa KWENYE pochi then akazificha KWENYE sehemu za siri yaani NDANI ya chupi
 
I hope hizo ATM tayari ziko blocked, manake with those details it is enough kwa mwizi kuchukua pesa kwenye account hata bila three digits at the back
 
Alizificha kwenye chupi au "Ukeni" kama ulivyosema?? Nawaza tu hiyo mikadi yote ndani ya kipochi halafu iingizwe ikulu kweli muumba kaumba. Halafu anatembea njiani bila shida!!! Nawaza tu
 
Alizificha kwenye chupi au "Ukeni" kama ulivyosema?? Nawaza tu hiyo mikadi yote ndani ya kipochi halafu iingizwe ikulu kweli muumba kaumba. Halafu anatembea njiani bila shida!!! Nawaza tu
Na bado atalalamika vidume wana vibamia wkt kwny mbunye yake zinaingia cards 23.
 
Na bado atalalamika vidume wana vibamia wkt kwny mbunye yake zinaingia cards 23.
Sikiliza; Ziwe zimenyooka vizuri ili zisijikunje mashine ikazikataa. Upana wake wote na urefu wake wote. Je, huyu akikutana na kibamia itakuwaje?? Nadhani atadhania ni njiti imemuingia
 
Taarifa ya kukamatwa kwa mtuhumiwa wa wizi kwenye mashine za kutolea fedha benki (atm) mnamo tarehe 25/10/2019 katika kituo cha polisi Mbagala maturubai, mzee Ernest Mika Sakala, ambaye ni afisa mwandamizi mstaafu wa jeshi la polisi alitoa ripoti kwamba tarehe 23/10/2011 majira ya 10:00hrs alibadilishiwa kadi yake ya benki ya crdb na kupewa ya mtu mwingine bila yeye mwenyewe kufahamu, wakati alipokwenda kutoa fedha kwa wakala wa benki hiyo ambaye anaendesha biashara yake maeneo ya Dar live Mbagala Zakh-em.

Kwamba siku mbili baadae aligundua kuwa kadi ya benki aliyo nayo siyo yake, na alipokwenda kufuatilia benki ya crdb Mbagala siku ya tarehe 25/10/2019 aligundua kuibiwa kwa fedha kutoka kwenye account yake kiasi cha tzs. 10,000,000/=. Fedha hizo zilitolewa kwa mawakala watatu tofauti siku ya tarehe 23 na 24 october, 2019. Upelelezi wa shauri hili ulianza kufanyika, ambapo mawakala ambao fedha zilitolewa na baadhi ya maafisa wa benki walihojiwa. Pia CCTV footages zilizomuonyesha mtuhumiwa wa kike aliyeonekana kutoa fedha kwa kutumia kadi hiyo iliyoibiwa kutoka kwa wakala mmoja wapo.

Wakati upelelezi ukiendelea, tarehe 19/11/2019 katika benki ya crdb Mbagala wakala mmoja akiwa katika maeneo ya benki hiyo alimtilia shaka dada mmoja aliyeonekana kwenye atm za benki hiyo akijaribu kutoa fedha, na alipomsogelea na kuanza kumuhoji dada huyo alijaribu kukimbia, lakini aliweza kudhibitiwa. Polisi walipewa taarifa na bila kuchelewa polisi walifika eneo hilo la benki na kumkamata dada huyo.

Alipofikishwa kituoni na kupekuliwa, alikutwa na jumla ya kadi 23 za watu na benki tofauti akiwa ameziweka kwenye kipochi kidogo na kuzisokomeza ndani ya uke wake. Mojawapo ya kadi alizokutwa nazo ni ya mzee Ernest Mika Sakala. Kadi hizo zipo katika mchanganuo ufuato:

1. CrdB- kadi 07

2. Nmb- kadi 06

3. Nbc- kadi 02

4. Amana- kadi 02

5. Posta- kadi 02

6. Acb- kadi 01

7. Stanbic- kadi 01

8. Dtb- kadi 01

9. Equity- kadi 01

Katika mahojiano, mtuhumiwa huyo ameeleza kwamba yeye na watuhumiwa wenzake, ambao bado tunawafuatilia, wamekuwa waki-target watu wenye umri mkubwa (wazee) na wastaafu ambao huenda kwenye mashine za atm na kushindwa kuzitumia hivyo kuomba msaada kwa mtu wa pembeni. Kwamba wakati wanapowasaidia kutoa fedha, kwa kutumia ujanja wanakariri namba za siri, na baada ya kufanya muamala wanachukua kadi ya muhusika na kuificha, na kumueleza kuwa kadi imemezwa kwenye mashine. Hivyo basi, victim anapoingia ndani ya benki kufuatilia kadi yake, wao wanaondoka na kadi kwenda kwa wakala yoyote yule au kwenye mashine nyingine ya atm kuangalia salio na kuanza kutoa fedha.

Mbinu nyingine ni kuwafuatilia wateja wanaokwenda kutoa fedha kwa mawakala, na kukaa pembeni yao na kuchungulia pindi mteja anapoingiza namba yake ya siri. Baada ya hapo mteja akishapewa fedha na wakala anakuwa busy kuweka mfukoni fedha alizopewa, huku kadi yake akiwa ameicha mezani, na hapo ndipo wanatumia mbinu ya kumbadilishia na kumuwekea kadi ya mtu mwingine ambayo tayari fedha zake wanakuwa walishaziiba. Amekana kushirikisha afisa yeyote wa benki au wakala katika kufanikisha wizi huo. Upelelezi bado unaendelea.

=========

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM KUIMARISHA ULINZI KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limejipanga vizuri kuhakikisha uchaguzi wa Serikali za Mitaa unafanyika kwa amani na utulivu.
Ndugu wana habari, tarehe 24/11/2019 ni siku ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji hivyo basi sisi kama Jeshi la Polisi tutaimarisha ulinzi maeneo yote ya Jiji la Dar es Salaam,
katika vituo vya kupigia kura, ofisi zote za vyama vya siasa na ofisi zote za watendaji wa kata.
Aidha Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linatoa onyo kali kwa mtu yeyote au kikundi chochote cha watu watakao jaribu kuvuruga amani jeshi la Polisi halitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria.



KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA WA WIZI WA FEDHA KWENYE MASHINE ZA KUTOLEA FEDHA (ATM) NA ATM KADI 23
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Bi Halima Juma (23)Mkazi wa Chalinze kwa tuhuma za wizi wa fedha kwenye mashine za kutolea fedha (ATM)
Mnamo tarehe 19/11/2019 katika benki ya CRDB tawi la Mbagala akiwa katika ATM hizo, aidha alimtilia mashaka binti huyo aliyekuwa kwenye chumba cha ATM ya benki hiyo akijifanya kuwasaidia wazee na wastaafu wasiojua kutumia ATM mashine vizuri, lakini lengo lake ni kuchukua namba za siri za wastaafu na wazee hao na kisha kuwabadilishia ATM kadi zao na baadaye kuwaibia fedha kwenye akaunti zao kwa kutumia kadi halisi za wahusika baada ya kuwabadilishia kadi na kuchukua namba za siri.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa na askari wanaolinda Benki hiyo na alipopekuliwa alikutwa na ATM kadi 23 za watu mbalimbali za benki tofauti tofauti zikiwa katika pochi yake huku akiwa amezificha katika sehemu zake za siri ukeni.
Kadi hizo ni kama ifuatavyo;
1.CRDB kadi 07
2.NMB kadi 06
3.NBC kadi 02
4.AMANA kadi 02
5.POSTA BENKI kadi 02
6.ACB kadi 01
7.STANIBIC kadi 01
8.DTB kadi 01
9.EQUITY kadi 01
Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na atafikishwa mahakamani hivi karibuni.


TAHADHARI YA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA JIJINI DAR ES SALAAM.

Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es salaam linapenda kutoa tahadhari kwa wakazi wa jiji la Dsm wote kuwa makini kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha ili kuepukana na majanga yanayoweza kuepukika. Hivyo wananchi wote wanatakiwa kuwa makini na watoto wadogo wanaohitaji uangalizi wa karibu, pia kujiepusha kupita kwenye maji ya mito midogomidogo au madimbwi ambayo yanaweza kuhatarisha usalama wao.
Aidha hadi sasa zimepokelewa taarifa za watu wawili kufariki dunia kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

LAZARO .B. MAMBOSASA – SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.

22.11.2019

View attachment 1268455View attachment 1268457
Unaenda kuiba umevaa T-shirt imeandikwa lost ulitegemea nn
Hongera kwa wakala na jeshi la police kwa kazi nzuri
 
Tunapoelekea Kwenye Sikukuu Za Mwisho Wa Mwaka
Watu Umakini Uongezeke Mara Dufu
 
Back
Top Bottom