Chukua kadi sasa ama acha kabisa-with us or with them-red line

Mkwawa

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2011
Messages
1,336
Points
1,500

Mkwawa

JF-Expert Member
Joined Jun 8, 2011
1,336 1,500
Kamati kuu inatakiwa kutoa maamuzi ya mwisho kuhusu hawa wasaliti haraka iwezekanovyo. Siku kumi na nne zikiisha tutangaziwe hukumu. Kuendelea nao au kutoendelea lazima ijulikane mapema asubuhi.

Kuwaacha ni hatari sana, kama wametumwa na ushahidi ni wakutosha lazima waondoke, historia ya siasa za Tanzania ukisha kula rushwa huwezi kuacha, ukinunuliwa umenunuliwa. Kama nia yao ilikuwa kuisanbaratisha CDM watafanya kila mbinu wabaki, hata kupiga magoti watapiga kwani wanataka kumalizia mission.

Nikisikiza kauli za ZZK mara baada ya kusimamishwa na kuachishwa uongozi, utaona jinsi alivyo arrogant. Anaongea kama vile hakuna wa kumfanya lolote. Watu kama hawa wakipewa madaraka makubwa ndio walochini watajua mlango ukoje.

Maneno yake yote ukimsikiliza kwa makini ni ya kizandiki, ugomvi, kuuwa chama na kudharau harakati kazi za wanachama zaidi mamilioni.

Ukiwaacha kwasasa wanahasira mara kumi wanatamani waone chama kimekufa ili wafurahi. Nia yao ni kumkomoa mtu hivyo hawaoni umuhimu wa CDM kwani tayari wamejijengea katawi NCCR via CCM. Mission ya ZZK ni kusaidiwa na CCM kwenda NCCR kumkimbiza Mbatia na kuwa mwenyekiti, ila lazima wakidhoofishe CDM ili wakifika kule wawe chama kikuu cha upinzani. AKili hizo mfadhili Magamba line.

ZZK anaamini atakujua kuwa Raisi wa TZ ila lazima apitie misukosuko, ila ninamwambia ZZK huwezi kufika kileleni kama huheshimu wapiganaji wenzeko, kama kwa Kafulila na kwako vivyo hivyo alivuliwa vyeo CDM kaenda NCCR katishia nyau watu kala kadi, mbunge wa mahakama. Na wewe hata Magamba watakucheuwa tu. Cant sit still.

Dr Kitila kachemsha sana, namba moja kujiandikia hekaya ya kipuuzi yenye personal attacks imemshushia hadhi sio tu ya PHD yake bali heshima mbele za jamii. Unaweza kumpinga mtu tena kwa maandishi bila lugha ya matusi. Leo usamehewe ufanye kazi na nani?????

Critics nzuri hazina personal attacks, wangeshambulia cheo sio mtu, ile ilionyesha mambo binafsi zaidi kuliko siasa. Sijui wafuasi wa hawa watu wakoje.

Usomi ni pamoja na kujikomboa kifikra na kiakili lazima utambue hadhira yako na kila unachofanya ujue risk zake na faida. Watu wanne wameshindwa kutunza siri ya kurasa tano au sita kweli leo wangepewa chama wangeweza kututunzia siri??

Eti ZZK anasema yeye angefaidika tu na waraka. Je walipowashauri madiwani wa Arusha waidindie kamati nani alikuwa anafaidika?

Ukweli kabisa waraka na matendo ya ZZK na Dr K ni mwendelezo wa maisha na uongozi wa Daruso na mambo ya panch. Walifikiri wako chuo bado waende usiku wakaweke yale mabandiko asubuhi watu walie.

Akili ya yakiuwanafunzi kwamba mapinduzi ni kulala na kuamka tayari ZZK mwenyekiti, Kitila katibu Mkuu, Mwigamba Makamu mwenyekiti chama kinasinyaa tunakula fungu kutoka Magamba for rest of our time just kama Mbatia. Kalagabahao.

Hatumchukii ZZK kwa sura yake la hasha bali tabia yake ya uchu mpaka awe tayari kuuwa chama. Ni kweli mzuri kwa macho ya magamba wamchukue wakanywe naye chai, au wambebe wakaishi naye ikulu, wampe uwaziri mkuu au wampe agombee uraisi au uenyekiti CCM aende tu. CDM hatuhitaji vurugu sasa tunaka kushinda kwanza.

Makamanda wote kazi moja kujenga Chama.

Nilimpenda sana Raisi wa Marekani Bush JR, alikuwa harembi upende usipende akisema anafanya. Sasa CDM kamati kuu tunataka majibu, je tununue snake repellant tuanze kujipuliza au mnamtoa nyoka ndani ya chumba????

Chief Mkwawa
Nilimpenda sana ZZK nilimwita Kamanda- tulipanda naye majukwaa mengi tulikubaliana usaliti hauna nyumba ya kujificha. Hoja hujibiwa kwa hoja kwanini umetusaliti sisi wanachama? Dhambi hii hutasamehewa popote.
 

Forum statistics

Threads 1,388,964
Members 527,839
Posts 34,015,160
Top