Chukua hatua: Vitanda vya sita kwa sita chanzo cha ndoa kuvunjika! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chukua hatua: Vitanda vya sita kwa sita chanzo cha ndoa kuvunjika!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mohamedi Mtoi, Oct 15, 2012.

 1. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #1
  Oct 15, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Enzi zetu sisi ndoa zilikuwa hazivunjiki! Mimi na bibi yako tumekuwa tunagombana lakini usiku ilikuwa lazima tupatane! Tukiamka asubuhi tu wapya mapenzi yanaendelea kama vile hakuna lililotokea jana.

  Pamoja na mapenzi ya dhati yasiyo angalia kitu kama yenu kitanda chetu cha kamba cha futi tatu kwa tano kimetufanya tumekuwa karibu sana! Tunagusana hata kama tumeudhiana, bibi yako anasikia harufu ya jasho langu na mimi nasikia la kwake, akiguna namskia akigeuka ananigusa, usiku kucha joto lake joto langu. Maisha yamekuwa ya raha mustarehe.

  Nyie ndoa zenu hazidumu kwa sababu ya vitanda na sio wavumilivu, lakini wengi wenu mnaingia kwenye ndoa mkiwa tayari mmesha wahi kupenda sana watu wengine kuliko mlio waoa na hivyo inawawia vigumu kuwasahau kirahisi.

  BABU HAPA KWENYE VITANDA PAKOJE?!

  Nyie vitanda vyenu ni sita kwa sita, ama tano kwa sita! Hivi vinamkaribisha shetani! Mwenyezi mungu anasema "wawili wakishikamana yeye anakuwa kati yenu" vitanda vyenu vinavunja ndoa zenu!
  Unakuta mmeudhiana, vitanda vyenu vya sita kwa sita wakati wa kulala mmoja yuko kule mwingine yuko huku katikati nafasi! Hapo katikati analala "shetani" upande wa kule mke anamuwaza mtu wake (john/ally) upande wa kule mume ana muwaza mtu wake (maria/asha), hawagusani, hawapeani joto, hawapeani harufu za kimahaba maana nafasi ya kitanda inawapa jeuri. Hata wakati wa kugeuka una weza kugeuka bila hata ya kumgusa mwenzako! Hili ni tatizo kwa ndoa, ndio maana mnaachana maana hamko pamoja na Mungu mnapo kuwa vitandani. Mnamruhusu shetani katikati yenu! (Hapa nikakumbuka kale ka mstari ka umombo kanako sema 'nearest is dearest')

  Nakushauri mjukuu wangu! Kama unataka kuendelea kuishi na mkeo hadi uzee kama wangu achana na uleo! Haraka sana fanya hima ubadirishe kitanda.

  ** Haya yalikuwa ni masimulizi ya babu yangu mmoja niliyekwenda kumtembelea kijijjini kwetu, kama kawaida siku ipoteza fursa nikampiga na yeye darasa la M4C, kwa sasa anamiliki bendera na kadi ya chadema **

  ONYO.
  KITANDA CHA SITA KWA SITA NI HATARI KWA NDOA YAKO.
   
 2. harakat

  harakat JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  J3 inaanza kwa raha nikiwa kwenye 5 kwa 6 nimekumbatia laptop
  nacheka mwenyewe jf kiboko
   
 3. gobore

  gobore JF-Expert Member

  #3
  Oct 15, 2012
  Joined: Aug 17, 2009
  Messages: 730
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Hapo kwenye mapenzi ya mara ya pili na kutowasahau wapenzi wa zamani nakuunga mkono. Ndoa za zamani pia zilidumu kwasababu ya "innocence" ya first xperience kwa wapendanao wanakua hawajaonja ladha nyingine
   
 4. akohi

  akohi JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2012
  Joined: Jul 13, 2012
  Messages: 761
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 60
  Mkuu naunga Mkono hoja, maana ki ukweli hayo ndo Maisha na athari za dot com na mbaya zaidi cku hizi kuna smart phones, laptops, palm tops, nk ambazo mara nyingi watu tumekuwa bize sana navyo. Babu zetu hawakua na vitu mbadala vya Kuwa keep busy na Kuwa liwaza.
   
 5. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 199
  Trophy Points: 160
  sipendi kubanana mie....baada ya kale kamchezo kila mtu na upande wake...though hii mada ishajadiliwa humu jamvini...
   
 6. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #6
  Oct 15, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Ndoa nyingi sasa hivi zimekuwa za jumapili jumatatu zimesambaratika, ipo ndoa ya jamaa yetu mmoja aligharimu karibu milioni 20 baada ya miezi mitatu chali! Ukimsoma babu katikati ya mistari utagundua mengi kuwa haongelei vitanda tu!
  Bali hata ukaribu wa kusoma na kujuana vyema tabia zetu. "Yeye anasikia harufu yangu na mimi nasikia harufu yake, joto langu, joto lake" hapa ndio hekima ilipo lala. Usiliwaze kama joto na mguno wa kawaida tu!

  There is something when you read between the lines!
   
 7. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #7
  Oct 15, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Six by Six inawezakuwa...nakubaliana na hoja, . mohamedi.Mtoi, nimefurahi kwa hilo la M4C
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Mahmetkid

  Mahmetkid JF-Expert Member

  #8
  Oct 15, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 557
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Muda mwingine hata kitanda kiwe 3 X 3 mkigombana na mmoja kati yenu hakikataa kuwa chini ya mwenzake timbwili litaendelea tuu.
   
 9. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #9
  Oct 15, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Umenena mkuu! Big up!
   
 10. cutetoto

  cutetoto Member

  #10
  Oct 15, 2012
  Joined: Oct 4, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ya kweli kabisa kah...
   
 11. Tigga Mumba

  Tigga Mumba JF-Expert Member

  #11
  Oct 15, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 747
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Ni ukweli aisee
   
 12. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #12
  Oct 15, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Kila fursa inapo patikana inatumika mkuu. Ukipewa somo la unyumba akifikia hitimisho una shusha somo la M4C. Wewe una faidika na yeye anajiunga kwenye m-bus mkubwa wenye plate namba T2015CDM
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. K

  Karug JF-Expert Member

  #13
  Oct 15, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 332
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kumbe kuna watu katika ndoa ambao wana vitanda vya 3x6 ambavyo hawajawahi kuviona vikuuubwa kuliko kipimo cha kitanda chenyewe...

  Kumbe hujawahi kuthuthiwa kitanda wewe....
   
Loading...