Chukua hatua, kila ugonjwa una kinga zake

XhosaVica

Senior Member
Sep 29, 2020
132
133
Ikiwa katika wave ya ugonjwa wa shida ya kupumua tuliandaa miongozo ya Wizara ya Afya( ambayo haijafutwa kwa miongozo mipya) ikiwa ni pamoja na kunawa na maji tiririka, kuvaa vifunika pua vya mdomo na pua-barakoa, kutokua na mikusanyiko isiyo lazima) mazoezi na kula vyema kwa nini inakua ngumu nyakati hizi. Tuliweza kusali kitaifa. Tusiweke afya zetu na tuwapendao rehani. Tukiweza tuanze na sala ya taifa bila hofu huku tukizingatia.

Kila ugonjwa una kinga zake, mfano tunalala kwenye net kujizuia na mbu. Tunanawa mikono tukitoka chooni kuzuia magonjwa ya kuhara.
Tuchukue hatua kila mmoja, siasa si suluhisho la kila tatizo. Ni wakati wa kutotoa lawama bali kuchukua hatua dhabiti.
 
Hatua!Zinachukuliwa sana,mamlaka haziwezi kukwepa jukumu lake la kulinda raia dhidi ya maadui na majanga.Huu ni wajibu wa kikatiba wala tusipepese maneno.

Kama mtu mmoja mmoja atachukua hatua lakini wengi wakapuuza kwakuwa mamlaka zimepuuza uwepo wa ugonjwa tutaangamia tu.
Huwezi kusafisha tope ukitumia maji ukiwa matopeni ukategemea kuwa msafi
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom