KadaMpinzani
JF-Expert Member
- Jan 31, 2007
- 3,715
- 92
Mbowe tuachie chama chetu
March 12, 2008
Baada ya yeye mwenyewe kukwepa vikwazo kadhaa vya kujibu hoja na mambo mengine anayoulizwa kwa njia ya mtandao au kwa simu za mkono kwa muda mrefu , sasa limekuja swala lingine nalo ni la yeye kufeli masomo yake katika chuo alichokuwa ameenda kujiendeleza .
Kufeli masomo sio kitu kipya hapa duniani au popote pale au kushindwa kitu chochote sio kitu kigeni lakini inategemeana umeshindwa au kuanguka kwa sababu zipi haswa , je kuanguka kwako kutaathiri vipi morani ya wale waliochini yako au unaotarajia kuongoza hapo mbeleni .
Na ndio hapo tunapokuja katika mada yenyewe ya jioni ya leo , habari zinazozidi kusambaa sasa hivi katika vyombo vya habari na duru zingine za habari zinasema kwamba Freeman Mbowe mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani chadema amefeli masomo yake ya chuo .
Kwa kuwa amefeli masomo ya chuo na amekuwa akifeli katika mambo mengine mengi katika uongozi wake ndani ya chadema basi ni vizuri sasa aachie ngazi hata katika chama aachie wale wengine wanaoweza kufanya mambo haya zaidi yake .
Kwa kuanza tu kati kati ya mwaka jana kulitokea vijana machachari katika chadema wakimshutumu mbowe binafsi kwa mambo mbali mbali yaliyochangia katika kukidhoofisha chama yeye kama mwenyekiti hakuwahi kutoa kauli yoyote kuhusu shutuma zile alikaa kimya kama vile hakuna kinachoendelea .
Shutuma zilizotolewa ni pamoja na ukabila ndani ya chama chenyewe pamoja na kuchaguana kwa kujuana bila usawa wowote ule , na sakata hili mpaka leo bado linaivuruga chadema na wanachama wake wengi haswa wale masikini wasiokuwa na uwezo wa kusema .
Katika harakati za uchaguzi wa kiteto napo mwenyekiti huyu ameshindwa kuonyesha cheche zozote badala yake wakashindwa kwa kishindo na baadaye akaja kufeli mitihani yake ya chuo .
Ushauri wangu ni kumuomba ndugu mbowe aachie ngazi katika chadema sasa akafanye mambo mengine naamini katika chadema wako watu wengi wenye uwezo kuliko yeye na waliowazalendo zaidi katika chama na nchi yao ya Tanzania kuliko yeye