CHuji kufanya majaribio Galatasalay

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
734
Kiungo wa kutumainiwa wa Yanga na Taifa Stars anatarajiwa kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa kwenye kilabu cha Galatasalay cha Uturuki mara baada ya ligi kuisha.
Chuji kama atafanikiwa ataungana na wachezaji nyota kama Nonda Shabani na Milan Baros, kila la kheri chuji na inatia faraja kuona sasa wachezaji wetu wanaanza kupata mianya ya kucheza ULAYA.
 
Kila la kheri Chiji..."Lugha ndio huwa inawaangusha...komaa kijanautapita tu...
 
Chuji ni moja wa viungo bora kabisa Tanzania kwasasa kusema kweli na hata katika mchezo wa juzi kati ya Yanga na Al-Ahly alicheza mchezo mzuri sana.KILA LA KHERI CHUJI.
 
Ninamtakia kila la heri Chuji.
Ushauri wangu kwa Chuji ni kama ifuatavyo.
Nidhamu nje na ndani ya uwanja ni muhimu sana kama atataka kuendeleza kipaji chake.
Bidii katika mazoezi bila kuwa na visingizio.
kukwepa kutumia madawa ya kuongeza nguvu.
Kukwepa kutumia madawa ya kulevya.
Naomba kuwasilisha.
 
Nani kawadanganya?Wangapi wameshindwa hata soka la uarabuni japo si gumu kama ulaya?Msijifariji enyi wapenzi wa yanga.Huyo Chuji kashindwa kuonesha kiwango kule Cote d'voire.Au ni majina ya timu yamefanana tu?
 
Mkuu Isaac Chuji hakucheza mechi yoyote ile Cote d'voire, uwezo wa soka anao. Hili ndio tatizo letu watanzania bado tunasema hatuwezi, tutaweza lini????? Mpeni baraka kijana akajaribu bahati yake, kama wataridhika nae watamchukua kama hawatamkubali atarudi kwetu kupiga makelele na akina Maximo.
 
Nani kawadanganya?Wangapi wameshindwa hata soka la uarabuni japo si gumu kama ulaya? Msijifariji enyi wapenzi wa yanga. Huyo Chuji kashindwa kuonesha kiwango kule Cote d'voire.Au ni majina ya timu yamefanana tu?

Kila la heri Chuji. Tusisahau kwamba alijifunzia kucheza mpira na kupatia jina alipokuwa msimbazi.
 
Mkuu Isaac Chuji hakucheza mechi yoyote ile Cote d'voire, uwezo wa soka anao. Hili ndio tatizo letu watanzania bado tunasema hatuwezi, tutaweza lini????? Mpeni baraka kijana akajaribu bahati yake, kama wataridhika nae watamchukua kama hawatamkubali atarudi kwetu kupiga makelele na akina Maximo.
...Hakuna cha kumpa baraka aende akakaze msuli apate nafasi apige soka kwa faida yake na ndugu zake. Ulisikia wapi midomo mingi ikitoa baraka unafanikiwa??
 
Mijitu yenye Roho Mbaya Na Roho Za Kwanini Utaijuwa Tu Kuanzia Hapa Katika Soka. Sasa Soka Tu Watu Washakuwa Mahasidi Kisa Nini?....Eti Ni Mchezaji Wa Zamani Wa simba Na Ni Mchezaji Nyota Tegemo wa Yanga Loh!!! Ndio Maana Hatuendelei Tutabaki Kudanganyana kuwa Kuna Mchezaji wet anaitwa machupi Anacheza Denmark ktk Mtando hutapati source......
 
Huyu bwana Chuji si ni Mchezaji Nyota Tegemo wa Yanga? Si Ni Mchezaji Wa Zamani Wa Simba? Sasa hizi lugha za ''mijitu, mara roho mbaya, mara ndio maana hatuendelei'' zinahusika vipi wakati watu wanamtakia tu heri mtanzania mwenzetu?
 
Nani kawadanganya?Wangapi wameshindwa hata soka la uarabuni japo si gumu kama ulaya?Msijifariji enyi wapenzi wa yanga.Huyo Chuji kashindwa kuonesha kiwango kule Cote d'voire.Au ni majina ya timu yamefanana tu?
usikurupuke wewe Soma Kwanza hii Comment inaashiria nini .....Ndio Uniulize
 
All the best Chuji ,kizazi cha sasa wana nafasi kubwa ya kupata nafasi ya kwenda ulaya waongeze bidii
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom