Chui azua taharuki Wilayani Hai, ajeruhi watu kadhaa

Itakuwa Chui wa Sabaya huyu alitumwa kumuua Mbowe alipomkosa kisa yupo Central akaamua kumalizia Hasira zake kwa wanachadema
 
Lakini si vizuri kuuwa wanyama,wanyama nao ni viumbe hai kama sisi nao wana haki ya kuishi
 
Leo Asubuhi kuna Chui ameleta fujo na kujeruhi watu kadhaa.

Askari wa wanyama pori wafanikiwa kumuua.

Majeruhi wanne waliojeruhiwa na Chui huyo ni pamoja na
1.Emmanuel Urassa(37) ambaye amejeruhiwa maeneo ya usoni na mkononi,

2.Jesca Nkoo(21) amejeruhiwa usoni na mgongoni,

3. Urusula Cosmas (26) amejeruhiwa kichwani na puani na

4. Maliki Sakia (31) aliyejeruhiwa kichwani na mdomoni.

Wanapatiwa matibabu hospitali ya Wilaya ya Hai.

View attachment 1957264

View attachment 1957265
Iteni wataalamu wa maabara ya mifugo wachukue sampuli, kuna uwezekano huyo chui akawa na kichaa cha mbwa (rabies)....pia waliojeruhiwa wahakikishe wanapewa kinga ya kuzuia kichaa cha mbwa.
 
Iteni wataalamu wa maabara ya mifugo wachukue sampuli, kuna uwezekano huyo chui akawa na kichaa cha mbwa (rabies)....pia waliojeruhiwa wahakikishe wanapewa kinga ya kuzuia kichaa cha mbwa.
Wahusika wameshashughulikia
 
Lakini si vizuri kuuwa wanyama,wanyama nao ni viumbe hai kama sisi nao wana haki ya kuishi
Ni kweli wana haki ya kuishi ila sehemu sahihi.
Hata wewe ukikutwa mbugani bila mpangilio utapigwa faini
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom